Bongo kunakera!

Alikuwa na nguo zaidi ya moja zenye thamani ya shilingi 150,000, na siyo nguo moja.

Alianza kwa kusema alikuwa na nguo ya thamani ya 150,000 hata mimi mwanzoni niliewa hivyo mpaka mwisho wa story.

Mimi nadhani tatizo sio BONGO, exposure wala LOW LIFE kama wengine wanavyodai.

Napenda kuamini kuwa hao wenye maduka wana exposure ya kutosha, nadhani TATIZO NI CHEAP LABOUR. suala la customer care is sometimes a common sense and sometimes a person need to undergo some training, kama wenye maduka wanashindwa kuwatrain wafanya kazi wao au kurecruit train employees kwa kuogopa kuwalipa mishahara minono tegemea treatment kama hizo.

Jaribu kuangalia customer care ya hotel tofauti tofauti hapa bongo utakubaliana na mimi, sometimes tusifuate MAJINA ungekuja dukani kwangu ungepata the quality stuffs na lugha laini mpaka ukafikiri uko mamtoni.

POLE SANA LAKINI.
 
Jamani kama wanaleta mapozi nenda Mchikichini,Manzese ,Ubungo kwa MACHINGA kuna pamba kali tu
 
ulifanya nini baada ya kujibiwa hivyo?

Nilimtafuta Meneja nakumweleza alichonijibu yule muhudumu, nilitaka angalau kibarua kiotee majani, au wampeleke training, au jamaa wampeleke back office aendee jikoni akae mbali nawateja, lakini kule jikoni naona angefanya madhambi zaidi...
 
Eti mtu unampa tiketi, anaigeuza geuza kama mtu anayeikagua noti halali, anaiangalia weee halafuu anakuuliza unaenda wapi? Huu si ndo ujinga ? Lakini akija 'mdhungu' anapita fastafasta..

limenikuna hili "UNAENDA WAPI?" Swali maarufu sana huku bongo. Niliwahi kuulizwa na askari mmoja swali hilo. Nilimuuliza, Ina maana unaniita kichaa sijui niendako? Niwashe gari nitoke nitokapo bila kujua naenda wapi? Akabaki mdomo wazi! lol
 
Wabongo ndivyo walivyo jamani, kuonyeshana ufahari na kujitanua ili waonekane bora zaidi ndo zao. Mbona hata nyie mlioko nje ya nchi mnafanya mambo ya ajabu kwa kutukanana kwenye mitandao kama zeutamu? Hasa wa kina dada mnapenda sana mashindano, badala ya kumind business zenu. Inawezekana huyu dada alionyesha nyodo flani ndo maana akafanyiziwa, maana sisi huku ukijadi kuleta ujanja wako lazima tukufanyizie. Hii ndo bongo bwana
 
Naamini katika suala hili polisi wetu hawawezi kutoa msaada. Nashauri kama kuna uwezekano lishikiwe bango ili hawa makaburu waweke taratibu nzuri za kuhudumia wateja. Katika vita hii mdau muhimu ni vyombo vya habari. Ikitoka mara kibao kwenye magazeti na media nyingine itasaidia.

Hata hivyo kama kuna mtu alisoma makala ya Makengeza wk 2 zilizopita kwenye gazeti la Mwananchi alisema TZ kila kitu ni kimeo. Mfano mtu anaanzisha biashara ya hoteli, anaajiri wafanyakazi wasiosoma (kimeo), kwa hiyo chakua kitakuwa kimeo na watoa huduma watakuwa kimeo. Hata hivyo naye atawalipa kidogo (malipo kimeo). Unaweza kuendelea hadi kila sekta!!
 
kote kote yapo mwenzangu ... mimi ndugu yangu yalinikuta sokoni .. yote kwaajili ya kiranga cha mwanangu cha kupenda zabibu .. basi nikaenda pale buguruni kuzinunua .. kufika meza moja nikakuta mwenye meza anapigastory na rafiki yake .. nikauliza zabibu bei gani .. nikaona kimya .. nikauliza tena .. yule jamaa akamgusa mwenzie akaambiwa unamteja ... akamwambia nimemsikia vizuri .. aaah achana nae .. bei ataiweza anazuga tu ... nilihamaki nikasimama pembeni nikajiuliza kwanini kanidharau kiasi kile .. sikukubali nikazunguka tena baada kama dakika kumi nikarudi palepale nikamuuliza bei akaniambia .. nikamwambia sinunui kwako kwani mwanzo ulinidharau sasa nanunua kwa mwenzio .. basi kwa hasira nilinunua kama sina akili nzuri .. kapu tele japo budget yangu ilivurugika sikujali nilihakikisha namkomesha kwa makusudi kila baada siku chache naenda meza jirani nanunua kwa mbwembwe .. mpaka leo ananiheshimu
 
Hii kadhia inanikumbusha siku moja nilikuwa nakwea pipa la madachi, sasa wale wabongo na njaa zao kwenye ukaguzi wa tiketi wanakuja na maswali meengi utadhani upo fuleni ya kuingia sijui mbinguni? Lakini niligundua kinachowasumbua ni kijiba cha roho tu hawana la ziada. Eti mtu unampa tiketi, anaigeuza geuza kama mtu anayeikagua noti halali, anaiangalia weee halafuu anakuuliza unaenda wapi? Huu si ndo ujinga ? Lakini akija 'mdhungu' anapita fastafasta..

Mdharau kwao ni mtumwa, Kila mahali ulimwenguni kuna ubaguzi na tabia za ajabu ajabu, it better evaluation zenu zisiwe ni sifa za kuwapa wabongo wote nyie WATUMWA.
 
Supa maketi nyingi zinatangazo kuwa hauruhusiwi kuingia na begi au mkoba. Lakini sheria hii inawahusu kwa kiasi kikubwa watu weusi. Ni mara chache mtu asie mweusi kuambiwa leta begi tukuwekee! Na mweusi ukiingia basi wale wafanyakazi wanaganda na wewe ile mbaya ati utadokoa kitu!

Hapo Mlimani City kuna duka moja ambalo ukiingia na kutoka unapekuliwa utadhani kuwa uko kwenye mgodi wa Tanzanite!

Ni sisi ndiyo tunaolea hii tabia. Unapofanyiwa hivi piga kelele kwa sauti kubwa na dai kuonana na bosi mkubwa. Ikishindikana, tuanze tabia ya kususia sehemu zote zenye reverse discrimination. Pamoja na hayo tusambaze taarifa kwenye balozi zote na mashirika yote ya kigeni maana wafanyakazi wao ndiyo wanaoabudiwa.

Tukiwagusa kwenye mifuko, pengine watashika adabu.
 
Nilishawai kwenda slipway nika order supu ilivyo fika nikagundua kulikua na inzi wawili kwenye supu, hasira zikanipanda kishenzi nikamwita muhudumu kumwambia kwamba kuna inzi kwenye supu, nikajibiwa "Nikusaidie kuwatoa???".....
...Short and clear answer!!! I like this.................
 
WANDUGU,
1.Hili ni tatizo la kweli bongo na hii tabia inapofanywa na wabongo wenzetu inakera kupita kiwango.Sijui ni lini tutajifunza kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe! Inachekesha hasa pale unapokuwa umemwalika mzungu for dinner/lunch kwenye restaurant halafu inapoletwa bill anapelekewa mzungu! Ni kwamba watz siye hatuna culture ya kula kwenye restaurant zinazoeleweka au?

2.Customer care ni eneo ambalo linahitaki kufanyiwa kazi sana kwenye biashara.Nadhani wajasiriamali mlioko humu ndani mnaweza kujipatia ujiko endapo mtajikita katika kutoa mafunzo.Tanzania mteja siyo mfalme bali mhudumu wa duka/restaurant etc ndiye mfalme.

3.Tusisahau pia kuwa nchi yetu ilipitia vipindi vigumu vya shortages za bidhaa, watu wakajenga fikra kuwa ili upate bidhaa unahitaji kusujudia muuza duka hata kama unalipia.Hili shombo bado limebaki ..sijui litasafishwa kwa sabuni gani.
 
limenikuna hili "UNAENDA WAPI?" Swali maarufu sana huku bongo. Niliwahi kuulizwa na askari mmoja swali hilo. Nilimuuliza, Ina maana unaniita kichaa sijui niendako? Niwashe gari nitoke nitokapo bila kujua naenda wapi? Akabaki mdomo wazi! lol

Mkuu Mangi,

Hili swali la 'UNAENDA WAPI' wakti tiketi inaonesha destination ni la kipuuzi kwa kweli .. Wanabahati nimempokea Yesu wajinga wale..
 
Mdharau kwao ni mtumwa, Kila mahali ulimwenguni kuna ubaguzi na tabia za ajabu ajabu, it better evaluation zenu zisiwe ni sifa za kuwapa wabongo wote nyie WATUMWA.

Sikiliza boss,

Hapa unataka kuchanganya mambo..Hapa tunazungumzia poor or worst customer care service ktk bongo yetu ..we unaleta habari za utumwa..wapi na wapi boss?

Hata kama kuna ubaguzi ndo tusiukemee? Kuna baadhi ya sehemu (nje ya Tz) unakuta mfanyakazi tu wa serikali (non-profit) anakuhangaikia utafikiri mwana wake wa kukuzaa seuze sehemu za kibiashara ndo kiboko, utahangaikiwa mpaka utamani kurejea japo kuwasalimu..
 
Wakuu achaneni na hiyo ya ukaguzi wa tiketi na visa uwanja wa ndege ambayo huwa inanibughuzi kinoma, mimi nina experience na walinzi wa bank ya Barclays Arusha...mwaka jana nilikuwa A-town kwa ka likizo kafupi. Nikawa nataka ku withdraw ka pesa kadogo kutoka kwenye account yangu.nikaona ngoja nitumie ATM za Barclays Bank kwa sababu kuna mtu aliniambia wana charge fees ndogo. Bahati mbaya sana au nzuri sana...wakati ninaenda Bank nilikuwa nimeandama na mzungu volunteer wa PeaceCorp. Kwa nini walinzi wasinizuie kwenye gate..wamruhusu mzungu kwenda...hata baada ya kuwaambia kuwa mimi ndio ninayetaka kutumia huduma ya ATM...wakasema ATM zao zina charge fees kubwa kwa Tembo kadi kwa hiyo I am better off kwenda CRDB Clock Tower. Yaani walishakuwa na assumption kwamba I am a Tembo Card holder kwa sababu ni mbongo. Nikashindwa kuvumilia nikawaambia waniitie manager kama hawataki niende kutumia ATM, baada ya kuona hivyo wakaniachia niende, huku nyuma yule mzungu akaanza kupiga nao kiswahili akawaambia kuwa mimi ninaishi Marekani. Baada ya kumaliza haja yangu wakati narudi gateni...jamaa wakawa wananichangamkia kinoma...nikaona hawa washenzi tu. I was so pissed kidogo niandike barua kwenye mgmt ya hiyo bank.

teh teh teh..Pole sana mkuu..

Huu ni mfano tosha wa watu kuogopa rangi .. Dah wabongo nuksi asee..
 
Bongo Darisalamaaa...Kuna kale kasuper market ka Shoprite kapo JM Mall, Samora Ave wale nao ni hatari, kuna siku nienda shopping ya kizushi pale, nikanunua vitu kulingana na mfuko wangu, Kasheshe wakati wa kulipa, Mayonnaise nilioina inameandikwa bei 3000, kwenye kulipia risiti likuwa 3800 TShs, Wine 12,000 kwenye display kwenye kulipia 15,000 Shs kifupi kila kitu bei waliodisplay siyo unayo lipia. Nilikuwa mkali sana, nikaomba aje manager wao mdosi nikamwelewesha na tukaenda cross cheki naye...akasema samahani sana nikalipishwa bei halali nilisevu kitu kama 40,000 hivi...sasa wale wasiocross check huwa wanalipa tu na kuibiwa....Bongo inakeraaa si kidogo.
 
Bongo Darisalamaaa...Kuna kale kasuper market ka Shoprite kapo JM Mall, Samora Ave wale nao ni balaa, kuna siku nienda shopping ya kizushi pale, nikanunua vitu kulingana na mfuko wangu, Kasheshe wakati wa kulipa, Mayonnaise nilioina inameandikwa bei 3000, kwenye kulipia risiti likuwa 3800 TShs, Wine 12,000 kwenye display kwenye kulipia 15,000 Shs kifupi kila kitu bei waliodisplay siyo unayo lipia. Nilikuwa mkali sana, nikaomba aje manager wao mdosi nikamwelewesha na tukaenda cross cheki naye...akasema samahani sana nikalipishwa bei halali nilisevu kitu kama 40,000 hivi...sasa wale wasiocross check huwa wanalipa tu na kuibiwa....Bongo inakeraaa si kidogo.

Shoprite ukinunua items nyingi .. scrutinize the receipt .. nimeshawahi kubambikiwa vitu kwenye receipt .. ila i realized after 2 days
 
Unajua tatizo letu nyumbani Tanzania ni umasikini wa fikra especially amongst ourselves. Tunadharauliana sisi kwa sisi..Utakuta mtu ameajiriwa dukani kwa mhindi au position mbovu mbovu ya u teller kwenye bank ya kigeni, basi ukienda kutafuta huduma, these people I call them "gate keepers" watakuangalia kwanza umevaa nini, au una usafiri gani, na vitu vingine kabla ya kudecide wakupe huduma au wakuletee nyodo. Uzuri wa hapa States ni kwamba competition ni kubwa na ukimfanyia mtu "wrong" ubaya utavuma kuliko pale utakapompa huduma nzuri.
Kama wafanyabiashara bongo wangekuwa na concept kwamba sio kila shopper ni lazima awe buyer...na wakawa train hao associates wao kuwa na lugha nzuri ili kuwa turn hao shoppers into buyers....biashara nyingi zingefika mbali sana lakini kwa mwendo huu...mmh inasikitisha.

Point. Niliwahi kufika pale na mtoto wangu ameshika chupa ya maji ambayo alikuwa ameishakunywa nusu. Nikaambiwa haturuhusiwi kuingia nayo ati tunaweza kubadilisha na kuchukua nyingine iliyojaa!!!! #%@^&%#!!! wakati tunabishana wakapita wazungu wakiwa na 'magunia' yao mgongoni, nikawauliza wale askari mbona hawa hawazuiwi wakajibu ati wameweka pesa zao kwenye rucksack zao ndio maana!!! Nikaondoka na kwenda zangu kwa mpemba wa mtaani. na nina kitambi!
 
Any Suggestion ili tu-improve? maana mimi m'bongo wa bongo na ntafia bongo; Yalinishindaga ya uzunguni

Hivi yale ya kule north MD mweusi anakua kinyesi na kukimbiana kwa watu wa US na UK hayaboi?
 
Wakuu achaneni na hiyo ya ukaguzi wa tiketi na visa uwanja wa ndege ambayo huwa inanibughuzi kinoma, mimi nina experience na walinzi wa bank ya Barclays Arusha...mwaka jana nilikuwa A-town kwa ka likizo kafupi. Nikawa nataka ku withdraw ka pesa kadogo kutoka kwenye account yangu.nikaona ngoja nitumie ATM za Barclays Bank kwa sababu kuna mtu aliniambia wana charge fees ndogo. Bahati mbaya sana au nzuri sana...wakati ninaenda Bank nilikuwa nimeandama na mzungu volunteer wa PeaceCorp. Kwa nini walinzi wasinizuie kwenye gate..wamruhusu mzungu kwenda...hata baada ya kuwaambia kuwa mimi ndio ninayetaka kutumia huduma ya ATM...wakasema ATM zao zina charge fees kubwa kwa Tembo kadi kwa hiyo I am better off kwenda CRDB Clock Tower. Yaani walishakuwa na assumption kwamba I am a Tembo Card holder kwa sababu ni mbongo. Nikashindwa kuvumilia nikawaambia waniitie manager kama hawataki niende kutumia ATM, baada ya kuona hivyo wakaniachia niende, huku nyuma yule mzungu akaanza kupiga nao kiswahili akawaambia kuwa mimi ninaishi Marekani. Baada ya kumaliza haja yangu wakati narudi gateni...jamaa wakawa wananichangamkia kinoma...nikaona hawa washenzi tu. I was so pissed kidogo niandike barua kwenye mgmt ya hiyo bank.
Dawa yao ni kuanza kuwarishia ngumi.
 
Back
Top Bottom