Bongo Flava ni ya waliofulia?

Lutala

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
848
103
TMK waanza kebehi kwa waliofulia

na Ruhazi Ruhazi

KUNDI la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Family la Temeke Dar es Salaam, limeachia wimbo wake mpya uitwao ‘Wapinzani', unaoonekana kama kebehi kwa makundi yaliyofifia.

Akizungumza na gazeti hili jana, Meneja wa kundi hilo Said Fella, alisema kuwa, sababu ya kuutoa wimbo huo ni kutaka kuwahamasisha wasanii wa makundi mengine kuwa wavumilivu kama wao.

Fella alisema, katika wimbo huo ulioimbwa na wasanii wote wa kundi hilo, pia wameamua kumshirikisha msanii Shaban Katwila ‘Q. Chilla, kwa nia ya kuonyesha mshikamano wao na wasanii binafsi au makundi mengine.


"Mkubwa tumeachia wimbo mpya unaitwa ‘Wapinzani' tumeshausambaza kwenye vituo vya radio, hatujamtukana mtu, ila tunachokifanya ni kuwapa wenzetu ushauri wa kufanya kazi kwa bidii na bila kuchoka kwa faida ya muziki wetu," alisema Fella.


Alisema, wimbo huo utakuwa katika albamu ijayo ya kundi hilo, ambayo wameanza kuiandaa wakitarajia kuitoa baadaye mwaka huu.


TMK kundi ambalo lilikuwa likichuana vikali na East Coast Team, lililokuwa likiundwa na watoto wa Upanga, lilikosa mpinzani baada ya wapinzani wao kutoweka.


Pia kujitoa kwa wasanii kadhaa wakiongozwa na Juma Kassim ‘Sir Nature' kulionekana kungeleta mtikisiko kwa TMK Family, lakini kundi jipya la TMK Wanaume Halisi nalo limeonekana kushindwa kuleta upinzani wa haja.
 
Njaa hii!

Wanau'release sasa hivi wakati wa kampeni ili wachukuliwe na ccm na wauimbe majukwaani na ionekane wanawaongelea wapinzani wa kisiasa!

"Kula tule sisi...Washibe wao"...
 
Njaa hii!

Wanau'release sasa hivi wakati wa kampeni ili wachukuliwe na ccm na wauimbe majukwaani na ionekane wanawaongelea wapinzani wa kisiasa!

"Kula tule sisi...Washibe wao"...

PJ ndiyo yale yale ukipewa lift unataka upige na honi
 
Nilipanda daladala siti ya mbele hv karibuni nikakutana na maandishi.."abiria haruhusiwi kuchezea redio":lol::lol::lol:
:laugh::laugh::laugh: Hiyo kali si unajua daladala usafiri wa umma kila mtu akiingia humo anafanya anachotaka ikiwemo kuchora siti, kula miwa na kutupa maganda ndani yake kutupa chupa za maji ndani yake na maganda ya karanga kama vile jalala
 
Jamani bongo flava sio aina ya muziki, ila ni makelele ya vijana wavuta bange
Mkuu kazi ya watu hiyo, kauli yako si yakiungwana, kuna watu wanaishi kwa kazi hiyo tena wanamafaniko sana tu. na inatoa ajira kubwa sana kuliko unavyofikiria
 
hii yote sababu dada nakaaya kakimbia toka chadema!!:becky:
 
Bongo njaa kali, eti mwanamziki yupo kwenye game miaka zaidi ya mitatu, bado ananyanyaswa na baba mwenye nyumba tena temeke, unategemea nini ccm wakimtongoza kumpa milion moja?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom