Bongo Celebrities "washangaa"!!!

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
...kuna wakati 'celebrities' nao hushangaa watu wanapowashangaa?

Habari za kawaida
Posted Date::6/7/2008
Mashabiki Cape Verde wagombea bendera ya Tanzania
Na Saleh Ally, Praia, Cape Verde

MASHABIKI mbalimbali wa soka katika mji huu walionyesha kuwashangaza mashabiki wachache wa Tanzania waliotua mjini hapa, wakiongozana na timu ya soka ya taifa (Taifa Stars) baada ya kugombea bendera za Tanzania.

Mashabiki hao waliojitokeza kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, Praia walifanya kitu cha ajabu na kuwashangaza mashabiki hao wa Tanzania baada ya kuanza kugombea bendera ya Tanzania.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mashabiki hao waliomba wapewe bendera za Tanzania na baada ya wachache kukabidhiwa wengine walijitokeza na kuanza kugombea bendera hiyo.

Hali hiyo pia ilionyesha kumshangaza Kocha Mkuu wa Stars, Marcio Maximo ambaye alisema hiyo inaweza kuwa nyota njema kwa ajili ya mechi ya jana.

Walipoulizwa mashabiki hao walimjibu mwandishi kuwa wao ni wakarimu kwa kila mtu hivyo si ajabu kwao kubeba bendera ya nchi nyingine na walikuwa tayari kuishangilia Tanzania ili mradi wacheze vizuri.

Juzi maeneo mbalimbali ya mji wa Praia yalikuwa yamechangamka lakini walishangazwa zaidi na Tanzania kutua nchini hapa na ndege yao na ikaendelea kuwasubiri.

Mashabiki hao walitafsiri Tanzania ni nchi tajiri sana na kuwa wamekuwa tofauti na karibu kila nchi iliyokuja kucheza hapa.

Stars iliwasili mjini hapa ikiwa katika ndege ya Air Tanzania ambayo iliwasubiri uwanjani hadi siku ya kuondoka. Ndege hiyo aina ya Boeing 737 ni kubwa kuliko zote zinazomilikiwa na nchi hii.

wangejua kuwa ni ...'vijisenti' tu! he he he...

Facts;
Cape Verde is a small nation that lacks resources and has experienced severe droughts. Agriculture is made difficult by lack of rain and is restricted to only four islands for most of the year. Most of the nation's GDP comes from the service industry. Cape Verde's economy has grown since the late 1990s, and it is now considered a country of average development. Cape Verde has significant cooperation with Portugal at every level of the economy, which has led it to link its currency first to the Portuguese escudo and, in 1999, to the euro.
 
...kumbe Cape verde kunafaa huko kufanyia matanuzi ukiwa na 'vijisenti!'...
 
Kwa sana tu....sasa ingekuwa bomba kama tungeondoka na angalau kaushindi kembamba...wapi...
Yeah ni pazuri kwa matanuzi na vijisenti vyetu kumbe. Kwikwikwi
 
sasa chenge akienda na vijisenti vyake akiwaambia yeye ni bill gates kawa mweusi kwa jua la africa si watakubali na kumwabudu???!!!
mbwembwee zoooote na bao tukaliwa
 
Back
Top Bottom