PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,203
- 8,724
Wadau,
Naomba kusaidiwa maelezo ya kitaalamu au ya kiuzoefu kuhusu mambo ya ammunitions, hususan bomu.
Kufuatia ajali ya mabomu Mbagala na GongolaMboto, nimesikia kauli kama:
Bomu lilitua mlangoni kwangu, lakini halikulipuka!
Kinachinisumbua ni kwamba inakuwaje bomu lisafiri toka kwenye ghala hadi umbali wa km4,au 5 bila kuwa limerushwa na chombo maalumu, na bila kuwa limelipuka??
Nijuavyo mimi ni kuwa katika hali ya kawaida ya ulipuaji, bomu linawekwa kwenye mtutu au mzinga, ambao ndio hulirusha, na likifika huko lilikotumwa linalipuka.
Lakini kwa situation ya Gongolamboto, ni nguvu gani inayolirusha bomu(propulsion) tokea kwenye stoo, likiwa halijalipuka, na likasafiri km5, na likaanguka huko, na bado ikaripotiwa kwamba halijalipuka?