Bomu latibua futari Mbagala!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
Wakati wahanga wa mabomu ya Mbagala wakiwa bado hawajasau vizuri yaliyowakumba siku za nyuma....mlipuko mwingine wa bomu ulitokea juzi na kusababisha tafrani ya aina yake kwa wakazi hao ambao baadhi yao walikuwa wakijipatia futari.

Mlipuko huo ulitokea saa moja usiku mtaa wa Mbagala Kuu baada ya msimamizi wa nyumba namba MA/1/2835, aliyefahamika kwa jina la Emmanuel kumaliza kukusanya taka na kuzichoma kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi.

Emmanuel ambaye hakumtaja mmiliki wa nyumba hiyo, alisema alikuwa anafanya usafi saa 11 jioni na baada ya kufanya usafi huo aliondoka kwa muda lakini ilipofika saa moja usiku wakati taka hizo zikiungua, ghafla kulisikika mlio mkubwa eneo alilokuwa amekusanya taka hizo. Alisema baada ya mlio huo majirani wa eneo hilo ambao walikuwa wanamalizia kufuturu walilazimika kukimbia ili kunusuru maisha yao.

Kwa mujibu wa Emmanuel, mlipuko huo uliwakumbusha yale yaliyotokea Aprili 26 mwaka huu na kusababisha watu 26 kupoteza maisha. “Tunaiomba Serikali itume wataalamu wa mabomu ili kuchunguza zaidi kwani tumelipwa fidia na wengine tumeanza ujenzi, tuna wasiwasi hali inaweza kubadilika.

“Inaonekana kuna baadhi ya mabomu yamejifukia chini sasa tunapoanza ujenzi yanaweza kulipuka, tutaishi kwa hofu hadi lini? Mtu kachoma moto tu hapa kishindo kilichotokea kila mmoja alikimbia sehemu yake, tunaomba waje kuangalia kama mabomu yapo au hayapo ndipo tuanze kujenga,” alimalizia.

Source: http://www.darhotwire.com/home/news/2009/09/01/bomu_latibua_futari_mbagala.html
 
Poleni ndugu zangu mungu yupo atawaokoa. Serikali wasaidieni hao kusafisha kabisa maeneo au kuwahamisha
 
Back
Top Bottom