Bomu la machozi bungeni. Fundisho Tanzania?

whizkid

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
357
240
skorea_teargas.jpg


Katika hali iliyowashtua wengi, mbunge wa upinzani katika bunge la Korea ya Kusini, arusha bomu la machozi katika harakati za kupinga kupitshwa kwa makubaliano ya biashara ya soko huria (FTA) na USA ambayo hatimaye yalipitishwa jioni ya leo nchini mwao. Mabadiliko hayo yatakayofungua milango ya soko huria kati ya nchi yao na USA, EU, India na mataifa mengine yanayotumia sheria ya kimataifa ya masoko, yamepitishwa leo baada ya kupitia upinzani mkali tangu 2007 nchini humo. Bunge liliitishwa ghafla ili wabunge kujadili na kupiga kura, ambapo chama tawala (Grand National Party) kina wabunge wengi hivyo kushinda kwa kura 151 - 7. Waziri mkuu mstaafu Han Myeong-Sook anayetokea chama kikuu cha upinzani nchini humo (Democratic Party) anasema kupitishwa kwa makubaliano hayo si halali kwa sababu ni kinyume na matakwa ya wananchi.

Fundisho Tanzania?
Ama kweli kuwa mpinzani sehemu yoyote duniani ni shughuli nzito. Jamaa hadi karusha bomu la machozi bungeni lakini wapi, kitu kimepita. Kambi rasmi ya upinzani bongo wamesusia bunge lakini wapi. Muswada umepita!

Kimantiki, bunge lililohitimishwa Jumamosi iliyopita halina tofauti sana na hali hii ya Korea Kusini. Kote mijadala ni mambo yenye maslahi kwa taifa husika. Tofauti tu huku hayakuwa mabomu ya machozi katika harakati. Bali ni bomu zito la hotuba ya kambi rasmi ya upinzani alilolitoa Tundu Lissu kupitia hotuba yake kisha kususia vikao vya bunge, yeye na wenzie. Baada ya wabunge waliobaki Bungeni asilimia kubwa kutumia muda wao kuongea mipasho badala ya hoja, hatimaye muswada ulipitishwa. Kwa mbwembwe zote, shangwe na vigelegele.

Wapinzani na wapenda mabadiliko wanatambua kuwa hatua zote zitapitiwa lakini mwisho wa siku, CCM wana agenda yao ambayo lazima wataisimamia. Mkuu wa kaya ameshasema isiwe nongwa tunamuandama yeye mbona wengine waliomtangulia wamepitisha katiba? Ameonyesha mtazamo na msimamo wake. Kilichobaki ni nini? Tuingie mtaani kama Tahrir square? Au tuendelee kungoja kwanza? Wahenga na methali zao wachokozi sana. Eti ngoja ngoja yaumiza matumbo. Simba mwenda pole ndie mla nyama. Wananchi tumekuwa simba waenda pole kwa muda mrefu na matumbo yanauma, wakati nyama tunajua ipo wapi! TUKALE NYAMA!

**UPDATE:**
Mwaka 2008, wapinzani walienda na nyundo kuvunja mlango wa chumba ambapo kikao cha kamati ya bunge kilikuwa kinajadili muswada huu uliopitishwa leo. Hawa wapinzani wa South Korea ni noma!
 
Da nimeona sema nilikua sijaelewa vizuri(no audio) nimeona wanajipepea na wanaziba sura zao na vitambaa
 
Njiia moja wapo nzuri ya kuonesha umechukizwa na jambo ambalo halina masilahi kwa wananchi na hukubali kuburuzwa na wengi.
 
ila jamaa wa chama tawala wanakomaa kama magamba wamelia na makamasi kwa wingi lakini wamepitisha bora wangetumia formular ya bunge la somalia ukijifanya hauelewi bakora zinatembea zikivunjika viti pia vinafaa kutoa adabu
 
Hizo ndo harakati sasa za ukweili tarehe ishatangazwa kilichobaki ni hamasa kwa umma kutambua haki zao na kuzidai wala sio kuziomba kama tunavyofanya kila mara.
 
Kumbe nchi za wenzetu wanaruhusu raia kumiliki mabomu! safi sana natamani wabunge wetu wa upinzani nao waingie na mabomu mjengoni na kulipua wakati wa kupinga hoja za kipumbavu!
 
Hao wa sera ya "upiganaji" kama magwanda, nilipoisikia hii habari kwenye TV ilibidi nicheke.

Uzuri ni kuwa hilo lilkuwa bomu la machozi, nangojea siku "wapiganaji" wa magwanda wetu watapoacha kususa na wao wakawaonjeshe vibomu vya machozi magamba pale mjengoni, nna uhakika magwanda wengi wao wauzoefu navyo. Duhhh, najaribu kum imagine Mama Makinda atakuwaje. "aliomba muongozo, mara naona moshi, baada ya hapo sikuelewa kilichoendelea napata fahamu najikuta nipo Apollo, India."

Hapa itabidi mtowe maoni hawa wabunge wetu reaction zao na mswaada utakaofatia...
 
Magufuli: lile lijitu lilisimama meter 24.56 kutoka meza ya Supika, likanyanyua mkono futi 6 na inchi 11 juu ya usawa wa bahari, likarusha lile kombora likadondoka futi 2.8 kutoka meza ya supika na ilikuwa futi 12.3 kutoka meza ya kiongozi wa upinzani lakini kiongozi wa upinzani alikuwa inchi sita kutoka lango kuu alikuwa akiongoza kususa...

...moshi uliotoka pale ulikuwa unapanda juu kwa mita 3 kwa sekunde moja na ulikuwa unaelekea mashariki ya ukumbi kwa supidi ya mita 2.4 kwa sekunde...
 
Back
Top Bottom