Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,466
- 113,543
Mkuu Mchambuzi, kadri siku zinavyokwenda ndivyo unavyozidi kutitirika na mada za ukweli, naomba nikupongeze tena na tena kwa kuwa u miongoni mwa ma great thinkers wetu humu jf ambao mnasimama kwenye kweli!. Kuhusu EL nimekusoma vizuri kabisa in between the lines kuhusu Uwezo, Upeo, Uelewa na Political will kufanya maamuzi magumu!. Thanks.Tumeshaelewa hoja ya Lowassa, nadhani sasa ni wakati wa kuelekeza juhudi zetu katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu; Ni muhimu tukampongeza Lowassa kwa kuwa kiongozi wa kwanza nchini kulipa suala hili uzito unaostahili, Kitu muhimu alichofanya Lowassa ni kuamsha watu, kutokana na upeo wake mkubwa na uelewa juu ya masuala yanayozunguka jamii za dunia ya tatu, kupitia usomaji wa tafiti na ripoti mbalimbali, tofauti na viongozi wengi wa CCM ambao ni mchanganyiko wa wavivu wa kusoma na wasiojua kusoma kwa kuelewa;
Suala lingine muhimu, pengine zaidi ni kwamba, kitendo cha Lowassa kulizungumzia suala hili ni ishara kubwa kwamba pengine sasa suala hili litapata POLITICAL WILL, kwani lack of political will ni moja ya vikwazo vikubwa vinavyotukabili kama taifa katika jitihada za kutokomeza umaskini, na vile vile kuchukua maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa;
Hizi ni baadhi ya changamoto muhimu ambazo serikali ya CCM au Chadema, zote zitakumbana nazo Ikulu, na ni suala ambalo lipo katika nchi zote za dunia ya tatu; ni muhimu katika mjadala wetu juu ya ufumbuzi wa tatizo la ajira kwa vijana tukawa na ufahamu juu ya changamoto hizi, hasa kuhusu Nini serikali inaweza kufanya, na Nini Serikali haiwezi kufanya, bila ya kujalisha ni chama gani cha siasa au mtu gani anaingia Ikulu 2015;
P.