Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Tumeshaelewa hoja ya Lowassa, nadhani sasa ni wakati wa kuelekeza juhudi zetu katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu; Ni muhimu tukampongeza Lowassa kwa kuwa kiongozi wa kwanza nchini kulipa suala hili uzito unaostahili, lakini tutambue pia kwamba Lowassa sio mtu wa kwanza kuzungumzia tatizo hili kwani kwa wale wanaosoma tafiti mbalimbali, kwa miaka mingi sasa taasisi za utafiti kama vile REPOA, ESRF, na nyingine nyingi nje ya nchi (e.g. Benki ya Dunia n.k), zimekuwa zikilijadili suala hili na kutoa tahadhari kwa muda mrefu; Kitu muhimu alichofanya Lowassa ni kuamsha watu, kutokana na upeo wake mkubwa na uelewa juu ya masuala yanayozunguka jamii za dunia ya tatu, kupitia usomaji wa tafiti na ripoti mbalimbali, tofauti na viongozi wengi wa CCM ambao ni mchanganyiko wa wavivu wa kusoma na wasiojua kusoma kwa kuelewa;
Suala lingine muhimu, pengine zaidi ni kwamba, kitendo cha Lowassa kulizungumzia suala hili ni ishara kubwa kwamba pengine sasa suala hili litapata "POLITICAL WILL", kwani ‘lack of political will' ni moja ya vikwazo vikubwa vinavyotukabili kama taifa katika jitihada za kutokomeza umaskini, na vile vile kuchukua maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa;
Ni vigumu kulielewa tatizo la ajira kwa vijana bila ya kuwa na takwimu za kulitazama na kulielewa kwa undani, kwani tatizo hili ni la kimfumo kuliko kitu kingine chochote; Ukosefu wa uchambuzi usiozingatia takwimu na pia kulielewa tatizo hili kimfumo ni moja ya mapengo makubwa yanayotawala mijadala juu ya suala hili; Nia yangu ni kujaribu kuziba pengo hilo, ili kwa pamoja tusaidiane kuondokana na siasa katika mjadala huu na kuhamia katika mikakati ya kutegua bomu hili kabla halijalipuka; Nitakachofanya hapa haitakuwa uchambuzi bali kwanza kuweka takwimu muhimu ili kwa pamoja tufanye uchambuzi, na pengine kupata ufumbuzi angalau kimjadala; Nitaanza na mfumo wa elimu ya msingi, sekondari, Vyuo Vikuu, na kumalizia na mawazo yangu kuhusu masuala muhimu ya kutazama kabla ya kuanza kunyoshea vidole serikali au chama chochote cha siasa;
ELIMU YA MSINGI
Kufikia mwaka 2012, mfumo wetu wa elimu ya msingi unakadiriwa kuwa na jumla ya watoto karibia milioni kumi; hili ni ongezeko la karibia watoto milioni mbili na nusu ndani ya kipindi cha miaka mitano tu, kwani mwaka 2007mfumo huu ulikuwa na jumla ya watoto milioni saba na nusu); Inakadiriwa kwamba watoto wanaofanikiwa kumaliza elimu ya msingi ni 80% ya watoto wote, huku 20% wakishindwa kufika darasa la saba kutokana na sababu mbalimbali; Kwa maana hii, kila baada ya miaka kadhaa, watoto wasiopungua milioni moja huingia mitaani wakiwa 'primary school dropouts'; Hii ni nje ya idadi ya watoto ambao hawafanikiwi kujiandikisha darasa la kwanza, hivyo kufanya idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka kumi na tano wanaoishia mitaani bila elimu ya msingi kuwa kubwa zaidi, kila baada ya miaka kadhaa;
Tumeona kwamba ni 80% ya watoto ndio hufanikiwa kumaliza darasa la saba; Sasa kati ya hawa 80%, wanaofanikiwa kuendelea na elimu ya sekondari ni 20% ya hao 80%; kwa maana hii, nje ya wale watoto zaidi ya milioni moja tuliobaini kwamba hawafiki darasa la saba, kuna mamilioni wengine ambao hawafanikiwa kuendelea na elimu sekondari kila baada ya miaka kadhaa; Kwahiyo ukichanganya makundi haya mawili (primary school dropouts na standard seven failures), unakuta mamilioni ya watoto wenye umri chini ya miaka 15 wanaishia mitaani kila baada ya miaka kadhaa;
ELIMU YA SEKONDARI
Ukiachilia mbali kundi la watoto wanaoishia ngazi ya elimu ya msingi, kuna tatizo pia kwenye ngazi ya sekondari; Kwa mujibu wa Benki ya Dunia (2010), katika kipindi cha mwaka 2000 – 2010, jumla ya wanafunzi milioni moja la laki tatu walimaliza elimu yao ya Sekondari Tanzania; Matokeo yao mitihani kidato cha nne yalikuwa kama yafuatayo:
Iwapo tunachukulia kwamba wanafunzi waliopata madaraja ya Kwanza hadi Tatu ndio uendelea na elimu ya juu, basi ina maana kwamba kati ya wanafuzi milioni moja na laki tatu waliomaliza elimu zao za sekondari katika kipindi hicho (2000 – 2010), waliofanikiwa kuendelea na elimu ya juu ni 25% tu [sawa na wanafunzi 325,000 kati ya jumla ya wanafunzi 1,300,000]; Hivyo, katika kipindi hiki, wanafunzi wa sekondari walioishia mitaani ni karibia 975,000; Hata kwa wale waliofanikiwa kuendelea na elimu ya juu, kama tunavyoelewa, bado suala la ajira huko mbeleni sio la uhakika;
Benki ya Dunia inakisia kwamba takribani vijana 850,000 wenye umri kati ya miaka 15 na 25 huingia kwenye soko la ajira kila mwaka Tanzania, huku 40% ya hawa ikiwa ni form four failures; Benki ya Dunia inazidi kukadiria kwamba ifikapo mwaka 2015, kutakuwa na nyongeza ya vijana milioni moja na laki tatu katika soko la ajira;
Kwa mujibu wa takwimu nyingine kutoka African Economic Outlook (2010), 60% ya watanzania hawajavuka miaka 25, na inakadiriwa kwamba ifikapo mwaka 2015, 75% ya watanzania watakuwa chini ya umri wa miaka 25;
ELIMU VYUO VIKUU
Kuanzia kipindi cha uhuru hadi mwisho wa miaka ya themanini, inasemekana kwamba 90% ya wahitimu wa vyuo vikuu Tanzania kila mwaka walikuwa wanapata ajira (wage employment); Lakini ilipofikia mwaka 1999, idadi hii ilishuka hadi 70%; Leo hii, inasemekana kwamba wahitimu wa vyuo vikuu wanaopata ajira kila mwaka (wage employment) haivuki 50%;
BAADHI YA CHANGAMOTO
SEKTA KUU ZA AJIRA NCHINI
BAADHI YA MASUALA MUHIMU YA KUZINGATIA
Kwanza, chini ya mfumo wa soko huria unaofuata kanuni za kiliberali na ubepari, uchumi unaendeshwa kwa kufuata nguzo kuu tatu ambazo ni PRIVATIZATION, LIBERALIZATION & MARKETIZATION;
Pili, moja ya maeneo muhimu kisera katika mfumo huu ambayo yanasimamiwa kwa ukaribu na World Bank, IMF na WTO, ni pamoja na kupunguza inflation, kuondoa barriers on trade (ili bidhaa za nje ziingie kwa urahisi na kupata soko) & remove barriers on FDI (ili iwe rahisi kwa mitaji ya nje kuja kuwekeza kwenye sekta ambazo ni resource-based), kupunguza matumizi ya serikali (hasa matumizi katika uwezekezaji kwenye sekta ya UMMA na badala yake kuachia nguvu za soko zifanye hilo),n.k, yote haya kwa imani kwamba yatasaidia kukuza uchumi na kupunguza umaskini;
Tatu, chini ya mfumo huu, serikali haina nafasi ya kuwa mzalishaji, mtengenezaji wa ajira, n.k, na badala yake hayo hutegemea zaidi nguvu ya soko; Kazi kubwa ya serikali inabakia kuwa Facilitation; Hii ni tofauti na enzi za UJAMAA ambapo serikali ilikuwa na nafasi ya kuzalisha huduma na bidhaa kwa wingi, kutengeneza ajira n.k, hasa kupitia umiliki wake wa njia kuu za uchumi;
Na nne, tofauti na jinsi nchi tajiri zinavyoendesha sera za uchumu katika nchi zao, kwa mfano kwa kulipa suala la unemployment uzito mkubwa sambamba na economic growth na inflation, mataifa haya hayataki kushughulika na suala la unemployment kwenye nchi zetu, badala yake hujikita zaidi kwenye economic growth (ili mitaji yao ipate soko zaidi) na inflation (ili investor bonds zisiathirike); Kuondoa barriers to trade and foreign investment inasaidia wakubwa hawa kuua uwezo wetu to industrialize, na kuwa na a skilled pool of employees/labour force kwani tukifanikiwa katika haya mawili na kujitosheleza kwa bidhaa, tutaweza kuleta ushindani dhidi ya bidhaa zao ambazo zinaingia kwa urahisi kupitia trade liberalization; Vinginevyo suala la unemployment huwa treated on the sidelines na kwa umakini ili lisivuruge mpango huu;
Hizi ni baadhi ya changamoto muhimu ambazo serikali ya CCM au Chadema, zote zitakumbana nazo Ikulu, na ni suala ambalo lipo katika nchi zote za "dunia ya tatu"; ni muhimu katika mjadala wetu juu ya ufumbuzi wa tatizo la ajira kwa vijana tukawa na ufahamu juu ya changamoto hizi, hasa kuhusu Nini serikali inaweza kufanya, na Nini Serikali haiwezi kufanya, bila ya kujalisha ni chama gani cha siasa au mtu gani anaingia Ikulu 2015;

- Division One 3% (wanafunzi takribani 39,000)
- Division Two, 5% (takribani wanafunzi 65,000)
- Division Three, 15% (takribani wanafunzi 195,000)
- Division Four, 50% (takribani wanafunzi 650,000)
- Division Zero, 26% (takribani wanafunzi 338,000)
Iwapo tunachukulia kwamba wanafunzi waliopata madaraja ya Kwanza hadi Tatu ndio uendelea na elimu ya juu, basi ina maana kwamba kati ya wanafuzi milioni moja na laki tatu waliomaliza elimu zao za sekondari katika kipindi hicho (2000 – 2010), waliofanikiwa kuendelea na elimu ya juu ni 25% tu [sawa na wanafunzi 325,000 kati ya jumla ya wanafunzi 1,300,000]; Hivyo, katika kipindi hiki, wanafunzi wa sekondari walioishia mitaani ni karibia 975,000; Hata kwa wale waliofanikiwa kuendelea na elimu ya juu, kama tunavyoelewa, bado suala la ajira huko mbeleni sio la uhakika;
Benki ya Dunia inakisia kwamba takribani vijana 850,000 wenye umri kati ya miaka 15 na 25 huingia kwenye soko la ajira kila mwaka Tanzania, huku 40% ya hawa ikiwa ni form four failures; Benki ya Dunia inazidi kukadiria kwamba ifikapo mwaka 2015, kutakuwa na nyongeza ya vijana milioni moja na laki tatu katika soko la ajira;
Kwa mujibu wa takwimu nyingine kutoka African Economic Outlook (2010), 60% ya watanzania hawajavuka miaka 25, na inakadiriwa kwamba ifikapo mwaka 2015, 75% ya watanzania watakuwa chini ya umri wa miaka 25;
ELIMU VYUO VIKUU
Kuanzia kipindi cha uhuru hadi mwisho wa miaka ya themanini, inasemekana kwamba 90% ya wahitimu wa vyuo vikuu Tanzania kila mwaka walikuwa wanapata ajira (wage employment); Lakini ilipofikia mwaka 1999, idadi hii ilishuka hadi 70%; Leo hii, inasemekana kwamba wahitimu wa vyuo vikuu wanaopata ajira kila mwaka (wage employment) haivuki 50%;
BAADHI YA CHANGAMOTO
- Idadi ya wahitimu wa vyuo vikuu inazidi kukua kwa kasi kuliko uwezo wa uchumi kuzalisha ajira;
- Vile vile vijana wengi wanaohitimu darasa la saba, sekondari na pia baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu hawana ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira;
- Vijana wengi wanaohitimu ngazi mbalimbali za elimu pia hawana ujuzi unaohitajika kujiajiri wenyewe, ukiachilia mbali tatizo la mitaji ya kuanzisha biashara;
- Chini ya mfumo wa soko huria, Serikali bado haijafanikiwa kuja na sera zenye kuleta matumaini kwa vijana walio wengi;
- Nchi wahisani hasa kupitia WorldBank, IMF na WTO hawana nia ya dhati ya kulitatua tatizo hili kwani hali iliyopo inayapa mataifa makubwa faida kubwa kiuchumi;
SEKTA KUU ZA AJIRA NCHINI
- Kilimo ni takriban 80%;
- Sekta isiyo Rasmi (Informal Sector) takriban 9%;
- Sekta Binafsi/iliyo Rasmi (Viwanda na Huduma) takriban 5%;
- Serikali/Sekta Ya Umma karibia 2.5%;
- Kazi Za Nyumbani (mashamba boy, n.k) karibia 3.5%;