BornTown
JF-Expert Member
- May 7, 2008
- 1,716
- 481
Ni wazi kuwa ubomoaji wa majumba ya kifahari kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi,Dar es Salaam inavuta hisia za wengi.Wengine tunafuatilia tukishangaa namna wahuni wachache wa nchi hii walivyojilimbikizia mali na kujenga majumba ya thamani kubwa. Serikali inafanya kusudi kuvuta 'attention' ya watu ili wasahau mambo muhimu kama ya migomo na maisha bora.Serikali inajipalilia moto zaidi.Inaongeza chuki kwa wananchi.Kwanini isifanye sirini?
Tunafaidikaje kuangalia matingatinga yao? Ukweli ni kwamba,kila anayevunjiwa nyumba yake ameshalipwa. Serikali pale inafanya maigizo.Fahamuni kuwa Serikali iko kwenye harakati za kuwaaminisha watanzania kuwa yenyewe na viongozi wake si dhaifu.
Lakini siwalishaambiwa wabomoe tangu mwanzoni wa mwezi wa 4 na wengine waliambiwa waache kujenga wakakaidi sababu ya pesa zao sasa wajue sheria ni msumeno unakata kote kote, na hata ule mkutano wa mei 15 wa nemc na waandishi wa habari na mama tibaijuka waliwaabarisha kuwa wanatakiwa wabomoe nyumba zao wakakaidi