Bomoa-Bomoa ya UFUKWENI si bure

Ubomoaji wa myumba za ufukweni ni danganya toto maana tayari watu wameshalipwa stahili zao, kinachofanyika ni danganya toto kama ni kweli mbona wamiliki hawaja onekana kwenye nyumba zao? wameonekana wapangaji na vibaka waliokuwa wanajichukulia mabati.

Hizo nyumba nyingi zilikuwa hazijaisha kama ni zile za kule kunduchi chini ninazozifahamu mimi.
 
zamu ya matajiri imewadia tumelalamika sana kuwa ni masikini tu wanaguswa sasa maghorofa yameangushwa na tingatinga

hao matajiri wameshalipwa fidia ya bilions, ndo maana wako kimyaa, hawalalamiki. Tibaijuka akitaka kufanya kweli avunje majumba yaliyojengwa kwenye open space huku sinza na eneo lote la kinondoni. viwanja vinavyopimwa visitolewe kwa kupendelea yaani kwa wakubwa kama tunavyo witness viwanja vya gezaulole, mabwepande nk. majina ya wanaopewa viwanja na ya vigogo; wabunge, maRCs, mawaziri na watoto wao...
 
Ni wazi kuwa ubomoaji wa majumba ya kifahari kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi,Dar es Salaam inavuta hisia za wengi.Wengine tunafuatilia tukishangaa namna wahuni wachache wa nchi hii walivyojilimbikizia mali na kujenga majumba ya thamani kubwa. Serikali inafanya kusudi kuvuta 'attention' ya watu ili wasahau mambo muhimu kama ya migomo na maisha bora.Serikali inajipalilia moto zaidi.Inaongeza chuki kwa wananchi.Kwanini isifanye sirini?

Tunafaidikaje kuangalia matingatinga yao? Ukweli ni kwamba,kila anayevunjiwa nyumba yake ameshalipwa. Serikali pale inafanya maigizo.Fahamuni kuwa Serikali iko kwenye harakati za kuwaaminisha watanzania kuwa yenyewe na viongozi wake si dhaifu.

Hivi nchi hii mtaacha lini kulalamika? Nyumba zimejengwa kwa kukiuka sheria na serikali imechukua hatua then mnalialia. Migomo ya hawa wakamua majipu tumeshuona ni wa kijinga na wananchi wameshawaona wajinga. Wacha washushe hizo nyumba za watu wanaodhani fedha inaweza kufanya chochote, ikiwemo kusigina sheria.
 
Waliobomoa ni NEMC...NA wala haina uhusiano wowote na hali ya kisiasa nchini, mkumbuke NEMC imekua inasumbuana na hawa watu wenye mijengo kwa mda sasa na jana ndio walibomoa..taarifa za uhakika ni kwamba NEMC wanapanga kubomoa nyumba nyingi zilizojengwa kiholela bila kujali gharama ama umaarufa wa mmiliki...
 
Ubomoaji wa myumba za ufukweni ni danganya toto maana tayari watu wameshalipwa stahili zao, kinachofanyika ni danganya toto kama ni kweli mbona wamiliki hawaja onekana kwenye nyumba zao? wameonekana wapangaji na vibaka waliokuwa wanajichukulia mabati.

Hakuna mtu aliyelipwa mkuu mimi nimefatilia hili zoezi na nina ndg yangu ni Mkurugenzi pale Nemc...
 
hao matajiri wameshalipwa fidia ya bilions, ndo maana wako kimyaa, hawalalamiki. Tibaijuka akitaka kufanya kweli avunje majumba yaliyojengwa kwenye open space huku sinza na eneo lote la kinondoni. viwanja vinavyopimwa visitolewe kwa kupendelea yaani kwa wakubwa kama tunavyo witness viwanja vya gezaulole, mabwepande nk. majina ya wanaopewa viwanja na ya vigogo; wabunge, maRCs, mawaziri na watoto wao...
Tena hii open space ya ya mbele ya double view mbona kashindwa kuibomoa najamaa sasa wanaendelea na ujenzi!!
 
Mkuu the Choosen; hata kama unalipwa kufanya propagandar, au unafanya by goodwill ni vema ukawa makini na hicho unachokiandika. Ama sivyo propagandar za kitoto zikizidi utashusha hadhi yako, ya Chama chako, na hatimaye ya JF. Hivyo fanya a little bit of research, kisha jipange kuleta propagandar hizo. Ama sivyo hautaeleweka kabisa ndugu yangu. Kwa hili naomba wale wote wenye nia ya dhati kuleta propaganda zao ili kuepuka aibu tujipange.
 
Hakika ni ngumu kumridhisha binadamu kama ilivyo vigumu ngamia kupita kwenye tundu la sindano.

Hata kama unaichukia serikali inayoitwa dhaifu lakini ikifanya jambo jema tunahitaji kuinga mkono.

Mama porojo!

Acha utani kwani hizo Nyumba zilijengwa usiku? Si zimejengwa mchana kweupe na hao wafadhili wa serikali ya CCM iliyopo madarakani for the past 50years. Hilo jambo jema la kuwasifia ni lipi?

Zilijengwa chini ya CCM na sasa wameshachukua chao na kuamua kubomoa sasa uwasifu kwa uzembe wao?

Let us be serious kuna ile jengo la hotel sea cliff ya Ali Hasan Mwinyi na yule Mhindi wa Lugoba Subash Patel lilijengwa awamu yake ikafuatia lile jengo la Ladwa Golden Tulip jirani na Police Mess yote yamejengwa kinyume cha sheria hata Mkapa alishindwa kuyabomoa mbona wankimbilia kwenye mikoko mbali. Nadhani wangeanza ha hayo hata Lowasa anayajua alipewa nini and then tufuatilie yote tena nchi nzima, Kigoma, Mwanza, Tanga na hata Arusha kwenye mbuga za wanyama zile Serena,,,, The list is long zote zimejengwa infront of CCm in day light ,,,, Waache usanii pambafu!!!
 
Mmmmh, lile jengo la TANESCO , Ubungo watalibomoa lini?

thubutu, wana jeuri hiyo!...zile zilikua ni kelele za chura tu, hii ni nchi isiyokua na mipango mkuu.
kama ipo ujue imeandikwa kwa chaki, kila anayekuja madarakani anafuta anaandika yake au anapandishia kwa juu.
kuna majengo mengi sana along Morogoro road kama ikifuata sheria yanapaswa kuvunjwa na wala si Tanesco tu.
na hilo ndio linanifanya niamini hata jengo la tanesco halitavunjwa ng'ooo!
 
nyumba zimevunjwa zikiwa na vitu ndani baada ya kukaidi kuhama... mama Dr Gerudi Lwakatare kakimbilia mahakamani kupinga sio jambo dogo kama unavyodhani kwamba serikali imewalipa kisirisiri. Huyu ni mbunge lakini kaguswa na bomoa bomoa ya mama Tiba.
Inaelekea huyu hajakubaliana na malipo waliyomlipa.
 
Hili la kuwa wenye nyumba hizi wamelipwa naamini linahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi kwa sababu taratibu ziko wazi kama mjengaji amekiuka masharti hakuna malipo hapo, zaidi sana huyo aliyebomolewa atatakiwa kulipa gharama za kubomoa.

Mimi nilifuatilia ubomoaji kwenye TV (channel ten,itv na tbc) lakini nilichoshuhudia ni uvunjwaji wa vijumba vidogovidogo 2-3. Sikuona nyumba yoyote ya maana ikiguswa (ikiwamo ile nyumba kubwa nyeupe). Mashaka yangu zoezi hili lisije kuwa ni kiini macho tu.
 
hongera serikali kwa kazi nzuri ya kuwabomolea waliojenga kawe beach maeneo ya bahari! mnaonesha kuwa sheria ni msumeno
 
Tunafaidikaje kuangalia matingatinga yao? Ukweli ni kwamba,kila anayevunjiwa nyumba yake ameshalipwa. Serikali pale inafanya maigizo.Fahamuni kuwa Serikali iko kwenye harakati za kuwaaminisha watanzania kuwa yenyewe na viongozi wake si dhaifu.
Hapo siungi mkono hoja 1000%! Hapo red, una ushahidi japo kidogo, zaidi ya hisia zako? Serikali haipaswi kumlipa yeyote aliyejenga pasipotakiwa, kinyume chake, mwenye nyumba alitakiwa avunje mwenyewe au kulipia gharama za uvunjaji.

Kasema bungeni juzi kwamba hata kama hatalibomoa yeye bado litakuja kubomolewa bila fidia kwa sababu liko kwenye hifadhi ya barabara.
@MAMA POROJO kwanza binafsi ninaiunga mkono serikali kwa hatua zake hizo, vyenginevyo nchi itakuwa haitawaliki kwani kila mtu atakuwa anafanya atakavyo. Hongera serikali kwa hilo. Lakini sitaacha kukiri kuwa SERIKALI NI DHAIFU.

Akifanya mtu wa nje tutasema katoa rushwa au ni ubabe wake, lakini TANESCO, shirika la umma, la serikali, linavamia hifadhi ya barabara, huu ni udhaifu mkubwa. Na huko fukweni au popote, mtu anaanza kuweka msingi wa jengo, anajenga hadi kumaliza, TANESCO serikali, DAWASCO serikali, Manispaa serikali, zinmsogezea huduma za umma kama maji na umeme na kuchukua kodi, hatimae mmoja anashituka toka usingizi na kusema hapa hukupaswa kujenga! HAPANA MAMA POROJO, HUU NI UDHAIFU MKUBWA!
 
Mama Tiba kaanza kuwatiba wagonjwa sugu...... thanks mama.

Kama kweli anataka kuwatibua wakubwa akabomoe nyumba ya mbunge wa Segerea maana amejenga kwenye
eneo lililotengwa kwa ajili ya soko,pia baa yake ya Nyantare pale kona ya Bima Tabata imejengwa kwenye
open space.
 
nyumba zimevunjwa zikiwa na vitu ndani baada ya kukaidi kuhama... mama Dr Gerudi Lwakatare kakimbilia mahakamani kupinga sio jambo dogo kama unavyodhani kwamba serikali imewalipa kisirisiri. Huyu ni mbunge lakini kaguswa na bomoa bomoa ya mama Tiba.


Now you are writing....
I think there is more to it than bomoabomoa ya kawaida...
Asante
 
Tatizo la serikali watabomoa nyumba za vidagaa. Za kwao hazitabomolewa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom