Bombardier and Government of Tanzania Sign Purchase Agreement for Two Q400 Turboprops

A
Sawa. Lakini tumekaa miaka yote bila ndege na hakuna shida kwa sisi wananchi wa kawaida ambao ndio asilimia kubwa ya Raia. Mimi mawazo yangu JPM angejenga Power Plant ya maana ambayo mitambo ni yakwetu kwa 100%, hii ingewagusa watanzania wengi sana.
Acha ubinafsi.. Kwakuwa ww unapanda daladala basi hutaki teksi ziwepo.. Hayo ni mawazo mgando... Hzo ndege kuna watu wanazihitaji na watazitumia.
 
Mwisho wa changamoto moja ni mwanzo wa changamoto nyingine.

Baada ya kununua ndege, changamoto iliyoko mbele ya serikali kwa sasa ni kuweza kuendesha hii biashara kwa mafanikio.

Ninategemea watakaopewa majukumu ya kuendesha hii biashara watakuwa wanafahamu vizuri udhaifu au sababu zilizopelekea ATCL kushindwa kuendesha shirika kwa faida na kwa sasa wanafahamu njia za kukabiliana na udhaifu au sababu hizo.

Kama mashirika mengine yanaweza, kwa nini ATCL isiweze?
Kabla ya ndege kama Qatar, Emirates na ndege nyengine za ndani na nje kuanza kuingia kwenye soko la anga, ni Air Tanzania pekee walokuwa wanaruka asilimia kubwa ya ruti za ndani na nje. ATC ilifikia hatua hata ya kuacha abiria kutokana na wingi wa demands ya tiketi zake. Kilichoua shirika au udhaifu wa shirika ni: WIZI WIZI WIZI.
 
K
Ni kweli mkuu,kuwa na nishati ya kutosha na pengine ziada inge- trigger economy kwani gharama za uzalishaji viwandani zingepungua hivyo kuongeza/kuvutia uwekezaji wa viwanda,ku-create ajira na kukuza uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.Kuifufua ATCL ni pride tu but ukiangalia kwa upana impact yake kwa uchumi wa nchi kidogo sana ,yaani ni prestige tu.
kila kitu kina umuhimu wake kwa nafasi yake... Achana na hyo akili ya kufananisha fananishs mambo...
 
Ndani ya miaka 10 iliyopita walikuwa wanatumia nini?
Kwahyo kwakuwa ndani ya miaka kumi ulikua unatembea kwa miguu hutaki tena kununua usafiri... Jaribu kuyapumbaza mawazo ya kimasikini... Otherwise hautakwamuka toka hapo ulipo
 
Sielewi logic yako ya kununua hisa PW while iko hoi ina madeni kibao inasubiri kufa tu ,kabla Fastjet kuanza ndio ilikuwa afadhali na karibia route zote za wafanyakazi wa serikali walikuwa wanapanda PW
Kwa domestic route PW hawana tofauti sana na ATC ya sasa .
Kitu cha kwanza ni kuivunja ATC na kuajiri staff wapya wachache na kutafuta management yenye uzoefu na biashara ya airline (Sio kuteua academician Dr/Prof kutoka vyuoni) .Waanze na domestic route kwanza

Sawa.
 
Sababu kubwa inayofanya mashirika ya umma yafanye vibaya hapa nchini ni kuingiliwa katika utendaji wake na wanasiasa (political interference). Hii ndio saratani ambayo imekuwa inatafuna mashirika ya umma tangu utawala wa awamu ya kwanza. Na msingi wa tatizo ni kwamba sheria nyingi zilizoanzisha mashirika ya umma nchini zimemfanya rais kuwa appointing authority wa mtendaji mkuu (CEO) pamoja na bodi ya wakurugenzi. Kwa vile rais ni mwanasiasa na malengo yake (na ya chama chake) ya kisiasa siyo lazima yafungamane na malengo ya ufanisi wa shirika, kigezo cha kwanza kinachozingatiwa katika kuteua CEO na bodi ni utiifu wa kisiasa (political allegience) kwa mteuzi na chama chake. Weledi, uwezo na uadilifu ni mambo ya baadaye (secondary criteria). Kama ATC haitarekebishwa ili ijiendeshe kwa uhuru (autonomously) ununuzi wa hizo ndege ni biashara kichaa (i.e., throwing good money after bad). Shirika la ndege la Ethiopia ni la umma na linaendeshwa kwa ufanisi mkubwa kwa sababu haliingiliwi katika utendaji na wanasiasa.
 
Wanunue hisa za KQ na waongeze nyingine wawe na atleast 50% ya ownership ili wawes=ze kuwa na equal control of the company.

Serikali iajiri management iliyotukuka kwenye hii biashara. Ila akiendelea na hawa wa ATCL hilo shirika limeshakufa tayari.
Rais alishasema hakuna atamuajiri atamlipa zaidi ya 15ml anaetaka zaidi aache kazi
 
Lakini jamani kwani ni lazima awe ni Mtanzania, hii si siasa, hii ni biashara na kama hakuna which is what I believe kwakuwa hatuna shirika la maana la ndege ambalo tunaweza kusema kuwa mtu anauzoefu toka huko, je kuna ubaya gani tukatafuta experts waliobobea kwenye hii industry wakatufanyia kazi inayoeleweka na huku wakitoa mafunzo (capacity building) kwa Watanzania wazalendo kuchukua nafasi hizo baada ya mikataba yao kwisha. Si lazima wawe watu weupe though I have no objection on that too if they are qualified. Hii industry ni very competitive, sisi hatupo serious sana, Top management za mashirika ya ndege ya EMIRATES, QATAL na mengineyo ya mashariki ya kati walikuwa ni Wazungu na walikiwa wakiwapunguza na kuchukua nafasi zao kadri ilivyohitajika walivyokuwa wakitengeneza human resource yao na mengine hadi leo hao experts bado wapo. Kwahiyo inapohitajika kweli kwamba hakuna Mtanzania mwenye hizo sifa let us opt for hiring.
Umeongea jambo la maana sana tatizo Rais ameshaweka Limit ya mshahara 15ml...kwa hela hiyo tunaweza kumpata Expert?
 
Kwahyo kwakuwa ndani ya miaka kumi ulikua unatembea kwa miguu hutaki tena kununua usafiri... Jaribu kuyapumbaza mawazo ya kimasikini... Otherwise hautakwamuka toka hapo ulipo
Sawa, lakini sio kwa stahili hiyo nchi inamatatizo ya maji, watu wanakunywa maji pamoja na mifugo, wewe unaona kununu Ndege kwa hayo Mabilioni ni sawa. Kwenye kampeni wanaahidi vingine huku wanatenda vingine.
 
Watu 76
Yaani Inashindwa Na Idadi Na Basi La Mwendokasi Lile Kubwa Linabeba Watu 200 Mpaka Waliosimama
Hivi Airbus Hawakuziona Jamani
Acheni dhihaka hata kama inabeba Abiria wachache vipi kuhusu muda wakukaa njiani
 
Management iliyoua ndege za ATCL bado ile ile au imebadilika?Hatuwezi kupata maendeleo kwa watu walewale,mawazo yaleyale.
 
Sawa, lakini sio kwa stahili hiyo nchi inamatatizo ya maji, watu wanakunywa maji pamoja na mifugo, wewe unaona kununu Ndege kwa hayo Mabilioni ni sawa. Kwenye kampeni wanaahidi vingine huku wanatenda vingine.
Hayo yote yatafanyiwa kazi but usafiri wa anga nao ni muhimu.. Unafaham serikali inaingia hasara kiasi gani inapotumia mashirika binafsi ya ndege... Magufuli alishaahidi kulifufua shirika la ndege kwenye kampeni zake if ahadi ni case kubwa kwako.....
 
Mwisho wa changamoto moja ni mwanzo wa changamoto nyingine.

Baada ya kununua ndege, changamoto iliyoko mbele ya serikali kwa sasa ni kuweza kuendesha hii biashara kwa mafanikio.

Ninategemea watakaopewa majukumu ya kuendesha hii biashara watakuwa wanafahamu vizuri udhaifu au sababu zilizopelekea ATCL kushindwa kuendesha shirika kwa faida na kwa sasa wanafahamu njia za kukabiliana na udhaifu au sababu hizo.

Kama mashirika mengine yanaweza, kwa nini ATCL isiweze?

Kwa Tanzania sijui kama wataelewa ulichomaanisha. Mode ya watanzania ni tumia, kikiharibika kitupe nunua kingine. Hatujui wala kujali maana ya maintenance, pesa ya maintenance inapelekwa bar au kwa kimada. Waliokwenda business school na engineering school hawapewi nafasi kuendesha hivi vitu au hata wakipewa na wao hawafanyi kipasacho kufanyika kuendeleza biashara.
 
Natamani sana tungefufua shirika la ndege la Afrika Mashariki.. tungekuwa more competitive kwenye soko la dunia.
 
300 na hakuna ndege
Sasa hao wafanyakazi 300 wanafanya kazi gani wakati hakuna ndege za kuzalisha mapato? Na kila mwezi hao watu wanalipwa mishahara na marupurupu kibao.Fikiria hapo kuna mtu anaitwa waziri na palikuwa na waziri anayeshughulikia usafiri. Wait a minute si Magufuli alikuwa waziri wa wizara inayoshughulikia usafiri?
 
Back
Top Bottom