Bomba la gesi mtwara kutandazwa leo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797



[h=2]Monday, August 26, 2013 | 9:00 AM[/h]



BOMBA la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, linaanza kutandazwa leo likianzia mkoani Lindi. Kutokana na hali hiyo, Serikali imeonya kwamba, yeyote atakayethubutu kuharibu miundombinu ya bomba hilo, atachukuliwa hatua. Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alipofanya ziara ya kukagua, ubora wa vifaa, rasilimali watu na maandalizi ya miundombinu ya kutandaza bomba hilo.

Wakati wa ziara hiyo ya siku moja, alikuwapo pia Balozi wa China nchini, Lu Youging, viongozi mbalimbali wa Serikali na viongozi wa kampuni zinazotandaza bomba hilo.

Profesa Muhongo alisema ameridhishwa na maandalizi yanavyokwenda, kwa kuwa kuna vifaa vya kisasa na imara.

Kesho kutwa (leo), utandazaji wa bomba unaanza rasmi na kwa maandalizi niliyoshuhudia, nina imani mradi huu utakamilika kabla ya Desemba mwaka 2014.

“Naomba Watanzania wawe na imani kubwa na watoe ushirikiano kwani utandazaji wa bomba utafanyika katika pande zote mbili, kwa maana ya nchi kavu na baharini.

“Mradi huu ni wa gharama kubwa na kama mnakumbuka, tulikopa fedha kutoka Benki ya Exim ambazo ni Dola za Marekani bilioni 1.2 kwa masharti nafuu.

“Pamoja na kwamba nia yetu ni nzuri, kuna baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya nchi hii, nataka kuwahakikishia Watanzania wote, kwamba usalama wa miundombinu hii utakuwa shwari na kama mtu anataka kushughulikiwa na Serikali, basi ajaribu kuihujumu atakiona cha mtema kuni.

“Hapa tumeshuhudia Watanzania 45 walioanza kupata ajira kama madereva, vibarua, kampuni za usafirishaji, huu ni mwanzo tu na ikifika sehemu ya kuhitaji watu wenye utaalamu, wataajiriwa wenye utaalamu,” alisema Profesa Muhongo.

Kwa mujibu wa Profesa Muhongo, mabomba yanayotandazwa ni ya aina mbili yakiwamo ya inchi 36 na uzito wa tani tano na yenye inchi 24 yakiwa na tani tatu ambayo alisema kwa ujumla wake yatadumu kwa miaka 30 na kama yakitunzwa vizuri yatadumu hadi miaka 70.

“Tunataka ifikapo mwaka 2016, tuwe na umeme wa megawati 3000 na mwingine wa ziada wa utakaokuwa ukiuzwa nje ya nchi ikiwamo Kenya ambayo imeleta maombi ya kuuziwa megawati 1000,” alisema.

Pamoja na kufanya ziara hiyo juzi, Profesa Muhongo alisema itakuwa ni endelevu na itakuwa ikihusisha waandishi wa habari.

Naye, Balozi Youging, alisema gesi ni kitega uchumi kizuri ambacho kinaweza kuwaondoa Watanzania katika umasikini.

“China ni moja ya nchi iliyonufaika na gesi na ndio maana raia wake ni wataalamu wa nishati hiyo, naamini upatikanaji wa gesi hapa Tanzania, utasaidia Watanzania kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni.

Kwa upande wake, Meneja Mradi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Mhandisi Baltazari Thomas, alisema hadi sasa watu 163 wamepata ajira katika awamu ya kwanza na kati ya hao Watanzania ni 68.




Read more: http://talkbongo.blogspot.com/
 
Ajira hadi sasa kuanzia LINDI ni 163; kati ya hao 68 ni WATANZANIA waliobaki yaani 95 ni WAGENI

Kwahiyo pamoja na kulipia hilo bomba Dola Billioni 1.2 bado pia Wataajiriwa wageni wengi zaidi ya WATANZANIA

 
Aaah wapi, mtwara kitanuka tu! Waambie JWTZ walinde watafanikiwa maana bado wanaheshimiwa na wananchi. Lakini hawa akina Kamihanda wameshakosa weredi wa kazi na heshima siku nyingi. Kajeshi haka ka raia wakakamavu ni chanjo cha vurugu chenyewe.
 
[FONT=lucida
sans unicode]Ajira hadi sasa kuanzia LINDI ni 163; kati ya hao 68 ni
WATANZANIA waliobaki yaani 95 ni WAGENI

Kwahiyo pamoja na kulipia hilo bomba Dola Billioni 1.2 bado pia
Wataajiriwa wageni wengi zaidi ya WATANZANIA

[/FONT]

mkuu, tuipongeze serikali kwa kutoa ajira kwa watu hao. ila ukumbuke kuwa bomba hilo linatandazwa kwa kutumia mitambo maalum na si kuchimba kwa mikono. hivyo ujuzi katika mradi huo ni kitu cha msingi na bila shaka jukumu hilo lipo mikononi mwa serikali ya china
 
Aaah wapi, mtwara kitanuka
tu! Waambie JWTZ walinde watafanikiwa maana bado wanaheshimiwa na
wananchi. Lakini hawa akina Kamihanda wameshakosa weredi wa kazi na
heshima siku nyingi. Kajeshi haka ka raia wakakamavu ni chanjo cha
vurugu chenyewe.

hahahaaaa, kitanuka wapi? chezea serikali wewe? wamedhibiti kila kona na hakuna kufurukuta. tunataka mpaka 2015 TATIZO LA UMEME NCHINI LIWE HISTORIA
 
Ajira hadi sasa kuanzia LINDI ni 163; kati ya hao 68 ni WATANZANIA waliobaki yaani 95 ni WAGENI

Kwahiyo pamoja na kulipia hilo bomba Dola Billioni 1.2 bado pia Wataajiriwa wageni wengi zaidi ya WATANZANIA


oh! My God
 
hahahaaaa, kitanuka wapi? chezea serikali wewe? wamedhibiti kila kona na hakuna kufurukuta. tunataka mpaka 2015 TATIZO LA UMEME NCHINI LIWE HISTORIA

Nao wanamtwara wanataka mpaka 2015 iwe historia kuwa ccm iliiongoza Tz
 
Nimevutiwa sana na spidi na utendaji wa huu mradi,ila bado sina imani kabisa na matunda ya hiyo gesi kama watanufaika watanzania au kale kakikundi ka watu kama katika sekta nyingine.
 
Mradi mzima ni mbinu ya uchaguzi ujao!manufaaa ya gesi sidhani kama kweli tutayaona hivi karibuni!
 
Serikali inaendelea kukandamiza wananchi wa mtwara kwa kutumia dola(jwtz)
subirini adhabu ya wananchi wa kusini 2015.
 
mkuu, tuipongeze serikali kwa kutoa ajira kwa watu hao. ila ukumbuke kuwa bomba hilo linatandazwa kwa kutumia mitambo maalum na si kuchimba kwa mikono. hivyo ujuzi katika mradi huo ni kitu cha msingi na bila shaka jukumu hilo lipo mikononi mwa serikali ya china


Haya sasa Angalia VIBARUA wa KIBONGO na PICHA ya CHINI VIBARUA wote ni wa KIBONGO na KICHINA... Umeona Wachina wanavyotufanyia? Wanaleta VIBARUA wao zaidi ya Wa Kwetu huo sio MPANGO wa kuipongeza SERIKALI





Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akizungumza na baadhi ya vibarua wa kitanzania wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ya kichina katika kambi ya kuhifadhia mabomba ya Nyamwage, wilayani Rufiji, Pwani.






Waziri Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kamapuni hiyo ya kichina.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom