Bofya:kwa watetezi wa mafisadi tu!!

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
5,221
3,167
DSC00161.jpg
DSC00160.jpg
DSC00164.jpg
DSC00165.jpg

Maji safi ni muhimu kwa kila Binadamu.Picha hizi zinaonyesha hali hali ya upatikanaji maji katika Vijiji viwili,Solya na Kilimatinde huko Manyoni Mashariki,Singida.Mashine za Serikali hazifanyi kazi tena kutokana na ubovu hivyo watu binafsi wamewekeza za kwao na kuchaji shilingi 100 kwa Ndoo moja ya lita 20.Habari na Picha kutoka kwa Mdau Baby Bosco.
 
Tupo tunawaza kujenga Fly-Overs wakati hata matatizo ya msingi kabisa wala hatujui kama yapo
 
Tunashangalia miaka 50 ya uhuru................................
 
Maeneo ya makazi yachaguliwe kwa kufuata upatikanaji wa huduma muhimu kama maji, mvua za kutosha, kutokuwepo uwezekano wa mafuriko, udongo unaofaa kwa kilimo kwa wakulima, upatikanaji wa malisho kwa wafugaji n.k.
Elimu na maarifa ya kuishi itolewe kwa wananchi ili wasiishi maeneo ambayo ni nusu jangwa huku wakilalamika shida za maji. Pia waelimishwe kutunza vyanzo vya maji na mazingira yao kwa ujumla.
 
Abudhabi wapo jangwani lakini wana maji ya kutosha...
Tanzania tumezungukwa na mito na maziwa kila kona lakini hatuna maji ya kutumia wala kunywa....!!!!!!!!!!!1
 
Tupo tunawaza kujenga Fly-Overs wakati hata matatizo ya msingi kabisa wala hatujui kama yapo
Nimekuwa nikijiuliza viongozi wetu hawafiki sehemu zenye matatizo kama hizi au hawaoni hizi picha kwenye magazeti .Pesa ambazo tunataka kuwalipa Dowans zinaweza kujenga VISIMA 18,800 kwa thamani ya milioni 5 kwa kisima.Tutasubiri wafadhili waje kutusaidia wakati tukiangalia priorities zetu ni zipi tukaachana na vitu vya kujikweza na kuwashungulikia mafisadi, mambo kama haya yako ndani ya uwezo wetu.
 
Back
Top Bottom