Bodi ya Wachumi Tanzania

Mwanafalsafa na Mgonjwa wa Ukimwi

Nashukuru sana kwa michango yenu.

Naomba nijibu baadhi ya vipengele vilivyoulizwa na MgonjwaUkimwi. kuna baadhi ya maswali yamerudia ila nitatoa ufafanuzi

a)Kwa sasa matatizo ni mengi, na mifano ipo mingi sana, na baadi ya post imeoanishwa. Mfano sera za kodi katika sekta mbalimbali madini, uwekezaji, petrol &petroleum products,n.k.
jinsi gani serikali inaangalia suala la unemployment, Umeme na athari zake viwandani, income distribution na mambo kama hayo

b)Jinsi gani mambo haya yanatatuliwa: Nadhani wewe unalojibu sahihi zaidi yangu kwa kifupi Siasa zaidi inatumika kuliko principles za uchumi. Mfano, kama unafuatilia suala la inflation je unafikiri kweli serikali inayo taarifa sahihi na za kutosheleza kuhusu mfumuko wa bei? Unafikiri hatua sahihi na muafaka zimechukuliwa? Uchumi tumeambiwa unakuwa 6.8% hali ya watu ni mbaya zaidi kila kukicha, je huo uchumi unakua au ni siasa? utegemezi wa budget 40%,wakati waziri anakosesha serikali kodi kwa kutoa msamaha ni uchumi huo au siasa? na mengine so bado hakuna ufumbuzi kwa matatizo ya kiuchumi tuliyonayo. Ama inawezekana wanafanya kazi zao ila wanasiasa wanawaharibia.

hayo ni maoni yangu na baadhi ya maoni ya watu wengine

c)na (d) Bodi hii itakuwa proffessional bodi kama zilivyo nyingine isipokuwa itakuwa huru ili kuiwezesha kufanya kazi zake huru.
lengo lake kuu kwanza kuwasaidia members wake kukuza proffession yao (wachumi) kuanzia mwanafunzi wa uchumi ambaye atakuwa amejisajili na bodi hiyo, wachumi wote kwenye vyuo vikuu, wafanyakazi wa serikali na private sector na itakuwa ni ya kitaifa n.k

Jukumu kuu la pili kama ulivyoanisha ni kufanya kazi za tafiti mbalimbali kwenye masuala yenye utata . nitakupa mfano Juzi juzi umeona REDET wametoa report ya tafit yao (je ina impact kwa walio serikalini), je wanachi wameelimika? nini kinafuatia hatujui. So Bodi hiyo itakuwa ikifanya tafiti mbalimbali zinazolenga kuendeleza, kuelimisha na kushauri jamii na serikali kwa ujumla.

kazi nyingine za bodi kutoa ushauri wa kitalamu, kwa watu binafsi, financial institutions, private and public companies, serikali na mashirika ya kimataifa.

e) Nani Financer, Hili sio suala la kuogopa kwa sasa (ila bado linajadiliwa) kutaua na annual fees, subscriptions ni kiasi gani siwezi kujua hadi watakapo kaa na kuamua. Wachumi ni proffessionals naamini watatumia proffession yao katika kuraise fund. Mimi binafsi sitii shaka kwa hilo. n.k

F) Athari za wachumi binafsi zitakuwa positive, maana kila wakati kutakuwa na seminary mbali mbali kwa member zitakazokua zinalenga kukuza proffession. Pia kwa wale ambao wanafanya consultancies wataweza kukutana na wenzao ambao wanweza kushikiana na kufanya kazi bora zaidi. Na ieleweke kwamba wachumi nao wanatofautina (health economist, econometrician, industrial econ, n.k)kwa specialization hiyo wale waliokuwa wamejiajiri wenyewe ndio muda mufaka pia wa kufanya networking.

Ikitokea kuna kazi bodi imepewa itatolewa kwa members kwa merits za uzoefu, elimu na pia fair bid. so hakuna atakaye athirika iwe katika vyuo vikuu, private sector and serikalini

f) nadhani muundo nimeshasema ingawa bado majadiliano yanaendelea. Sio lazima bodi iwe inatoa kibali cha mtu kufanya kazi kama mchumi isipokuwa ukiwa na kibali hicho utaweza kusaidiwa katika kufanya kazi zako tofauti na asie nacho(so kutoa kibali haitakuwa primary aim ya kuanzishwa kwa bodi, hii inatokana na maoni ya watu))

g)Ukubwa itakuwa ya kitaifa, mchumi mmoja mmoja atakaribishwa, vile vile kama organisation watakaribishwa.


kama sijakujibu naomba uniwie radhi ila nipo kwenye pressure fulani hadi jumamossi nitakuwa settled nitaweza kujibu kama utakuwa na maswali zaidi. Maoni zaidi yanakaribishwa
 
Ndugu wana JF,

Nimesukumwa sana kuleta hoja hii hapa mbele yenu baaada ya kuona ni namna gani Uchumi wa nchi unaendeshwa bila kuzingatia maslahi ya nchi.

Kwa sasa Tanzania haina Bodi ya wachumi ambayo ingekuwa inatoa maoni(proffessional advice) mbalimbali, kukemea, kuelimisha, kushauri, kutafiti n.k kwa manufaa ya serikali, umma, na vyombo mbalimbali kuhusiana na sera mbalimbali, matokeo mbalimbali(Volatility of Oil prices, Gold, Increase in electricity cost, umasikini, afya, finance,n.k)

Kwa sasa serikali inategemea wachumi waliopo kwenye ofisi zake, ESRF, REPOA na Universities katika kuandaa na kutekeleza sera zake ikiwa wote wanategemea funding kutoka serikalini thus hawawezi kuishauri serikali vinginevyo pale inapotokea sera zake hazikuleta matunda yaliyotarajiwa.

Hivyo bodi inahitajiwa ili kuwahusisha wachumi wote walioma ndani nje ya serikali, pamoja nje ya nchi na wengine wanaopenda kujiunga na bodi hiyo kuisadia serikali kwa kushauri, kuelimisha, kutafiti, kukemea sera chafu kama za madini(kuanzia utafutaji, uchimbaji, uuuzaji, na hata ulipaji kodi), Sera za ubinafsishaji na Uwekezaji zisizomjali Mtz, ukusanyaji wa kodi, unemployment n.k).

Chombo hiki kilikuwepo wakati wa Mwl.JK ila baada ya Mh AHM kuingia madarakani viongozi wote wa chombo hiki na wengi wa members wao walipewa madaraka na majukumu makubwa serikalini wakashindwa kufanya kazi za chama na hata kuitisha vikao ili kuchagua viongozi wengine mwisho wake kikatoweka.

Je nini maoni yenu wana JF kwa kutaka kuanzisha kwa bodi hiyo?
Naamini humu kuna wachumi humu JF, wewe kama mchumi nini mchango wako kwa Tz?


Hint: Tumeona body ya wahandisi, wahasibu, boharia, wanasheria (refer to Ms. Karume issue)n.k jinsi wanavyoplay role yao collectively. Ni lini sisi wachumi tutaplay part yetu?

Nakaribisha maoni hapo na pia kwenye PM yangu

Bowbow hii kitu nilikua naisubiria kwa hamu sana imeishia wapi?

Nimeona sehemu www.wachumi.org na www.wachumi.com (ingawa haina content)je hizo ndio web za hii kitu ama vipi mkuu.

tupe majibu mkuu
 
Mnigeria (Bowbow),
Mie siyo mchumu. Ila niseme wazi kabisa kuwa ntakuwa nanyi katika hili walau kwa maombi (kama unaamini dini). Sintachangia kwani uchumi umenipitia kushoto labda kama mtakuwa mnajadili mambo ya kwenye anga zangu basi naweza kujulisha ninalolifahamu.
Kila la kheri katika uanzishaji. Haba na haba hujaza kibaba.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Kimsingi hoja ni nzuri japo inachalleng mbalimbali hasa tukizingatia kuwa Tanzania isu sio ushauri wa kitaalam bali kukubali ushauli wa kitaalam. Tuna paper nyingi nzuri sana lakini wenyedhamana hawataki kutekeleza. British Council mangement Forum ni moja ya board inayochambua mambo mengi muhimu kwa taifa letu lakini impact yake ni ndogo sana katika serikari ilifikia mahali nilisema ''professional boards are there to ease frastructions to professionals by debating within themselves funy things happening in the society as administered by the system''.

Hata hivyo naungamkono uanzishwaji wa board hii ila ushauri wangu juu ya muundo nadhani ili iweze kuwa na impact zaidi isiendeshwe kama academi board nyingine mfano board ya uhasibu yaani isiwe na mamlaka ya kuhakiki na kutoa kibali/license za wachumi katika kada mbali kwa kotoa mitihani. Kwa kufanya hivi members watakuwa interested kupata vyeti viweze kuwasaidia katika maswala ya ajira na kusahau lengo mahususi la kushauri maswalamuhimu yakiuchumi nchini. Kunaboard ambazo zinaendeshwa kwa namna hiyo na zinamafanikio makubwa sana Mfano the Chartered Institute of Logistics and Transport (CILT - UK) and the Institution of Highway and Transportion (IHT - UK) zote ni za Uingereza na mimi ni member wa board board hizi. Kimsingi zinamchango mkubwa sana inafikia mahali mapaka serikari inazipa ruzuku kufanya kaadhi ya tafiti na zinapublication nyingi sana.

Katika board hizi taaluma yako ndio inadictate uwe mwanachama wa namna gani mfano ordinary member, profession member and expert member. Nadhani muundo huu waweza kuwa mzuri.
 
BOWBOW alionekana hapa mara yamwisho mwezi december 2007.
Sijui kama bado ana intrest na issue hii tena vinginevyo kwa mwaka mzima wa 2008 asingepotea kwenye anga za jf na hasa katika thread aliyohusika kuiasisi. Mawazo yake mazuri yamepotelea hewani maskini.
Jamani mbona wa tz tuko hivyo? Tuna kila wazo zuri lakini mwisho wetu ni mawazo kulala usingizi.
Au alichaguliwa kuwa wazirikwenye sirikali ya JK na kisha akajitoa JF na mawazo yake?
 
Waheshimiwa, Nashukuru kwa concern yenu.

Kwanza niseme kuna progress kubwa sana kwenye hili suala la kuanzisha hiki chombo cha wachumi. Mhusika mkuu anasema kutakuwa na mkutano wa kwanza wa brainstorming wa wachumi wote 22 March 2009. lengo litakuwa ni kujadili muundo, Katiba, na kazi za chombo hiki. Hadi sasa kuna task force ya watu 7 lakini bado tunahitajika wengine zaidi.

Kwa taarifa nilizopewa hivi punde kuna wadau 56 hadi sasa wameshejitokeza kukiunga mkono wazo hili na kumekuwa na mawasiliano ya email kati yao. Hivyo kama kuna mtu anapenda kujiunga katika hili anakaribishwa kwa kufanya registration Wachumi Tanzania na kutuma email kwenda info@wachumi.org ama wachumi08@gmail ili uweze kupata regular updates.

Ngoja niwasiliane na mdau mkuu niwape updates za kutosha and will comeback with details
 
Back
Top Bottom