Mabulangati
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 796
- 164
Ndugu zangu ni mara kadhaa kumekuwa na thrend kuhusu bodi ya mikopo na namna inavyofanya kazi. Watu wengi walitoa mawazo na ushauri za uhakika na yanayotekelezeka. Pamoja na hayo, kulikuwa na swala la bodi ya mikopo kuwayaachia mabenki kazi ya distribution ya mikopo na collection of debts bila kutoza riba kwa kuwa hela hizo zingetoka serikalini. Bodi ibaki kufanya kazi za uratibu pekee. Pamoja na hayo yote na mambo mengi yaliyosemwa Bungeni na katika kongamano liliongozwa na Kitila Mkumbo pale UDSM, bodi imeng'ang'ania kazi isiyoiweza na kina Mwaisoba wanabaki wakisema watu wanafanya bodi kuwa jimbo la uchaguzi.
Leo tunavyozungumza bodi hawana pesa za kuwapa wanafunzi kwa mhula unaokuja na kwa habari nilizozisikia mtu akiongea na mtu mwingine kwa simu kutoka ofisi fulani nyeti ni kwamba kuna uwezekano mkubwa vyuo kadhaa hasa UDSM kufunguliwa baada ya wiki mbili badala ya jumatatu ijayo ya tarehe 27/02/2012. Hii ni kutoka na kuogopa migomo na migogoro isiyokua ya lazima vyuoni.
Nawasihi wanafunzi wenzangu wa Ardhi, tuwaombe watawala wetu waungane na UDSM kutofungua chuo mpaka wahakikishe kuwa wanafunzi wanapata fedha za kujikimu kabla ya kurudi vyuoni.
Mwenye mawazo zaidi au taarufa za uhakika kuhusu kusogezwa mbele tarehe ya kufungua chuo UDSm atupatie tafadhali