NeutralPolitics
New Member
- Nov 2, 2016
- 1
- 3
Kwa Bodi ya Mikopo. Je, hii ni haki?
Hii ni habari ya kweli. Mimi ni mtumishi wa uma kwa miaka 20 sasa. Kwa kuwa hali ya taaluma katika shule zetu za msingi na o-level haikuwa njema kwa kipindi kirefu, ambapo ni jambo ambalo halikuwa limepewa kipaumbele na mamlaza zilizopaswa, ilinilazimu kuwapeleka watoto wangu ambao wamefikia wanne sasa,katika shule za kulipia hadi kidato cha nne.
Hivi sasa wawili wameingia vyuo vikuu katika michepuo ya utabibu, lakini kilichowapata ni kuwa hawana mikopo eti kwa kuwa walisoma shule za kulipia wana uwezo.
Hii si haki kwa sababu zifuatazo.
1. Kunyimwa mkopo mtoto wangu, mtu ambaye nimekuwa nikilipa kodi ya PAYE hadi sasa sio kunitendea haki hata kidogo. Je nitafutiwa PAYE ili badala yake nilipe Milion 5 (mara watoto wawili sasa walioingia vyuoni) karo ya watoto wangu? Kama sivyo kwa nini niendelee kulipia wengine?
2. Gharama za karo kwa shule za awali ilikuwa mwisho Milion 2.5 kwa mtoto. Hii tulijitahidi kujinyima kama familia ili angalau tuwafikishe watoto katika ndoto zao. Leo hii karo ya mafunzo kozi za utabibu ni Million 5 na laki moja hadi Million 6 na laki saba. Je hapa uwezo wangu mimi umepimwaje na kuniona eti kwa kuwa watoto walisoma private o-level basi wazazi tuna uwezo, na hivi naelekea kustaafu?
2. Ukweli ni kuwa wakati wote wa kusomesha watoto wangu shule za awali tumejinyima sana sana kwa kila hali. Chakula chetu, matumizi mengine yote yamekuwa ni kwa dhiki tukijitahidi kwa ajili ya watoto hawa.
3. Mimi nadhani kila kijana anayeingia chuo, kwa kuwa anakuwa amepita umri wa miaka 18, na atakapomaliza anajenga taifa, anapaswa kuonwa kama raia mwenye haki zake sawa na raia wengine. Tofauti na hapo ni ubaguzi kwake pasipo sababu. Nasi wazazi baada ya kujitoa kwa awali basi tuachwe tujiandalie maisha ya kustaafu sio tena tuje kuishi kwa dhiki, ukizingatia kuwa hawa watoto nao watakuwa na maisha yao na wajibu kwa familia zao baada ya kumaliza. Mishahara ya nchi yetu kulingana na uduni wa uchumi inajulikana. Kipato ni kidogo na hatuwezi wote kukimbilia katika siasa ili tukachume posho.