Bodi ya mikopo na Rushwa damudamu... Mlalahoi hana chake zaidi ya ukondakta!!!!!

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
787
755
Maana ya Rushwa ni matumizi mabaya ya ofisi ya UMMA kwa manufaa binafsi... Sasa simwellewi waziri anapodai kuwa watoto wa vigogo ndo wenye akili wakati tunajua fika wao ndio vilaza namba Moja hapa mjini.. Japo kuna wachache wao waelewa flani hivi... Kusema watoto wa Vigogo wanapewa asilimia kisa division One sio kweli hata chembe... Yeye anataka kujustify rushwa ili hali twajua hukweli... 2010 onward hatudanganyiki!!! UKWELI: Bodi ya mikopo inatumika kufilisi nchi kwa kulipia vilaza wakasome India, Russia, China na kwingineko pamoja na chuo cha kata UDOM... tAFADHALI rushwa isitenganishwe na Bodi ya mikopo kwa kuwa wanazaliwa tumbo moja....


WAZIRI wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa ameiagiza Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu kubadilisha mfumo wa utoaji mikopo kwa sababu mfumo uliopo unawanufaisha watoto wa vigogo na matajiri.
Waziri Kawambwa alitoa agizo hilo jana wakati tayari Rais Jakaya Kikwete ameeleza nia yake ya kuunda tume maalumu kwa ajili ya kuchungunza mfumo mzima wa utoaji mikopo hiyo.

Rais Kikwete alisema serikali yake imeamua kufanya hivyo ili kuhakikisha kuwa tatizo la mikopo linalowakabili wanafunzi wa vyuo vikuu nchini linakwisha.

Alisema kamati hiyo itakuwa imeundwa ifikapo mwezi Januari mwakani.

Kwa muda mrefu yamekuwepo malalamiko kutoka kwa wanafunzi walalahoi kwamba hawatendiwi haki na bodi ya mikopo, kwa vile watoto wa vigogo wanapewa mikopo ya asilimia 100 wakati wao wanapunjwa licha ya wazazi na walezi wao kutokuwa na uwezo.

Akizungumza na watendaji na wajumbe wa bodi hiyo jijini Dar es Salaam jana, Waziri Kawambwa alisema wanafunzi wengi wanaopata mikopo ya asilimia 100, ni watoto wa vigogo na wasomi, wakiwamo maprofesa na madaktari. <HAPA ANATHIBITISHA RUSHWA ILIYOPO BODI::: KWA NINI WASIFUNGWE KWA MATUMIZI MABAYA YA MALI YA UMMA maana anawajua hao vigogo>

“Ili uweze kupata mkopo kwa asilimia 100, lazima uwe na sifa ya kupata alama ya ‘Division One au Two’ (daraja la kwanza au la pili). Ukweli ni kuwa wenye mazingira ya kupata alama hizo ni watoto wetu (mawaziri, maprofesa, madakatari)na si wa mfugaji, mkulima na hata mlalahoi ,’’ alisema Dk Kawambwa.
<Hapa ana-Justify uongo:::: ukweli ni watoto wasomao town au shule nzuri na si wa vigogo kama asemavyo kwa kuwa wao ni vilaza japo watapelekwa India, China, Poland na Russia kwa mkopo>
Kufuatia hali hiyo, Kawambwa pia aliitaka bodi hiyo kukiangalia upya kigezo hicho na kuagiza kuwa sifa hiyo isiwe kigezo pekee katika kutoa mikopo kwa asilimia 100.

Kawambwa alikwenda mbali na kutaka sheria namba 11 ya mwaka 2004 iliyounda bodi hiyo pamoja na muundo wa utendaji wake ubadilishwe ili uweze kukidhi mahitaji.
<Hii ni siasa yeye si mwanaharakati bali mtendaji::: atupe tarehe ya lini muswada utapelekwa bungeni sio chai na vitafunwa tuu>
Awali Mkurugenzi mtendaji wa bodi hiyo George Nyatega aliitaka serikali kukubali ombi lao la fedha za mikopo zinazotolewa zirejeshwe pamoja na riba.

“Kulingana na hali halisi ya mazingira ya elimu yalivyo hususani karo za shule kubadilika, mabadiliko ya thamani ya fedha, sasa tunataka urejesheshwaji wa fedha za mikopo uwe na riba,’’ alisema Nyatega.

Akijibu ombi hilo, Waziri Kawambwa alisema Serikali italifanyia kazi.

Akizungumza na wafanyakazi wa wizara yake katika siku yake ya kuanza rasmi kazi, Dk Kawambwa aliahidi kuboresha maslahi ya walimu na wastaafu wa vyuo vya elimu ya juu vya umma na kwamba atafanya kazi kimyakimya kama 'mchwa' na kuwataka wananchi kupima utendaji wake kwa matokeo ya kazi kwa sababu anaamini kuwa kazi inaweza kufanyika vizuri na mafanikio makubwa bila kutumia maneno makali.

Alitaja vipaumbele vinne atakavyofanyia kazi miaka mitano ijayo ambavyo baada ya uongozi wake katika wizara hiyo anataka wananchi na vizazi vijavyo wamkumbuke, ikikwamo kumaliza matatizo ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.


Habari hii imeandaliwa na
Mwanachi
 
INAPENDEZA!ila kinachotakiwa ni utekelezaji maana imekuwa ni wimbo kwa viongozi kuongelea mambo muhimu kama haya ukija kwenye utekelezaji ni zero!
 
Back
Top Bottom