Bodi ya mikopo na propaganda ya kulaumiana.....................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Bodi%20ya%20mikopo%20na%20propaganda%20ya%20kulaumiana.....................
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, George Nyatega akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam. (Picha na Yusuf Badi).
01_11_4txq2r.jpg
 

Bodi ya Mikopo ‘yapasua jipu'


Imeandikwa na Stella Nyemenohi; Tarehe: 26th January 2011 @ 07:51

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeshutumu kile ilichoeleza kuwa ni kugeuzwa jimbo la uchaguzi na baadhi ya watu, kwa kutumia mgongo wake kutoa shutuma bila kuzifanyika uchunguzi, ili wasikilizwe na wanafunzi wa elimu ya juu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, George Nyatega, jana aliwambia waandishi wa habari Dar es Salaam, kwamba Bodi yake imekuwa ikigeuzwa ajenda na watu hao huku ikihusishwa moja kwa moja na migomo ya wanafunzi wakati kasoro nyingi zinachangiwa na vyuo vyao na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Nyatega alisema lengo lake si kujibu tamko la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ambao hivi karibuni ulitoa tamko kutaka Bodi ipanguliwe.

Lakini taarifa ya maandishi iliyogawiwa kwa waandishi na pia kuchapishwa katika baadhi ya magazeti jana, Mkurugenzi Mtendaji aliijibu UVCCM kwa kusema imekurupuka kwa kutoa shutuma ambazo hazijafanyiwa uchunguzi.

"Bodi inapenda kusisitiza, kwamba hata kama ikivunjwa, kama kiongozi mmoja wa UVCCM
walivyokurupuka kusema, hata chombo kitakachoundwa badala ya Bodi nacho itabidi kivunjwe baadaye endapo changamoto zinazosababishwa na wadau wengine na si Bodi ya Mikopo, hazijapatiwa ufumbuzi," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Alisema suala la Bodi kutumiwa kisiasa halikuanza leo wala jana, bali ni la muda mrefu kwani hata Serikali za Wanafunzi katika kujinadi ili zikubalike, zimekuwa zikitumia mgongo wa HESLB kushawishi wanafunzi wenzao .

Nyatega ambaye alikiri kukosekana ushirikiano mzuri kati ya Bodi, TCU na vyuo vya elimu ya juu ya utoaji mikopo kwa wanafunzi, alivitupia lawama zaidi vyuo vikuu vya umma, kuwa
vimekuwa vikiingiza Bodi yake kwenye lawama zisizo za msingi kutokana na kutofanya kazi yao ipasavyo.

Alisema, "taasisi nyingi za elimu ya juu ambazo wanafunzi wao wanakopeshwa na Bodi zimekuwa zikichelewa kuleta taarifa muhimu zikiwamo orodha za wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliosajiliwa, matokeo ya mitihani na orodha ya majina ya wanafunzi wanaokwenda katika mafunzo kwa vitendo.

"Matokeo ya kucheleweshwa kwa taarifa hizo, yameibua malalamiko miongoni mwa wanafunzi na hivyo kuelekeza shutuma kwenye Bodi bila sababu za msingi," alisisitiza.

Alisema licha ya Bodi kuwa na hati ya makubaliano na vyuo juu ya mambo kadhaa, lakini bado upo upungufu katika kutekeleza.

Alitoa mfano, kwamba katika makubaliano hayo, vyuo vinapaswa kuleta orodha ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliosajiliwa ndani ya siku 30, lakini vyuo havizingatii hilo.

Kuhusu TCU, mtendaji huyo wa Bodi alisema pia imekuwa ikichelewesha taarifa za wanafunzi waliodahiliwa ili waandaliwe mkopo wao.

Alitoa mfano, kwamba zipo taarifa ambazo Bodi ilipaswa kuzipokea Novemba mwaka jana, lakini majina yaliletwa mwezi huu.

Alitoa mifano mingine ya vyuo ambavyo vilikumbwa na migomo na maandamano huku Bodi ikitajwa kuwa chanzo, kikiwemo Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) na kusema chuo hicho kilishindwa kuwasilisha namba za akaunti za wanafunzi kwa wakati na hivyo kusababisha ucheleweshaji kwa zaidi ya wiki tatu.

Kwa upande wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) ambacho wanafunzi waligoma hivi karibuni, chuo kiliwasilisha orodha ya majina kikiwa kimechelewa mwezi mzima. Wakati huo huo kiliwasilisha majina bila namba za akaunti.

Juhudi za kumpata msemaji wa TCU ili atoe maelezo juu ya shutuma hizo za Bodi hazikuweza kuzaa matunda kutokana na simu yake kutopatikana.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwa karibu na vyuo vya elimu ya juu, ili kutambua na kutatua migogoro inayozuka mara kwa mara.

Aidha ameitaka Kamati ya Wabunge iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mgogoro uliozuka hivi karibuni katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kutoishia chuo hicho pekee bali itembelee na kuchunguza migogoro ya vyuo vyote vikuu nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza semina ya wabunge wa CCM Dar es Salaam juzi usiku, alikiri kuwapo kwa matatizo mengi katika vyuo hivyo, ambayo yamekuwa kero kwa wanafunzi na wahadhiri na hivyo kuzua migogoro ya mara kwa mara.

Alisema uongozi wa wizara hiyo, hauna budi kutembelea menejimenti na uongozi wa wanafunzi na kuwa nao karibu ili kuelewa matatizo yaliyopo badala kutokea tatizo, wizara iegemee taarifa ya kuambiwa na si kushuhudia.

Alisema kimsingi matatizo ya vyuo vikuu ni changamoto kubwa kwa Serikali na mengi yametokana na ongezeko kubwa la wanafunzi mwaka hadi mwaka, wakati bado miundombinu ya shule ikiwa haitoshelezi.

"Changamoto tuliyonayo ni kuendana na idadi ya ufaulu wa wanafunzi kwani ongezeko ni
kubwa na miundombinu ni ile ile na wakati mwingine inafikia chumba cha kulala wanafunzi wawili hulala sita, tatizo hili pia huwa ni kero na kuchangia migogoro vyuoni," alisema.

Alisema pia tatizo lingine ni ufinyu wa bajeti ya mikopo kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi ambapo pia mfumo wa utoaji mikopo nao umekuwa ukichangia kutokana na kulalamikiwa hali ambayo imeilazimu Serikali kuunda Tume kuchunguza mfumo huo na kuona namna ya kuuboresha.

Waziri Pinda alisema matatizo mengine yanahusu uongozi wa vyuo hivyo kwa upande wa wanafunzi lakini pia wahadhiri.

"Kwa hapa tutajipanga kuhakikisha tatizo linajulikana na kuwekwa wazi, ndiyo maana tunasisitiza Kamati ya Taaluma iliyoundwa ishughulikie pia masuala ya utawala katika vyuo hivi.


 
vipi mikopo ya wanafunzi, ina mana wanafunzi wanakopesha kwa kwenda kusoma nje/ndani ya nchi.
halafu malipo inakuwaje, watalipa wazee wao au wakipata kazi, ndio wataanza kulipa huo mkopo/deni?
 
HTML:
Alitoa mfano, kwamba katika makubaliano hayo, vyuo  vinapaswa kuleta  orodha ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliosajiliwa  ndani ya siku 30,  lakini vyuo havizingatii hilo.  

Kuhusu TCU, mtendaji huyo wa Bodi alisema pia imekuwa ikichelewesha   taarifa za wanafunzi waliodahiliwa ili waandaliwe mkopo wao.  

Alitoa mfano, kwamba zipo taarifa ambazo Bodi ilipaswa kuzipokea Novemba mwaka jana, lakini majina yaliletwa mwezi huu.   

Alitoa mifano mingine ya vyuo ambavyo vilikumbwa na migomo na   maandamano huku Bodi ikitajwa kuwa chanzo, kikiwemo Chuo Kikuu Kishiriki   cha Elimu Mkwawa (MUCE) na kusema chuo hicho kilishindwa kuwasilisha   namba za akaunti za wanafunzi kwa wakati na hivyo kusababisha   ucheleweshaji kwa zaidi ya wiki tatu.

Hizi ni kutupiana mpira wa lawama kwa sababu hata wao wangeweza kutuma mtumishi wao kwenda TCU kuhakikisha takwimu zote zinapatikana kwa wakati............tatizo ni kuwa makosa yanapofanyika hakuna anayechukuiwa hatua..............................
 
Code:
vipi mikopo ya wanafunzi, ina mana wanafunzi wanakopesha kwa kwenda kusoma nje/ndani ya nchi.
halafu malipo inakuwaje, watalipa wazee wao au wakipata kazi, ndio wataanza kulipa huo mkopo/deni?

Ni wao walioingia mkataba wa mikopo hiyo...........hivyo wakipata kazi kwa maana ya kujiajiri au kuajiriwa na kuwa na uweoz wa kulipa watakatwa au kujikata wao wenyewe klila mwezi deni hilo......................
 
<table class="contentpaneopen" border="0"><tbody><tr><td class="contentheading" width="100%">Bodi ya mikopo: Vijana CCM ni wazushi </td> <td class="buttonheading" align="right" width="100%">
</td> </tr> </tbody></table> <table class="contentpaneopen"><tbody><tr> <td class="createdate" valign="top"> Tuesday, 25 January 2011 21:23 </td> </tr> <tr> <td valign="top">

Boniface Meena
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB), imeurarua Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), kutokana na kile ilichokiita ni kutoa taarifa, "za kizushi na za kukurupuka," na kutaka isigeuzwe jimbo la uchaguzi la wanasiasa.Tamko hilo la HESLB chini ya kichwa cha habari, "Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu haihusiki na Migomo ya hivi karibuni katika Vyuo vya Elimu ya Juu," linajibu mapigo ya tamko la UVCCM, lililotaka mapinduzi ndani ya bodi hiyo ikiituhumu kushindwa kukidhi mahitaji ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

Hata hivyo, ikitoa ufafanuzi wa tuhuma moja hadi nyingine kati ya zilizoelekezwa kwake, bodi ilipiga kombora ikisema, "mmoja wa viongozi UVCCM, amekitolea mfano Chuo Kikuu kishiriki Mkwawa (MUCE) kama mfano, wakati akitoa tamko la kukurupuka dhidi ya bodi bila hata kufanya uchunguzi wa sababu za ndani za migomo ya wanafunzi wa vyuo."

Vijana hao wa CCM katika tamko lao, walisema, "UVCCM umebaini kuna urasimu unaofanywa na watendaji na haiingii akilini, Mkwawa University wagome kwa kutolipwa posho zao na baada ya siku moja walipwe posho zao baada ya kugoma. Jambo hili si utamaduni wa vijana wa Kitanzania, wale wote wanaohusika CCM ichukue hatua,"

Umoja huo ulienda mbali ukisema, hauko tayari kuona vijana wakiendelea kugoma na wale wote wanaotaka kuanzisha utamaduni mpya wa utawala ambao mpaka watu wagome ndipo ufumbuzi upatikane, wapishe.

Lakini, taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, imeonyesha kukerwa na tamko la vijana hao wa chama kilichoshika hatamu ya dola huku ikitua mzigo ikisema , migomo yote iliyotokea katika vyuo vya elimu hivi karibuni haihusiani na bodi hiyo kwa vyovyote.

"HESLB imetaka isigeuzwe jimbo la uchaguzi ambapo kila anayetaka kusikilizwa na wanafunzi wa elimu ya juu, atumie kwa kutoa shutuma ambazo hazijafanywa uchunguzi wa aina yoyote," ilipiga kombora jingine.

Katika tamko hilo, HELSB ilitoa ufafanuzi kwamba wakati mgomo wa MUCE hapo Januari 14, mikopo yao ilikuwa imekwishalipwa kupitia benki tangu Januari 7 mwaka huu, hivyo madai ya malipo hayo yalifanyika baada ya wanafunzi kugoma si kweli na, "ni uzushi mtupu." "Pia wakati wanafunzi wa Chuo kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE), kinatangaza kugoma Januari 18 mwaka huu, bodi ya mikopo ilikuwa imekwishafanya malipo ya mikopo hiyo kupitia chuoni tangu Januari 11, hivyo siyo kweli kwamba walilipwa baada ya kugoma,"ilifafanua zaidi sehemu ya tamko hilo.

Kuhusu madai ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), bodi hiyo iliweka bayana kwamba, msimamo wake ni kuwa haiwezi kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea na ambao bodi hiyo haijapokea matokeo yao ya mitihani ya mwaka wa masomo uliopita.

HELSB ambayo imekuwa ikielekezewa makombora ya migomo ya wanafunzi wa elimu ya juu huku kukiwa na sauti za wadau mbalimbali wakitaka ifumuliwe na kuundwa upya, ilizidi kutoa ngumu ikisema haiwezi kutoa mkopo kwa mwanafunzi mwenye udahili wa zaidi ya chuo kimoja.

"Hivyo, wanafunzi mwenye tatizo hilo wanashauriwa kuwasiliana na vyuo vyao na TCU ili bodi iarifiwe na chuo gani wanaruhusiwa kujiunga nacho," ilisisitiza.

Kuhusu Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), bodi hiyo ilikwepa tuhuma hizo na kuruka kimanga huku ikisisitiza, si sahihi kulaumiwa bodi hiyo kwa mgomo wa chuo hicho kwani bodi inatekeeza maelekezo ya Serikali ambayo yanalenga kuzuia upandishaji holela wa ada katika vyuo vya elimu ya juu.

Tamko hilo likizungumzia malalamiko ya Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro(MUM), kutaka bodi ilipe ongezeko la ada, HESLB iliweka msimamo thabiti ikisema itaendelea kutumia viwango vya ada vya mwaka wa masomo 2008/2009 kwa mwaka wa masomo 2010/2011, kwa waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo hadi hapo Serikali itakapoamua vinginevyo.

Kuhusu madai ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), bodi hiyo ilifafanua kwamba itatoa mikopo ya mafunzo ya vitendo kwa programu ambazo vyuo vimezibainisha katika mitaala kuhusiana na mafunzo ya vitendo na si vinginevyo.

"Mikopo ya mafunzo ya vitendo itatolewa tu baada ya bodi kupata taarifa na orodha kutoka vyuoni ikiainisha wanafunzi wanaotakiwa kwenye mafunzo hayo..., muda na mahali wanakokwenda. Hivyo migomo iliyotokea UDOM haina uhusiano na bodi ya mikopo,"ilitua mzigo huo.

Kuhusu matatizo ndani ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), bodi ilizidi kuongeza wingu zito lililogubika chuo hicho, ikisema tatizo la chuo hicho linapaswa kupelekwa TCU.

Tamko hilo lililojaribu kutoa kile kilichoiitwa ufafanuzi wa tuhuma nyingi na za muda mrefu dhidi ya bodi, liliweka bayana kwamba , wanafunzi wanaosoma kwa mfumo wa (Open and Distance Learning) hawana sifa ya kukopeshwa hivyo KIU inatakiwa kupeleka suala lake TCU na siyo bodi.

Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), sehemu ya tamko ilifafanua kwamba, bodi ilifafanua mafunzo kwa vitendo yatatolewa kwa programu ambazo vyuo vimezibainisha katika mitaala kama ndizo zinazohitaji mafunzo kwa vitendo na si vinginevyo. "Pia mikopo katika robo ya pili, kwa ajili ya chakula na malazi kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza inatolewa mara baada ya kuwasilisha orodha za wanafunzi waliosajiliwa vyuoni hivyo mikopo haitatolewa pasipokuwa na orodha hiyo."

Hata hivyo, bodi hiyo imelalamika taasisi nyingi za elimu ya juu ambazo wanafunzi wake wanakopeshwa na bodi kwamba zimekuwa zikichelewa kupeleka taarifa muhimu zikiwemo orodha ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliosajiliwa, matokeo ya mitihani na orodha za majina ya wanafunzi wanaokwenda katika mafunzo kwa vitendo.

"Matokeo ya kucheleweshwa kwa taarifa hizo yameibua malalamiko miongoni mwa wanafunzi na hivyo kuelekeza shutuma kwenye bodi bila sababu za msingi,"imeeleza taarifa hiyo.

Hili ni tamko la kwanza kwa mwaka huu kutolewa na HELSB lenye kubeba maudhui mazito kuhusu sababu za migomo katika vyuo vya elimu ya juu, ambayo imekuwa ikiitikisa Serikali na kuifanya itumie nguvu na muda mwingi kuutatua.

Mgomo uliotikisa zaidi ni wa hivi karibuni katika UDOM ambao ukiacha wahadhari kugoma, baadhi ya wanafunzi waligoma na kuandamana wakitaka fedha za kufanyia mafunzo ya vitendo, lakini walielezwa kozi zao hazikuwa na fungu kama ilivyosisitizwa pia na tamko la bodi. Ends
</td></tr></tbody></table>
 
Back
Top Bottom