Bodi ya mikopo HESLB nini hiki?

Je, wauonaje utendaji kazi wa mfumo huu wa bodi ya mkopo?

  • Unafanya kazi vizuri sana

    Votes: 1 14.3%
  • Ni wa kawaida

    Votes: 0 0.0%
  • Ni m'baya kupindukia

    Votes: 6 85.7%

  • Total voters
    7

shatisuruali

JF-Expert Member
Jul 28, 2016
893
2,659
Habari ndugu zangu!
Kuna vitu HESLB lazima itambue kuwa inacheza na maisha ya watu. Mwaka huu umekuwa ni mwaka wenye changamoto nyingi hasa kwa wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu. Wanafunzi wengi wameshindwa kupata Vyuo kwa wakati, Mkopo umekua historia kwa wanafunzi wengi.
Kuna utaratibu ambao bodi ya mkopo wameuanisha ili kupinga matokeo ya kukosa mkopo. Nisahihisheni kama ntakosea.
Mwanafunzi anatakiwa kujaza fomu zinazopatikana katika URL ya http://olas.heslb.go.tz anaziprint hizo fomu na kuambatanisha taarifa zinazohusika. Ofisa wa mkopo wa chuo husika anakusanya fomu hizi na kuzituma bodi ya mkopo fomu hizi hazipokelewi na bodi kutoka kwa mwanafunzi moja kwa moja. na mwisho ni tarehe 31 januari 2017.
Tatizo: Tovuti hii inachukua zaidi ya dakika 7 au 8 kumaliza kufunguka kwenye mtandao wenye kasi sana. Na ikifunguka kuna link nyingi ambazo hazifanyi kazi. Kurasa ambazo hazijapangiliwa. Kuna mapungufu makubwa kwenye mfumo huu napata wasiwasi mkubwa hasa kama maombi yangu yatafika kwa wakati na usahihi. Imenichukua zaidi ya siku tatu kujaribu kuupata mfumo huu bila mafanikio na hauna maelezo ya kutosha. Nathubutu kusema MFUMO HUU HAUFANYI KAZI KABISA.

Bodi ya mkopo jamani hii si sawa, kama mumeamua kutumia mifumo ya kompyuta basi hakikisheni mifumo yote inafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu. Ni wanafunzi wengi sana wataoathirika na matatizo katika mfumo wenu na kukosa fursa ya kupata mkopo na kuendelea na elimu ya juu.

Pamoja na haya nakuja ofisini kwenu. Mnaidhalilisha serikali yetu.

“Whatever you do, do it well. Do it so well that when people see you do it, they will want to come back and see you do it again, and they will want to bring others and show them how well you do what you do.”

Walter E. Disney
homepage.JPG
home.JPG
help.JPG
 
Back
Top Bottom