Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Wamulikeni Watu Hawa

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,366
2,397
Kumekuwa na kundi la vijana wake kwa waume kati ya 10 hadi 15 wanaweka meza pale ubungo darajani karibu na mitambo ya umeme ya songas na kujifanya wanachezesha kamari. Sina tatizo na mantiki ya mchezo huu kwa sababu nafaham ni mchezo unaokubalika kama unaendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zake. Tatizo ni namna wahusika hawa wanavyochezesha mchezo huu. Mara kadhaa nimekuta wakidhulumu watu kwa mbinu za ujanjaujanja na hata kukwapua pochi za watu wanaojaribu bahati yao kwa kucheza mchezo huu. Sina shaka, hawa si wachezesha kamari, bali ni kikundi cha wahuni wanaopaswa kuchukuliwa hatua badala ya kuachwa hapo wakiendelea ‘kuliza watu’.
 
Ni kweli serikali inapaswa kuwachukulia hatua wahuni hawa wanaowaliza wapita njia, hasa akina mama. Inauma sana.
 
Dodoma wapo pia. Wanakaa kwenye mahema ya blue, wanaweka pikipiki, tv, redio wa kuzuga eti zinashindanishwa.
Mmoja yuko kwenye gari.
Mwingine anaongea kwa microphone
Mmoja anachezesha kamari.
Alafu cha kushangaza na akina mama wnajihusisha humo.

Ukija dodoma ukiwaona hawa wanakaa karibu na stendi ya shabiby near round about.
Na pia wako nyerere square.

Msiende tafadhali ni matapeli na wezi.
 
Back
Top Bottom