Boda Boda - SUNLAG

Hii biashara mwanzoni ilikuwa ina faida sana, ila kwa siku hizi TRA wameziwekea kodi ya mapato ambayo ukipiga hesabu unakuta faida si kubwa sana kama ukiwa na moja.

Kwa mfano kwa sasa pikipiki nzuri inauzwa Tshs 1.8 M ukiongeza na kodi, bima, namba, road licence n.k inafikia kama Tshs. 2.1 hapo hiyo laki tatu inajirudia kila mwaka (kodi ya mapato, bima na road licence)

Na pia mapato yake kama unapokea kila wiki ni Tshs 42,000/= hapo ina maana 7000/= kwa siku moja ila kwa wiki unamwachia dereva siku moja kama mshahara wake ambapo service na matengenezo madogo chini ya 3000/= anafanya dereva kwa gharama zake.

sasa mwaka uwa una wiki 52 so take 52 x 42,000 = 2,184,000/= kwa mwaka hapo sijapiga hesabu za matengenezo makubwa ambayo yakitokea unaletewa tajiri ambayo nayo yanapunguza sana kipato. Pia kuna vitu kama kuisha matairi, shock ups, taa kuvunjika, betri kwisha nguvu bila kusahau ajali ndogo ndogo n.k

Hivyo ukitaka ilipe inatakiwa ukae nayo zaidi ya miaka miwili ambapo pikipiki inakuwa imechoka sana na gharama za matengenezo ni kubwa.

Vitu fake pia vipo ila kama ukiwa makini unaweza kupata bidhaa original ila kama unapenda vitu cheap au ukiwa unamwachia dereva tu atengeneze bila wewe kufuatilia anaweza kukuwekea vitu fake ili ale cha juu

Sasa ili hii biashara ilipe na uifurahie inabidi ufanye kifuatacho ambacho mimi uwa nakifanya; ingia mkataba na dereva wa pikipiki wa maandishi kuwa akuletee tshs 3.5 M kwa mwaka mmoja na nusu kisha unamwachia pikipiki inakuwa yake. Hiyo inamwezesha kufanya kazi kwa bidii na kwa kuwa wanapata ziada nyingi atajitahidi akusanye ili alipe hiyo hela kwa muda mfupi pikipiki iwe yake. Pia ataitunza sana kwani itakuwa ni mali yake.

Hiyo mbinu hapo juu ndio imenifanya mpk leo niendelee na hiyo biashara na kila pkpk nimeifungulia daftari na nimefungua akaunti. Ila nakutahadharisha kuna madereva wanaweza kukutia kizunguzungu mpk unaweza kupiga mtu makofi.

Ukiwa na nyingi na ukitumia mfumo huyo hapo juu utaona faida kidogo ila kama ukitumia njia a kuchukua pesa bila mkataba utakuwa unawapa ajira madereva tu ila wewe mwenyewe hupati chochote na waliovuruga utaratibu ni TRA wameweka kodi ya mapato kubwa ambayo sio realistic ukitazama na kipato anachopata mwenye pkpk na kwa ufupi mimi niko mbioni kuachana na hii biashara.

NB: Hii biashara si nayoitegemea kuendeshea maisha, ninaifanya tu kama hobby yangu kufanya ujasiriamali

Mkuu, Dawa ya TRA ni kuunda Kampuni,then unasajili ulipaji kodi kupitia kampuni,so mwisho wa mwaka unapeleka kodi kulingana na matumizi yako na uendeshaji wa biashara yako.
kimsingi,unakata matumizi yako yote kupitia kampuni,e.g kodi yako ya nyumba (ukiwa kama chairman kwa kampuni)allowance nyinginezo,gharama za vipuri ,etc.kinachobaki ktk kipato ndo unapeleka kodi TRA so sometime unaweza kushtukia kodi halali haizidi laki na nusu.

ndo wahindi na wafanyabiashara wakubwa wanavyofanya.TRA hawajui na hawana mbinu za kukusanya kodi zaidi ya kuwabana wafanyabiashara wadogo wasio na kampuni za LTD,
kimsingi wanapata kodi kulingana na ignorance ya wafanyabiashara wengi wa TZ
 
usilolijua kweli kiza kinene.... kumbe janja za ponjoroz ndo hiziiii.....
 
Back
Top Bottom