Boban atinga airport na kandambili

TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,787
2,078
Boban wa pili kushoto.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ jana alikuwa kivutio kwa mashabiki, wasindikizaji na hata baadhi ya wasafiri waliomuona wakati wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuelekea Sudan. Uvaaji wa Boban, ndio uliowavutia watu kumtizama, kutokana na kuvaa kama mtu asiyesafiri.
Boban alikuwa amevaa fulana, suruali ya kimichezo ‘trakisuti’ na kandambili, hivyo kusababisha watu kuvutika kumuangalia, huku baadhi yao wakibaki kujiuliza kuhusu vituko vya nyota huyo ambaye mashabiki humuita Balotteli wa Bongo.
 
Mbona hata mie hupendelea kuvaa sandals zozote zitazokuepo around ili kuepa longolongo za kuvua na kuvaa viatu. Ni mapenzi tu ya mtu.
BTW, there is only one Boban, Zvonimir Boban, left-footed na kiungo mpishi mahiri kabisa wa zamani wa Dinamo Zagreb, Milan 1899 na timu ya taifa Croatia, hao wengine wa kwenu ni wakuchonga tu si lolote si chochote...they don't worth the comparison.
 
Boban kasafiri mara nyingi sana na nchi tofauti tofauti, inawezekana mwanzoni wakati anaanza kupanda ndege alikuwa anatinga misuti, kipapaa n.k, may be baadae akaona watu wengi wanavaa simple tu ndo maana kaamua nae kutinga kihivyo. Isitoshe kuna usumbufu mwingi sana ktk checking kila mara kuvua na kuvaa viatu ni heri kuvaa makobazi au ndala tu.
 
balloteli wapi hana lolote ajitaidi tu soka imsaidie asilewe misifa astaafu aishie kuuza ugoro na kucheza draft
 
Mbona hata mie hupendelea kuvaa sandals zozote zitazokuepo around ili kuepa longolongo za kuvua na kuvaa viatu. Ni mapenzi tu ya mtu.
BTW, there is only one Boban, Zvonimir Boban, left-footed na kiungo mpishi mahiri kabisa wa zamani wa Dinamo Zagreb, Milan 1899 na timu ya taifa Croatia, hao wengine wa kwenu ni wakuchonga tu si lolote si chochote...they don't worth the comparison.

Absolutely.
Boban ni mmoja tu, nae ni Zvonimir Boban aliyepata kukipiga Aszocione Calcio Milan ama AC Milan klabu yenye mafanikio zaidi hapa Ulimwenguni ambayo pia imechezewa na nyota wengi zaidi ya klabu yoyote hapa ulimwenguni...
Hao wengine ni ushuzi tu.

Forza Milan
 
Taib sheikh, taib.
 
salute G Chomba

Unanifurahisha sana na ile damu ya AC Milan... and you have been consistent

POle tu kwa last week kupoteza mechi but you are a good AC Milan Ambassador, anzisha fan club mkuu - kwa wabongo
 
Janjaweed ishu ni kuwa...
Inaaminika kuwa kila mpenzi wa Soka basi ni shabiki wa AC Milan...
Hili liko wazi.
 
Kwani tatizo hapo lipo wapi?

Tuna mazoea mabaya sana mkuu, usishangae mawaziri wapya nao watakwiba ngawira kwa kuwa waliotangulia walikwiba. Kwani kandambili zinazuia ndege isiruke? au mlitaka atinge buti la kamanda Nkunda.
Mimi nimeipenda stail ya haruna. Tusiwe watumwa wa akili.
 
Boban wa pili kushoto.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Haruna Moshi ‘Boban' jana alikuwa kivutio kwa mashabiki, wasindikizaji na hata baadhi ya wasafiri waliomuona wakati wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuelekea Sudan. Uvaaji wa Boban, ndio uliowavutia watu kumtizama, kutokana na kuvaa kama mtu asiyesafiri.
Boban alikuwa amevaa fulana, suruali ya kimichezo ‘trakisuti' na kandambili, hivyo kusababisha watu kuvutika kumuangalia, huku baadhi yao wakibaki kujiuliza kuhusu vituko vya nyota huyo ambaye mashabiki humuita Balotteli wa Bongo.

angevaa MZUNGU ingeonekana kawaida ila kwa kuwa ni mweusi ishakuwa nongwa!ishi kwa uwezo wako na nafsi inavyopenda usiangalie wala kuiga yasiyokuwa na manufaa kwa watu wengine
 
Back
Top Bottom