TANZIA Bob Makani afariki dunia

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223
Habari za uhakika muda mchache uliopita nimepata taarifa ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kabla ya Mbowe... Mzee Bob Makani amefariki.

R.I.P Bob Makani

Kwasababu ya msiba huu, CHADEMA wamesitisha Operesheni Okoa Kusini na wanarejea Dar kwa shughuli ya msiba.

Source: Kutoka kwa ndugu zake.

UPDATES...






Bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ikipepea nusu mlingoti katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaa kufuatia kifo cha Mwasisi wa chama hicho, Mahmoud 'Bob' Makani



Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu, Mahmoud 'Bob' Makani




Baadhi ya waombolezaji



DAR ES SALAAM, Tanzania

Aliyekuwa Naibu Gavana wa Tanzania na mwasisi wa Chama cha Demokrasia (Chadema) marehemu, Mahmoud Nyange Makani maarufu Bob Makani, anatarajiwa kuzikwa katika kijiji cha Negezi kilichopo mkoani Shinyanga.

Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Hassan Makani amesema kuwa, marehemu Makani ameacha mke na watoto saba na wajukuu wanane na anatarajiwa kuagwa rasmi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kesho. kwa hisani ya Kiganyi
 
Last edited by a moderator:
Makani.jpg


RIP Mzee Bob Makani
Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi

Amina
 
Poleni wakuu,tatizo lake lile lile au jingine? Maana nakumbuka kulikua na uzi alilazwa aghakan!!
 
Confirmed

Naona uzi wa awali ulifutwa kabla hata mtu mmoja hajapost. Lakini wanaJF tujifunze jinsi ya kuleta habari kubwa kama hizi,
mzee wa njaa alileta kama tetesi halafu breaking news hivi inawezekana kweli? Nawapongeza MoDs kwa kuwa makini.

Tukiachana na hilo, poleni sana wanaCDM na watanzania kwa ujumla. RIP Makani.
 
Mungu mwenye wingi wa Rehema Uilaze mahala pema peponi Roho ya Mpendwa wetu Bob Makani Amen.
 
Mzee wa Njaa na Wana JF,
Nawapa Pole Familia ya Marehemu Bob Makani na Ndugu na Jamaa na Marafiki, Kazi ya Bwana haina Makosa, Bwana alitoa na Bwana alitwaa, Na Jina la Bwana Yesu na lihimidiwe.
Nawakilisha



Habari za uhakika muda mchache uliopita nimepata taarifa ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kabla ya Mbowe...Mzee Bob Makani amefariki.

R.I.P Bob Makani


Source: Kutoka kwa ndugu zake.
 
Mwenyezi akutangulie mzee wetu,mwambie Baba wa Taifa CDM inakaribia kuwakamata wahujumu uchumi kama enzi zake... mwambie tunamwomba apendekeze adhabu.
 
Back
Top Bottom