Blood Group Yenye Rhesus

je nikweli kwamba mtu mwenye blood group yenye rhesus - hawezi kupata mtoto,au watoto watakuwa wanakufa?
 
Mimi si Daktari ila kwa vyovyote vile ninauhakika hiyo si kweli.Ni percent ndogo sana ya watu ndo hawana Rhesus factor,sasa ingekuwa kila mwenye Rhesus factor hapati mtoto basi tungeona wagumba wengi saaaaaaaaana kuliko ilivyo sasa.
 
Je nikkweli kwamba mtu mwenye blood group yenye rhesus- hawezi kupata mtoto?

Si kweli...mtu mwenye Rhesus -ve anaweza pata mtoto. Rhesus factor hupatikana katika seli nyekundu za damu (red blood cells) na zaweza kuwa positive (Rh +ve) au negative (Rh -ve). Watu wengi hasa weusi (waAfrica) ni Rh +ve..karibu 95%, na wachache ni Rh -ve. Tatizo hutokea inapokuwa mwanamke ni Rh -ve, na akakutana na mwanaume Rh +ve na kupata ujauzito (wakikutana wote Rh +ve, au wote ni Rh -ve, au mwanume Rh -ve na mwanamke Rh +ve kunakuwa hakuna tatizo kabisa).

Mwanamke Rh -ve anapopata ujauzito wa mwanume Rh +ve, basi mtoto kule tumboni kuna uwezekano akawa Rh +ve. Na ikitokea hivyo, basi wakati wa kuzaliwa, mchanganyiko wa damu ya mama (Rh -ve) na mtoto (Rh +ve) utasababisha mama kuzalisha antibodies nyingi mwilimwake, lakini mara nyingi huwa hazimuathiri mtoto wa kwanza. Mtoto wa kwanza huanzisha reaction kwa kustimulate kuzalishwa antibodies.

Sasa kwa mimba zinazofuatia ambazo mama anakuwa tayari ana antibodies zilizozalishwa baada ya mimba ya kwanza, zitakuwa zinashambuliwa na antibodies hizo na watoto kufa!

Cha kufanya: Ikigundulika kuwa mama ni Rh -ve na baba ni Rh +ve, basi mama huyo inabidi achome sindano (anti-D) ambayo itazuia antibodies kwenye damu ya mama zisishambulie mtoto na kumuua. Sindano hii huchomwa ndani ya masaa 72 kabla ya mama kujifungua. Kuna wakati mweingine sindano inabidi ichomwe hata miezi mi3 kabla ya kujifungua kwani mchanganyiko wa damu na kuuawa kwa mtoto kunaweza tokea katika miezi mi3 ya mwisho ya ujauzito.

NB: Mwanamke Rh -ve anaweza kuzaa na kwa na watoto zaidi ya mmoja ila inahitajika achomwe sindano ya/za anti-D kwa wakati!
 
Asante Daktari. Nilikuwa naihitaji sana hii knowledge...kwenye mambo yangu fulani. SHukrani sana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom