Blandina Nyoni, You are tired, you deserve to be fired!

Meningitis... kwakweli Nyoni kashindwa kazi sasa....
huyu mama hawezi kazi ameshindwa kuwashauri mawaziri wake vizuri.Haji mponda kila anachoulizwa hajui,lucy nkya hajui kutofautisha MAT na baraza la madaktari Tanzania.yaani kumejaa vichekesho na ulimbukeni.wizara ipo kwa ajili ya kupiga mihuri kwa wale wanaonda india tu!!!shame.ajira za mwaka huu ambazo zilitegemewa kuanza mwezi wa kumi zimechelewa kuliko mwaka jana yaani badala ya kuimprove mambo yanakua mabaya.this is why i personally recommend kwamba huyu mama hafai!!!!!!!
 
yote ni kukosa uwajibikaji, kama hamna bajeti mbona watoto wa vigogo wamepangiwa mijini

pili mishahara halipi blandina nyoni zinalipa halmashauri hivyo hakuna sababu kuchelewa kuwapangia vituo vya kazi[/QUOTE

haiingi kichwani,cv tutume wote halafu siye mpaka saa hizi hatujapata post za kazi.watoto wa vigogo wamepangiwa sehemu zote nzuri,wengine tutatupwa mwisho wa dunia.huu ni uonevu,where is the fairness?yaani wanaanza kutubagua mapemaaa.she has to leave
 
Kweli huyu mama anajitahidi sana ni mfano bora wa kuigwa, wanaojaribu kumhukumu wanafanya hivyo kwa hisia potofu tu!!
:poa

ndugu upo kwenye system au unaongea tu?unajua uozo unaoendelea kwenye hiyo wizara?au unafikri watu wanapenda tu kumponda?
 
Nina Vijana rafiki zangu wamewai kufanya kazi na huyu mama. Wanasema ana matatizo na mapungufu yake kama walivyo viongozi wengi tu serikalini lakini huyu mama anawazidi utendaji wa kisasa watendaji wengi sana

Rafiki yangu alinimbia kama kuna kijana atashindwa kufanya kazi na huyu mama basi hawezi kufanya kazi na bosi yeyote katika serikali . Mabosi wengi wenye umri kama wa huyu mama ni wazito. Huyu mama yuko sharp. Kama itachukua mwaka ku alocate kazi za madaktari basi ujue angekuwepo mwingine ingekuwa miezi 18.

Unachosema mkuu ni sahii kabisa, huyu mama ni mchapa kazi kupita maelezo. Ni kiongozi anayependa na kukuza vipaji vya wafanyakazi vijana, ni mwalimu anayefunza wafanyakazi vijana jinsi ya kufanya kazi na kujitegemea ni yeye pekee aliyeajiri vijana wengi kuliko ma PS waliomtangulia hapo Wizarani, fanya research, pitia pale Wizarani uone jinsi vijana walivyokuwa wengi, ni tofauti kabisa na ilivyokuwa hapo mwanzo. Suala la ajira ni suala mtambuka ambapo ujumuisha Wizara zaidi ya moja yaani Wizara ya Afya, Utumishi na Wizara ya Fedha so si suala la kumlau mama Nyoni peke yake. Amefanya mengi sana pale Wizarani na tunatakiwa tumpongeze kwa sauti si kila siku kulaumu tu. Mama Nyoni atabaki kuwa PS mchapakazi na mweledi aliyekuwepo kwenye Serikali ya Mkulu mpaka sasa.
 
JK anawachekea hawa aliowateua!
wanamshauri vibaya ndio hawa.kama wameshindwa kuongea na ma-interns na kutuliza hali ya mambo unategemea watamshauri rais kitu cha maana?hata JK ajue anapopata tuzo za kuboresha afya ajue kuna watu wanakesha,wanatembea mabarabarani saa tisa za usiku,wanajichoma na sindano na kuathirika,wanaacha familia zao,wanatukanwa na kupigwa na wagonjwa,wanaishi kwa stress ya kufikiria wagonjwa,wanapigwa loba za mbao wakati wanatoka kazini usiku n.k


watu hawa(ambao hawasamehewi kodi kama barrick) ndio wanaofanikisha haya na mara nyingi hatuwezi kuwalipa mihela mingi lakini ni kuthaminiwa kwa kazi wanayoifanya.wananchi wa kawaida wanawathamini sana iweje viongozi wasiwathamini,viongozi hawa wametoka wapi??nalia kwa uchungu!!!!!!!
 
wakuu poleni sana na misukosuko ya siku nzima ya leo.poleni kwa uchovu wa kelele kati ya madaktari na serikali.
pia tuwaombee wale wote waliotangulia mbele ya haki hata kama siku zao ziliandikwa lakini kwangu mimi inawezekana vifo vyao vimetokana na mgogoro huu.huko nyuma niliwahi kutoa post iliyokuwa inamtuhumu bi blandina nyoni na kumshauri ajiuzulu kwa sababu mambo yalikuwa hayaendi vyema pale wizarani.kama kuna uadui kati yako na wadau wengine wa sekta ya afya ni wazi hutaweza kutekeleza majukumu yako.kipindi kile kulikuwa na matatizo kadhaa lakini mojawapo ni kuchelewa kuajiri watumishi wa afya bila sababu za msingi,tatizo hili limerudia tena mwaka huu tena hali ni mbaya zaidi kuliko mwaka jana.mwaka jana watu waliajiriwa mwezi wa 10 na ushee lakini mwaka huu tangazo limetoka mwanzoni mwa mwaka huu.kwangu mimi huu ni uzembe wa wizarra yako hata kama hazina wana tatizo kama pinda alivyojaribu kukutetea jana.

Tatizo la allowance kwa interns
hili tatizo halijaanza leo,sio kwamba zilikuwa ndogo la!!ni kwamba hakuna utaratibu unaoleweka wa kuwalipa interns.yaani intern akishaondoka pale wizarani basi!!wizara haimkumbuki na huko alipokwenda hawamjali kwani sio muajiriwa wao(sijui pinda jana alifukuza kina nani).kinachotokea ni intern kuteseka kwa kukosa allowance au kufunga safari za kila siku wizarani ili apate allowance zake.nakumbuka mliwahi kuunda tume ya kutembela na kutambua matatizo ya interns nchini kote,iliyoongozwa na director wa BMC dr majinge,yule dokta wa private hospitals Dr pamela na dokta mmoja wa muhimbili Dr lembariti.sijui kama walikueleza nini lakini ninachoamini hukufanyia kazi maoni ya interns(jamani, mpaka watu wangoma huwa wanapitia steps kadhaa!!) na kama uliyafanyia kazi basi maoni ya interns hayakuletwa kwa usahihi.

Tatizo la interns waliogoma muhimbili

hivi kulikuwa na umuhimu gani wa kuwafukuza wale interns?na hata baada ya viongozi wa MAT kukushaurini kwamba interns wale warudishwe kwani walikuwa wanadai haki zao,nnyie mkaleta dharau.

Kuhusu madhara ya mgomo wa madaktari
siamini kama unvitumia vizuri vyombo vyetu vya usalama au unakurupuka katika kuamua na kushauri mambo.ki msingi uzembe wako umeleta maafa,watu wamekufa kwa kiburi au uzembe wako.
mwisho naendelea kusisitiza wewe ndiye engine ya uendeshaji wa wizara na kama watanzania walivyoshuhudia wizara yako imeshindwa kulihandle vizuri jambo lilokuwa dogo sasa limekua ni maafa.nina wasiwasi kuendelea kuwa na wewe kama katibu mkuu ni kukaribisha mabalaa na maafa makubwa ambayo hatujawahi kuyaona tanzania.

ni vyema sasa ukafanya maamuzi yatakayokupa heshima na msamaha kwa mungu. JIUZULU utapangiwa shughuli nyingine zisizogusa moja kwa moja maisha ya mwanadamu!!

nawasilisha...................
 
Pamoja na madhaifu yote ya Blandina Nyoni, kwangu mimi she is an iron lady, no nonsense lady!. She never bow down to any pressure over her dead body!. Akiwa Accountant General alimgomea CAG kuwa auditors wanakuja kufanya ukaguzi with malice aforethougts kuwa kuna wizi hata kabla ya ukaguzi. Akahamishiwa Malialisili ndiye aliyeving'oa vile visiki kama kina Severe!. Kwa miaka yote akiwa PM maliasili ndipo wizara ikawa top exihibitor wa DITF for 3 consecutive years!. Sasa kaletwa Afya kusafisha mauza uza!. Na atasafisha vilivyo!.
 
Pamoja na madhaifu yote ya Blandina Nyoni, kwangu mimi she is an iron lady, no nonsense lady!. She never bow down to any pressure over her dead body!. Akiwa Accountant General alimgomea CAG kuwa auditors wanakuja kufanya ukaguzi with malice aforethougts kuwa kuna wizi hata kabla ya ukaguzi. Akahamishiwa Malialisili ndiye aliyeving'oa vile visiki kama kina Severe!. Kwa miaka yote akiwa PM maliasili ndipo wizara ikawa top exihibitor wa DITF for 3 consecutive years!. Sasa kaletwa Afya kusafisha mauza uza!. Na atasafisha vilivyo!.
pasco hapa hatubishani who is who.mimi ninachotaka kuona mtu mmoja wa wizara ya afya anawajibika.kwangu mimi kama nilivyowahi kutabiri huko nyuma ni your iron lady.angeonyesha kwa kulihandle hili swala bila kelele na vifo vya watu.
 
Pamoja na madhaifu yote ya Blandina Nyoni, kwangu mimi she is an iron lady, no nonsense lady!. She never bow down to any pressure over her dead body!. Akiwa Accountant General alimgomea CAG kuwa auditors wanakuja kufanya ukaguzi with malice aforethougts kuwa kuna wizi hata kabla ya ukaguzi. Akahamishiwa Malialisili ndiye aliyeving'oa vile visiki kama kina Severe!. Kwa miaka yote akiwa PM maliasili ndipo wizara ikawa top exihibitor wa DITF for 3 consecutive years!. Sasa kaletwa Afya kusafisha mauza uza!. Na atasafisha vilivyo!.
i think your iron lady is no more.......thats why we fired her
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom