BLACKBERRY SERVICE VODACOM Vs ZAIN

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,855
8,251
Ndugu zangu leo nimeona niongelea juu ya huduma ya BIS kwa kutumia blackberry kati ya kampuni ya Zain na Vodacom,ingawa hii mada imewahi jadili hapo kitambo,kuwa ni kampuni ipi ambayo inatoa huduma murua.
kwa utangulizi hapo mwanzo nilijiunga na Vodacom,lakini tatizo kubwa nililopata ni kuwa mimi siwezi kutumia email ya yahoo kwa hiyo nitafute zingine kama gmail au hotmail ili hali mi natumia yahoo,nikaulize kulikoni nikaambiwa nikitaka kutumia anuani ya yahoo inabidi nilipia dola 40.
Pia ingawaje niliambiwa kuwa ni Unlimited ukweli ni kuwa sio,huduma ya BIS ikaishia kabla ya hata mwezi kwani kutokana na kazi zangu ilibidi niwe natuma na kupokea mafaili mengi na makubwa.
Nikaone ngoja nijaribu Zain, loh Zain ni chiboko kwani nimeweza kutumia anuani ya yahoo bila pingamizi lolote na pia kuna vionjo kibao,pia GPS kama kawa na iko sahihi inakuonyesha mahali sahihi ulipo n.k pia ni unlimited na kwa sasa kuna offer ya bure kwa waliojiunga kutumia mwezi mmoja bureee.
Kwangu mimi naona Zain ni zaidi ya vodacom inapokuja huduma ya kutumia BB.kama kuna nyongenza karibuni waitu
 
Huo ni mtazamo wako....mimi nina BB mwaka nusu sasa na Vodacom....
Inafanya vizuri unajua BIS services and access zinatoka RIM sio zain wala vodacom hao carrier tu..

Tatizo la yahoo lilikuwa tokea RIM na yahoo...wamekubaliana sasa wameweka free....now unaweza ukaweka emails za yahoo kwa BB

GPS google wameweka GPS kali zaidi inakuonyesha chochote unachotaka....sio zain zantel au vodacom ni zote tu...

Simply download google map ....done.

Issue iwe kwenye support ya hizo BB kwa wateja....hapo ndio kama una muda na unapenda fanya ulinganisho
Kwa vigezo utakavyo!!!
 
Nashukuru Skill na je Vodacom wanaposema matumizi ni Unlimited ilihali sio hilo je limekaa vipi
 
Mkuu hapo sijajua vizuri labda uwapigie na kuwauliza....wenyewe vodacom....ila nasikia ni fast kiasi chake na haizidi 64k...mimi nina line ya zantel na vodacom zote ziko sawa sawa kwa speed
 
Niko Zain. Japo sijajiunga kwenye huduma zao za kulipia, kila nikituma SMS wanakata Tsh 390. Yupo mwingine aliyeona hili au kufahamu kwanini SMS iwe 390?
 
@mfianchi
nakubaliana na ww juu ya zain na voda wanatangaza kibiashara ukija kivitendo nitofauti kabisa kamchezo ako walikuwa nacho zantel pia
 
Juzi juzi niliandika makala ya Kiingereza ikisema "Vodacom market Leadership claim is a misnomer". Nilitaja vitu vingi ambavyo Vodacom wanasema wanaongoza kumbe sivyo ndivyo. Utawala wa Vodacom ukampigia Mhariri wa gazeti lililochapa makala hiyo na kulalama sana wakasema mimi nimehongwa na wapinzani wa Vodacom kuwachafua! Mhariri akawapa Vodacom nafasi ya kujibu mapigo sasa ni wiki ya tatu sijaona kitu. I think Vodacom's succcess has gone too much into their head wameanza kuchukulia wateja for granted.
 
Zain wako matawi ya juu bana kwenye huduma ya BB,mimi kwanza nilikuwa vodacom baada ya kuona longolongo na unlimited yao nikahamia Zain ,kwanza nimepata offa ya mwezi mmoja buure na pia najishushia vitu kiulaini bila mwisho mpaka mwenyewe naamua basi ,
 
Back
Top Bottom