BirthDay

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
UKUMBUSHO WA SIKU YA KUZALIWA.
Nawashukuru wanajamii wa JAMII FORUMS kwa kunikumbuka (kunikumbusha!!!!!) kwa/na kunipongeza ktk siku yangu ya kuzaliwa tarehe 30/08. Ila nasikitika tu kwamba tangu nizaliwe miaka kadhaa nyuma sijawahi kusherekea siku hiyo. Kabla ya kusoma kitabu fulani kuhusu siku hiyo, sikuwa na sababu kwanini sipendi kusherekea wala kuhudhuria sherehe hizo. Jamani hebu someni maelezo haya (Nukuu zote ni kutoka Biblia ya Union Version):


Fasili: Siku ya kuzaliwa kwa mtu au sikukuu ya siku hiyo. Mahali fulani fulani sikukuu ya kuzaliwa kwa mtu, hasa ile ya mtoto, huadhimishwa kwa kufanya karamu na kutolewa kwa zawadi nyingi.

Je! Marejeo ya Biblia kwenye maadhimisho ya siku hiyo huyaweka ktk njia ya kuyakubali? Biblia inataja tu mawili ya maadhimisho hayo.

Mwa. 40:20-22. Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao……
Mt. 14:6-10 Wakati ukumbusho wa siku ya kuzaliwa kwake Herode…
NB: 1: Sherehe zote hizi ziliishia kwa MAUAJI.
2: Kila jambo lililomo ktk Biblia limo humo kwa sababu maalum/fulani hivyo basi kwa ufupi Biblia inakataza sikukuu hizo.


Wakristu wa mwanzo Je! Waliyaonaje maadhimisho hayo

Wakristu hao yaliyaona maadhimisho hayo kuwa ni sehemu ya ibada ya SANAMU, maoni ambayo yalidhibitishwa kwa wingi na yale waliyoyaona juu ya maadhimisho yenye kupendwa na watu wengi yaliyohusiana na siku hizo.


Ni nini iliyo asili ya desturi zenye kupendwa na wengi zinazohusiana na maadhimisho ya ukumbusho wa siku za kuzaliwa?

Desturi mbalimbali ambazo kwazo watu LEO wanaadhimisha siku zao za kuzaliwa zina historia ndefu. Roho Asili zake ni kt makao ya MIZUNGU NA DINI. Desturi za kutoa pongezi, zawadi na kuadhimisha-zikiwa kamili pamoja na mishumaa iliyowashwa-ktk nyakati za kale zilikusudiwa kumkinga mwenye sikukuu asiumizwe na mashetani na kuhakikisha usalama wake kwa ajili ya mwaka ujao….. Mpaka kwenye karne ya nne, Ukristo desturi tajwa kwani ilikuwa ni ya kipagani.

Wagiriki waliitikadi kwamba kila mmoja alikuwa na roho (daemon) yenye kutoa himaya iliyohudhuria kuzaliwa kwake na ikamlinda maishani. Roho hiyo ilikuwa na uhusiano wa KIFUMBO pamoja na mungu ambaye ktk ukumbusho wa siku ya kuzalliwa kwake mtu huyo alizaliwa. Warumi pia waliunga mkono wazo hilo Dhana hiyo iliendelezwa ktk itikadi ya kibinadamu na inaoneshwa ktk malaika mlinzi, mama mdhimini wa kizimwi na mtakatifu msaidizi.

Desturi ya mishumaa iliyowashwa juu ya keki ilianzishwa na Wagiriki. Keki za asali zenye umbo kama mwezi na yenye kuwashwa mishumaa midogo iliwekwa juu ya madhabahu ya hekalu la mungu (Artemi). Mishumaa ya kukumbuka siku ya kuzaliwa, ktk itikadi ya watu wa mashambani, ina uwezo wa kipekee wa ajabu kwa ajili ya kutoa mema yanayotakwa. Mishumaa iliyowashwa na mioto yenye dhabihu imekuwa na maana ya kipekee ya kifumbo tangu Binadamu aliposimamisha kwa mara ya kwanza madhahabu ya miungu wake. Kwa njia hiyo, mishumaa hiyo ni heshima na sifa kwa mtoto na huleta ufanisi mwema……Salamu za ukumbusho wa siku ya kuzaliwa na kutakiana mema kwa ajili ya furaha ni sehemu ya asili ya sikukuu hiyo……Hapo awali wazo hilo lilikuwa na shina lake ktk mizungu. Salamu za ukumbusho wa siku za kuzaliwa, zina nguvu kwa ajili ya mema au mabaya kwa sababu mmoja huwa karibu zaidi na ulimwengu wa roho ktk siku hiyo.

Sherehe zinazofaa kwa jamaa na marafiki ktk nyakati nyingine kwa ajili ya kula, kunywa, na kufurahi hazikatazwi.

Mhu. 3:12-13. Kula, kunywa na kufurahi ni zawadi ya Mungu.
1 Kor. 10:31. Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.


MASWALI.
1; Je! Hizi sio sababu tosha kuunga mkono mkono msimamo wangu toka awali wa kutojihusisha na MAADHIMISHO hayo
2; Je! Kabla ya kuja kwa wazungu, sisi Wadanganyika weusi wenye asili ya nchi hii tulikuwa na utamaduni, mila au desturi ya kusherekea sikukuu hiyo



Source: Watch Tower Bible & Track Society of Pennsylvania (1989). Kutoa Sababu kwa
Kutumia Maandiko. Watchtower Bible & Track Society of New York, Inc., and International Bible Students Association, Brooklyn- New York, USA. 445pp.
 
Back
Top Bottom