Birthday ya CCM Mwanza, Malori yaanza kumiminika

Kesho na kesho kutwa vichwa vya habari vitasomeka 'SHEREHE ZA KUZALIWA CCM ZAFANA NA KUHUDHURIWA NA MAELFU YA WATU' Kumbe watu wenyewe wamesombwa toka nje ya jiji la MZA!
 
Mkuu Bukwimba ndo wapi?

Mkuu iko Mashenzini huku Mwanza, Kuna hata kituo cha reli ya Kati.

Bukwimba

location: Kwimba, Mwanza, Tanzania
coordinates: 2° 48' 0" South, 33° 25' 0" East


Inapakana na miji midogo ya Bungulwa, Izugawima na Nyandekwa

Google map kama unataka kupajua zaidi

Bukwimba Map | Tanzania Google Satellite Maps

rQgicds5QGxh4HPwIao1iY9RR1xmW+FEbKBYedoIQmD5ro1R8tUXHSDn1+P8PNqJfwgdIYAcAAAAASUVORK5CYII=
 
Niko hapa maeneo ya Villa Park Resort jirani kabisa Kirumaba stadium mpaka dakika hii yameishaingia malori sita yakiwa yamejaza watu,tatizo yanapita kwa kasi ajabu nakuingia uwanjani moja kwa moja ila wakazi wengi walio jirani wanapiga miluzi na kuzomea kila lori linalopita huku wakionyesha vidole viwili alama ya cdm,ajabu waliomo kwenye malori hawajibu chochote badala yake wanonekana kushangaa shangaa,niki bahatisha japo picha nitawawekea,japo malori yanakuwa so speedy.

Waache tu waendelee kudanganyika kubebwa kama mizigo pasipo kujijua hawajui kama wanavipalilia vizazi vyao hali ngumu
 
Zimeingia zingine 4 na taarifa zinasema wanatolewa maeneo ya Magu,Misungwi,Sumve,Kwimba na vijiji vingine vinavyo zunguka jiji la Mwanza,na wakishaingizwa uwanjani wana valishwa sare za ccm,na duru zinaarifu kuwa kuna mafundi vyerehani zaidi ya 40 wamo uwanjani toka juzi wamekuwa wakishona sare za ccm usiku na mchana chini ya ulinzi mkali wa Polisi na greenguard.

Kwahiyo kulala ni humo humo uwanjani?
 
Leo wamepita hapa Saint Augustine University gari lao la matangazo kidogo litekwe! Wamekimbia wameacha T-shirt tumechoma moto! Natuma picha sahivi.
 
Suala la malazi na wataoga wapi ndiyo gumzo hapa mitaani maana wako wengi mno,sidhani kama ccm wanaweza ingia gharama za kuwalaza guest coz wanaonekana kuwa pirimitivu sana na hawajielewi.

Waacheni tu yawakute yatakayowakuta maana hayo ndiyo malipo ya ujinga wao
 
hii ni dalili tosha zinazoonyesha sasa ccm kushney.wanajua hapa mjini hawawezi jaza uwanja wa kirumba, suluhisho wameona wakachukuevwatu wa pembezoni mwa mji ili wasiaibike.
 
Kuna kijana mmoja wa pikipiki amepita hapa National Nyakato na bendera ya CCM, kapigiwa milusi sana. Anaonekana anafanya kitu cha ajabu.
 
Habari za uhakika kabisa kutoka kwa kada mbalimbali ndani ya CCM Mwanza zinasema sherehe hizi zilipangwa kufanyika Mza kwa sababu kuu zifuatazo:KWANZA taarifa za ndani kabisa zinadai wenyeviti wale wa mashina walitakiwa kujieleza ni kwanini chama kilipoteza majimbo,kulikuwa na taarifa kuwa nao WAVUE MAGAMBA,baadae waliona chama kitakufa kabisa,hali hii iliongeza mpasuko,sasa kwa "Chakula hiki cha CCM Kirumba"tuwe pamoja na Wanachama.PILI:Kuzindua harakati za kupata kiti cha udiwani cha kata ya Kirumba ambacho diwani wake(CHADEMA) alifariki dunia.Ni moja kati ya kata muhimu sana kwa CCM.TATU:Makovu makubwa yanayotokana na uchaguzi uliopita,wanachama,viongozi na wangineo......UTANI KIDUCHU,Ni kwamba Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA wanasema CCM imekuja kujifanyia"HITMA" na kwamba wamekuja kuwapumbaza watu kwa nyama,kuwafanya "Mazuzu"
Source:MWANACCM Aliyeasi-Kirumba
 
hivi kweli ccm imefikia hatua wanaona diwani ni muhimu kiasi hicho? wakuu fikirieni inakuwaje fisi anapokatiza kijijini mchana kweupeeeeee? hushangiliwa au hozomewa? ndiyo ya ccm(fisi) hayo!!!!!!!
r.i.p kolimba, ni heri wangechukuwa maneno yako.
 
Nipo maeneo ya hapa Mkolani - millennium bar limepita Lori na vijana kibao! Wanapelekwa Kirumba kuvalishwa mavazi ya Kijani na njano. Wamezomewa na vijana kwa alama ya CDM Nina picha nitaiweka!

Usisahau kuhama lokesheni mkuu kila unaporipoti,jf members tunawindwa sana na usalama wa taifa japo hawatuwezi,wamatumia magari yaliyoandikwa(Mukesh Traves Ltd) kwa sherehe hii,haaaahahaaaaaaa!Mie ni dereva wa Mukeshi
 
Back
Top Bottom