Birthday Parties To Our Lovely Kids: Ni muhimu au hazina maana?

Teamo

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
12,272
1,034
Hivi wakubwa,
Kuna umuhimu wa kuwafanyia kajisherehe japo kadogo ka kuikumbuka siku yao ya kuzaliwa watoto wetu bila kuangalia kwamba hawalitambui hilo?
 
... Mimi naona inafaa tu, tena kwa watoto ndiyo muhimu kwa saaana.
... Tusipowafanyia hivi watoto, ni sherehe gani nyingine zinazowahusu wao tuwajumuishe?!- Kumbukumbu ya siku ya kupata uhuru, mapinduzi ya Zanzibar, au mafisadi kufikishwa mahakamani na kuachiwa huru?!!!
... Birthdays are a perfect celebration moments, particularly for kids to connect with their peers as they grow and appreciate the magnificence of life, its value and adventures.
 
kuna 'mjomba-angu' ananiambia ni kuonyesha ufahari!..............
 
Inategemea unaifanyaje hiyo sherehe! Kwa mtizamo wangu, kama party inaweza kufanyiwa nyumbani na waalikwa mainly watoto inapendeza sana. Lakini inapokuja unakodi ukumbi mkubwa na mbwembwe za magari kama harusi, nadhani hapo ndo watu wanaanza kuona kama unataka kuonesha ufahari.
 
Lakini inapokuja unakodi ukumbi mkubwa na mbwembwe za magari kama harusi, nadhani hapo ndo watu wanaanza kuona kama unataka kuonesha ufahari.

...mtoto anatimiza mwaka unadondosha bonge la party umekodi ukumbi magari kibao wageni kibao hii birthday ina muhimu kweli?au ndo kutaka kujionyesha kuwa wewe unazo.
Je ndugu zetu wanao ishi uswazi wanakumbuka kufanya hata hivyo visherehe vidogo vya kuzaliwa?
 
...mtoto anatimiza mwaka unadondosha bonge la party umekodi ukumbi magari kibao wageni kibao hii birthday ina muhimu kweli?

HILI SWALA HALIJAWAHI KUTOKEA BANA!it is not something practical
 
Birthday ya mtoto, ni kuashiria furaha uliyonayo mzazi kuona mwanao anakua kwa stage by stage na hivyo huna budi kuisherehekea..Jinsi ya kusheherekea ndo inaweza kuwa tofauti kati ya familia na familia lakini binafsi naamini ikiwepo keki,bites,picha(kamera), vinywaji na rafiki zake basi sherehe imefana.
Kwangu mimi inaweza kuwa muhimu kwa mwingine siyo muhimu na vice versa ila kwa anayefanya ni vizuri na kuweka kumbukumbu ya mtoto kuanzia anazaliwa na kuendelea.
 
Sijui kama "party" ni muhimu, lakini kusema kuwa watoto wadogo hawajitambui sio sawa kabisa. Tena malazi anayopata mtoto kwenye umri mdogo yanachangia sana atakavyokuwa ukubwani, hata kama hawawezi kuyakumbuka.
 
Kwangu mimi naona birthday haina umuhimu wowote ule.
Na sioni mantiki ya kufanya birthday nikiwa kama mzazi sioni umuhimu wake maana sherehe ya kufurahi na mtoto wangu nae anajisikia ni x-mass, new year, pasaka na Idd
 
Mimi ni bora nisherehekee birthday na new year kuliko hizo nyingine. Naona hazihusiani na chochote kwangu mimi kama mwafrika ambaye bado naabudu imani/dini za mababu zangu wa kiafrika za miaka 300 iliyopita!
 
WEWE KAMA MZAZI!lakini umesahau kwamba hii ni b'dei ya mtoto,SIO YAKO!mi nadhani yako ndo haina umuhimu,ila ya mtoto ina umuhimu!waliodesign hii kumbukumbu walia ngalea all 'the unforeseen parameters' wakaona iwepo!

SWALI:Mkuu utajisikiaje mtoto akifika miaka saba anaomba picha zake za bethidei wakati bado kichanga,kwasababu tu watoto wenzie wanazo?Utajisikiaje?
 
Mimi ni bora nisherehekee birthday na new year kuliko hizo nyingine. Naona hazihusiani na chochote kwangu mimi kama mwafrika ambaye bado naabudu imani/dini za mababu zangu wa kiafrika za miaka 300 iliyopita!

Mkuu kama unadumisha tamaduni za mababu zako sikumbuki kama kweli walikuwa wanasherekea birthday au kama walikuwa wanaazimisha kumbukumbu ya kuzaliwa hizi kwa vile umekuwa katika mazingira ya kizungu zungu ndo umeyaona na umeyaiga.
 
...swadakta!!
...na hilo ndilo nililolenga!
...xmas na pasaka tulijitengenezea sisi wabantu?!
 
Mkuu kama unadumisha tamaduni za mababu zako sikumbuki kama kweli walikuwa wanasherekea birthday au kama walikuwa wanaazimisha kumbukumbu ya kuzaliwa hizi kwa vile umekuwa katika mazingira ya kizungu zungu ndo umeyaona na umeyaiga.

We hua unazidumisha!?
Umewahi kwenda kutambikia mizimu walau mara moja kwa mwaka?
Umewahi Kwenda sherehekea sherehe za kuikaribisha mvua?
Unadumisha kwa kusapoti TOHARA KWA WANAWAKE?
 
Mkuu kama unadumisha tamaduni za mababu zako sikumbuki kama kweli walikuwa wanasherekea birthday au kama walikuwa wanaazimisha kumbukumbu ya kuzaliwa hizi kwa vile umekuwa katika mazingira ya kizungu zungu ndo umeyaona na umeyaiga.

Nadhani kasema dini za mababu, sio utamaduni wote.
 
We hua unazidumisha!?
Umewahi kwenda kutambikia mizimu walau mara moja kwa mwaka?

Hii mkuu sana tu mwezi July naenda huko tena ni bonge la sherehe.
Iwa tunaenda tunakusanyika ukoo mzima mbuzi, ng'ombe, kondoo, kuku iwa wanapoteza shingo yaani ni bonge la party na kusafisha makaburi ya mababu zetu. Hii iwa naipenda sana kule kijijini maana inakuwa bonge la sherehe
 
So?
Nisherehe gani hapa inaonyesha UFAHARI?hiyo ya mizimu mnayochinja wanyama kadhaa

..........au hii ya kuonyesha namna gani unampenda na kumjali mwanao kwa kwenda ibada hata ya masifu ya asubuhi,kuandaa cake nzuri,na camera kwa ajili ya kumbukumbu na labda dinner nyumbani kwako usiku tena baada ya kazi zoote?

WAPI PANA KUONYESHANA UFAHARI?
 
Back
Top Bottom