Birthday For Lowassa: JK ndani ya nyumba

Maane, Kumbuka usemi wa "usikatae wito.........." Paroko ni mtumishi wa Mungu hivyo ni ktk kufuata matendo ya bwana wetu Yesu kristu aliyewaambia mafarisayo kuwa" Sikuja kuwaita watu wema bali wenye dhambi ili wapate kutubu".
Pili watu walioalikwa na EL ni marafiki zake hata kabla hajapata matatizo ya kashfa je wataanzaje kumsusa leo awapo kwenye matatizo na pengine anawahitaji isivyo kawaida. Pia kumbuka "rafiki ni yule akujua hata uwapo ktk matatizo".
Is it really possible duniani humu mtu uwe na marafiki 'wa kweli' zaidi ya wawili watatu? kama ni acquitances sawa lakini 'friends' mh!
 
Bila shaka mheshimiwa Lowasa anataka kupata att ya vyombo vya habari pengine kupima upepo wa urais mwaka 2015.Lowasa aliporudi kutoka Israel na kijarida kidogo cha kurasa chache aliwaalika viongozi wakubwa wa dini kuja kuzindua kijitabu chake.

Mheshimiwa Lowasa bado hajakata tamaa ya kuwa rais wa Tanzania mwaka 2015,inavyoelekea ana mtandao mkubwa nyuma yake unaofanya kila linalowezekana na hata yasiyowekana ngoyai atimize azima yake.Hakuna mjadala tena kwamba CC na NEC imeshatekwa na mtandao wa Lowasa yamkini hata muungwana hana ujanja wa kumdhibiti Ngoyai.Pengine muungwana anatishika na namna Lowasa anavyochanga karata zake anajua fika yaliyomtokea aliyekuwa rais wa Afrika kusini Bwana T mbeki yanaweza kumkuta ata yeye.
 
Nimrod Mukono ndiye anafaa kuwa the next President. Kwa sababu ameonyesha ujasiri mkubwa sana katika mapambano dhidi ya Makampuni ya kuchimba dhahabu Mara. It si free country. Kila mtu anaruhusiwa kutoa maoni,na hayo ndiyo maoni yangu. Lakini kama watu opaque wakichaguliwa kuwa Rais,we will end with a Government of kleptomaniacs,like we have now.

Mzee kampeni nini? ila misamiati mzee mpaka tukimbilie dictionary sisi tulio kimbia umande lkn poa
 
Kama binadamu yeyote amejiwekea kautamadni ka kufanya besidei ni vizuri kabisa. Ni kwa visingizio hivyo mtu kama Lowasa, Fisadi wa mafisadi anaweza kuandaa sherehe kubwa sana ili kuendelea kujisafisha kwa maandalizi ya 2015. Ni aibu gani kwa viongozi wa dini kuendelea kumuunga mkono huyu bepari na fisadi!!!?? Ukweli ndiyo huu!!!
Viongozi wengi wa dini na makanisa hasa yale ambayo yanajiita ya kiroho wamejawa na tamaa sana. Wamekuwa wakiwakumbatia waumini wale ambao wanatoa sadaka na mafungu ya kumi bila kujali yametokana na nini!!! Wamekuwa wakifanya harambee na kuwaalika hawa wenye pesa hata kama ni mafisadi au majambazi huwa hawajali. Ni wazee wangapi wa kanisa ambao wamekuja kugundulika kuwa ni majambazi na pengine ni wafanya biashara wakubwa wa madawa ya kulenvya?? Wana EPA wangapi akiwemo Njake, Lukaza, Makubo (alisevu), na wengine wengi ambao wanavaa ngozi ya kondoo na kuwa mstari wa mbele kuchangia kaika makanisa na wanakalishwa pale mbele ya makanisa kwa kuwa pia wana uwezo wa kuvaa vizuri ili watu wavutiwe na kuona kuwa pengine kundi au kanisa hili linatoa watu shida maana wote wako sparkling!! Kumbe ni usanii wa viongozi wa dini/wachungaji???

Ngoja leo EDO afilisike uone kama kuna kiongozi wa dini atakuwa karibu yake!! Kwanza watajificha ili wasije wakakutana naye asije akawadai sadka yake na mafungu ya kumi. Enyi viongozi wa dini wa kileo, acheni unafiki.

Huko nyuma, mtu akigundulika kuwa hata alikuwa mlanguzi, jambazi, mwenye hawara, asiye na ndoa rasmi, etc alikuwa haruhusiwi kupata huduma za kanisa. Leo hii haya yamewekwa pembeni, wanapata huduma kama kawaida mpaka vikundi vya kwaya vyenye njaa ambavyo vikizindua albam utasikia mgeni rasmi Lowasa, mgeni rasmi hovyo kabisa, kisa wanataka waandiwe cheque!!

Na huyo Paroko wa kanisa katoliki alienda kufanya nini huko?? Wakatoliki hamko maskini kiasi hicho. Mhashamu Pengo na Kilaini mmulikeni huyu traitor!! Au askof mkuu Josephat Lebulu uko upande upi wa mafisadi??

Mkuu naunga mkono hoja, hasa hapo penye maandishi mekundu..
 
Nakupongeza EL kwa kusherehekea ukiwa home..... kama si JK ungesherehekea Sgerea kama Liyumba
 
Back
Top Bottom