Birthday For Lowassa: JK ndani ya nyumba

tetesi nilizozipata A-Town, hiyo licha ilikuwa birthday lakini pia ilikuwa mahsusi kwa mafisadi kujipongeza kwa mambo yaliyojili pade Dodoma kwenye vikao vya chama kwa kuweza kumbana spika Sitta
Tehe tehe teheee!
 
Mungu yupo nasi maana kwa siasa zinavyokwenda nimekata tamaa na wana siasa tulionao. Wanaishi kwa double standard
 
Ni kweli kwamba Mkuu wa Nchi alikuwa Mkoani Arusha Jana,alikwenda Wilayani Longido kuangalia hali ya Ukame,na baadaye Jioni alirudi mjini Arusha,ambako aliwaandalia waumini wa Kiislamu Futari,Hakuna habari ya kwamba alikwenda Monduli kwenye Sherehe ya kuzaliwa Mbunge Lowassa,Baadhi ya viongozi walioambatana na Rais walikwenda kwenye sherehe hiyo,Lakini Rais alibaki Ikulu ndogo Arusha.
 
Happy birthday EL our next presidaa...2015

Happy Birthday my A..............S
Kama kweli JK alikuwepo huko tuambiwe wazi ni fungu lipi limetumika kuhudumia safari yake, au kama EL ameweka down payment hapo. Halafu hapo ndipo utadai maamuzi ya Bunge yafuatwe???? Please....
 
msijali, Mungu alikuwa na wananchi wa longido ambao wanakufa njaa kilomita chache toka mahali lowasa alipokuwa naponda raha kwa mvinyo na nafaka na kutupia mbwa makombo! Mungu amemwona lowasa akiiba toka kapu la maskini hawa ndo maana amempa maisha marefu ili ashuhudie mwenyewe anguko lake na mafisadi wenzake! BWANA WA MAJESHI ATAWAIBISHA NA KUSHAMBARATISHA UMOJA WENU
 
Nimrod Mukono ndiye anafaa kuwa the next President. Kwa sababu ameonyesha ujasiri mkubwa sana katika mapambano dhidi ya Makampuni ya kuchimba dhahabu Mara. It si free country. Kila mtu anaruhusiwa kutoa maoni,na hayo ndiyo maoni yangu. Lakini kama watu opaque wakichaguliwa kuwa Rais,we will end with a Government of kleptomaniacs,like we have now.
 
Hapa basi kwishne picha tumeliona na star tumenjua!!

Mkuu hii avator yako ni disgusting. Unaionaje wewe? . Samahani lakini , ni maoni yangu binafsi.Ukipenda tusaidie ili tuweze kusoma thread zako kwa hamu zaidi.
 
Ni kweli kwamba Mkuu wa Nchi alikuwa Mkoani Arusha Jana,alikwenda Wilayani Longido kuangalia hali ya Ukame,na baadaye Jioni alirudi mjini Arusha,ambako aliwaandalia waumini wa Kiislamu Futari,Hakuna habari ya kwamba alikwenda Monduli kwenye Sherehe ya kuzaliwa Mbunge Lowassa,Baadhi ya viongozi walioambatana na Rais walikwenda kwenye sherehe hiyo,Lakini Rais alibaki Ikulu ndogo Arusha.

Sawa kabisa Mkuu, bahati mbaya nilikuwa safarini sikuweza kupata mtandao huku kijijini, ndio kwanza niko makao makuu ya wilaya nimeomba net mahala. Habari ni kwamba Mkuu hajakanyaga katika hiyo sherehe pamoja na kualikwa sana na habari za kwenda kwake zikaenezwa sana na kila mtu alijua atakwenda. Mtu mmoja alisema kwamba hata ziara yake Arusha imetengenezwa mahsusi ili aweze kwenda lakini wajanja wake wakaandaa ratiba ya futari. Kilichotokea ni kwamba EL hakutokea katika ziara ya mkuu pamoja na wafuasi wake kuwapo katika ziara na wengine katika futari na badaye kuchomoka na kwenda Monduli. JK hakuwapo kabisa katika sherehe ya mchana na hata ya usiku.

Mtoa habari aliyekuwapo sherehe zote amesema, hajamuona kabisa na kwamba anashangaa wanaotangaza hivyo walikuwa na nia ya kuwakatisha tamaa watu fulani fulani. Haya tutaona na kusikia mengi mwaka huu.
 
Kama binadamu yeyote amejiwekea kautamadni ka kufanya besidei ni vizuri kabisa. Ni kwa visingizio hivyo mtu kama Lowasa, Fisadi wa mafisadi anaweza kuandaa sherehe kubwa sana ili kuendelea kujisafisha kwa maandalizi ya 2015. Ni aibu gani kwa viongozi wa dini kuendelea kumuunga mkono huyu bepari na fisadi!!!?? Ukweli ndiyo huu!!!
Viongozi wengi wa dini na makanisa hasa yale ambayo yanajiita ya kiroho wamejawa na tamaa sana. Wamekuwa wakiwakumbatia waumini wale ambao wanatoa sadaka na mafungu ya kumi bila kujali yametokana na nini!!! Wamekuwa wakifanya harambee na kuwaalika hawa wenye pesa hata kama ni mafisadi au majambazi huwa hawajali. Ni wazee wangapi wa kanisa ambao wamekuja kugundulika kuwa ni majambazi na pengine ni wafanya biashara wakubwa wa madawa ya kulenvya?? Wana EPA wangapi akiwemo Njake, Lukaza, Makubo (alisevu), na wengine wengi ambao wanavaa ngozi ya kondoo na kuwa mstari wa mbele kuchangia kaika makanisa na wanakalishwa pale mbele ya makanisa kwa kuwa pia wana uwezo wa kuvaa vizuri ili watu wavutiwe na kuona kuwa pengine kundi au kanisa hili linatoa watu shida maana wote wako sparkling!! Kumbe ni usanii wa viongozi wa dini/wachungaji???

Ngoja leo EDO afilisike uone kama kuna kiongozi wa dini atakuwa karibu yake!! Kwanza watajificha ili wasije wakakutana naye asije akawadai sadka yake na mafungu ya kumi. Enyi viongozi wa dini wa kileo, acheni unafiki.

Huko nyuma, mtu akigundulika kuwa hata alikuwa mlanguzi, jambazi, mwenye hawara, asiye na ndoa rasmi, etc alikuwa haruhusiwi kupata huduma za kanisa. Leo hii haya yamewekwa pembeni, wanapata huduma kama kawaida mpaka vikundi vya kwaya vyenye njaa ambavyo vikizindua albam utasikia mgeni rasmi Lowasa, mgeni rasmi hovyo kabisa, kisa wanataka waandiwe cheque!!

Na huyo Paroko wa kanisa katoliki alienda kufanya nini huko?? Wakatoliki hamko maskini kiasi hicho. Mhashamu Pengo na Kilaini mmulikeni huyu traitor!! Au askof mkuu Josephat Lebulu uko upande upi wa mafisadi??
 
msijali, mungu alikuwa na wananchi wa longido ambao wanakufa njaa kilomita chache toka mahali lowasa alipokuwa naponda raha kwa mvinyo na nafaka na kutupia mbwa makombo! Mungu amemwona lowasa akiiba toka kapu la maskini hawa ndo maana amempa maisha marefu ili ashuhudie mwenyewe anguko lake na mafisadi wenzake! Bwana wa majeshi atawaibisha na kushambaratisha umoja wenu

amen !
 
Maane, Kumbuka usemi wa "usikatae wito.........." Paroko ni mtumishi wa Mungu hivyo ni ktk kufuata matendo ya bwana wetu Yesu kristu aliyewaambia mafarisayo kuwa" Sikuja kuwaita watu wema bali wenye dhambi ili wapate kutubu".
Pili watu walioalikwa na EL ni marafiki zake hata kabla hajapata matatizo ya kashfa je wataanzaje kumsusa leo awapo kwenye matatizo na pengine anawahitaji isivyo kawaida. Pia kumbuka "rafiki ni yule akujua hata uwapo ktk matatizo".
 
Michuzi hakuipata hii nini maana naamini angetutundikia angalau picha 2 au 3 hivi tukaona hiyo party maana inaweza kuwa ya kifisadi. Kwani katimiza miaka mingapi mapaka afanye party?
 
Thanks Shaycas. Huyo fisadi alikuwa ametimiza miaka mingapi mpaka afanye sherehe kubwa namna hiyo wakati wapiga kura wake wanakufaa njaa?
 
Ni kweli kwamba Mkuu wa Nchi alikuwa Mkoani Arusha Jana,alikwenda Wilayani Longido kuangalia hali ya Ukame,na baadaye Jioni alirudi mjini Arusha,ambako aliwaandalia waumini wa Kiislamu Futari,Hakuna habari ya kwamba alikwenda Monduli kwenye Sherehe ya kuzaliwa Mbunge Lowassa,Baadhi ya viongozi walioambatana na Rais walikwenda kwenye sherehe hiyo,Lakini Rais alibaki Ikulu ndogo Arusha.
Na habari za uhakika Mwakalinga yuko London since last week,natafuta namba yake ya mkononi ya UK niitundike hapa atakayetaka aongee naye.
 
Sawa kabisa Mkuu, bahati mbaya nilikuwa safarini sikuweza kupata mtandao huku kijijini, ndio kwanza niko makao makuu ya wilaya nimeomba net mahala. Habari ni kwamba Mkuu hajakanyaga katika hiyo sherehe pamoja na kualikwa sana na habari za kwenda kwake zikaenezwa sana na kila mtu alijua atakwenda. Mtu mmoja alisema kwamba hata ziara yake Arusha imetengenezwa mahsusi ili aweze kwenda lakini wajanja wake wakaandaa ratiba ya futari. Kilichotokea ni kwamba EL hakutokea katika ziara ya mkuu pamoja na wafuasi wake kuwapo katika ziara na wengine katika futari na badaye kuchomoka na kwenda Monduli. JK hakuwapo kabisa katika sherehe ya mchana na hata ya usiku.

Mtoa habari aliyekuwapo sherehe zote amesema, hajamuona kabisa na kwamba anashangaa wanaotangaza hivyo walikuwa na nia ya kuwakatisha tamaa watu fulani fulani. Haya tutaona na kusikia mengi mwaka huu.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,aliyekuwepo kwenye mnuso atajwe alikuwepo ambaye hakuwepo basi hakuwepo na asisingiziwe otherwise,vinginevyo tutapoteza nia njema na malengo mazuri ya jamvi tukufu la JF.
 
Back
Top Bottom