Birth day yangu ni 09.12.2011 natimiza miaka 50

Mpui Lyazumbi

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
1,856
371
Wakuu heshima mbele. Nimeanza mwezi wa kumi na mbili kwa faraja kuu. Kwamba ifikapo tarehe 09 natimiza umri wa miaka 50-sambamba na uhuru wa Tanganyika. Kwa kweli ni safari ndefu sana, na naomba nilete kwenu siku yangu muhimu kabisa. Na kwa kawaida yake, wanabodi mtazungumza mengi hasa yenye kunijenga mkizingatia kuwa miaka 50 si haba. Kuna wengi hawakuisogelea kiasi changu na kuna waliozidi hapa. Nasema binafsi nimekuwa na mafanikio kiasi katika MAISHA na mchango wangu umekuwa wa kuridhisha katika ujenzi wa TAIFA. Hata hivyo kasi ya kujiletea maendeleo kama taifa bado ni ndogo sana. Tufanye nini kwa ajili ya mafanikio ya kizazi kijacho?

NAWASILISHA.
 
You must be H.E. Freeman Aikaeli Mbowe(M.P)
 
hongera mdau....mwezi wa sita tulimpoteza rafiki na ndugu yetu, naye alikuwa anafikisha miaka 50 tarehe 09/12.
R.I.P BROTHER.
 
Hongera sana tuombe mungu ufike hiyo tarhe Bday itafanyikia wapi ndugu nije kukupongeza ?
 
Mbona kimawazo na fikra unaonekana ni kijana wa.......yrs au siasa na life la magamba ndiyo limekuhalibu hivyo (kifikra).
 
Hongerea zako kwa kutimiza miaka hamsini ukiwa hai, haka kajamaa ketu kalikufa tu miaka miwili baada ya kuzaliwa, baada ya mazishi tukapewa mtoto mwingine wa kuadapti, wakadai oo walikuwa wamepishana miaka miwili kuzaliwa, wakasema tutumie mwaka ulele wa marehemu kuzaliwa katika kusheherekea sherehe za huyu mtoto mwingine, tukasema sawa ( kwashingo upande lakini) .

Jamani karibuni kwenye sherehe za mtoto wangu ( adapted son)

kuna waganga wa jadi wamesema wanaweza kunisaidia kumfufua yule mtoto wangu, bado sijatoa maamuzi

i miss you Tanganyika (RIP)
 
mpe hi birthday mate wako tanganyika ukifanikiwa kufikia huko..
see you later..
 
nishamsamehe, si unajua leo weekend?
Sasa huyu bwana nae huwa anaenda kutembea kwenye maadhimisho? Maana kuna kipengee maalum cha watu waliozaliwa 9 Desemba 1961 kupita mbele ya halaiki...
 
Back
Top Bottom