Biriani ya Kuku wa Kuchoma wa Tanduri

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma Wa Tanduri

Vipimo


Mchele.................. 4 vikombe

Kuku.................. 1

Vitunguu.................. 3

Nyanya/tungule.................. 4

Zabibu kavu.................. ½ kikombe

Tangawizi mbichi na kitunguu thomu iliyosagwa.................. 2 vijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa.................. 1 kijiko cha supu

Mtindi (yoghurt).................. 2 kijiko cha supu

Masala ya tanduri.................. 2 vijiko vya supu

Pilipili manga.................. 1 kijiko cha chai

Hiliki.................. ½ kijiko cha chai

Mdalasini.................. kijiti kimoja

Ndimu.................. 3 vijiko vya supu

Chumvi.................. kiasi

Zaafarani (saffron).................. 1 kijiko cha chai

Mafuta.................. ½ kikombe


Namna Ya Kutayarisha Kuku

Baada ya kumsafisha kuku, mkate vipande vikubwa vikubwa kiasi upendavyo, muoshe mchuje atoke maji.
Katika bakuli, tia tangawizi, kitunguu thomu ilosagawa, pilipili mbichi ilosagwa, chumvi, ndimu, mtindi, masala ya tanduri na uchanganye vizuri, kisha mtie kuku na uchanganye tena na acha arowanike kwa muda wa kiasi saa au zaidi.

Panga kuku katika sinia ya kuchoma ndani ya oveni. Kisha mchome (grill) hadi awive, mtoe acha kando. Mwagia juu yake masala yatakayobakia katika sinia baada ya kumchoma.


Namna Ya Kutayarisha Masala Ya Nyanya

Weka mafuta katika karai, tia vitunguu ulivyokatakata, kaanga hadi vianze kugeuka rangi.
Tia nyanya ulizokatakata, tia pilipili manga, hiliki, mdalasini, chumvi, na zabibu. Kaanga kidogo tu yakiwa tayari epua.


Namna Ya Kutayarisha Wali


Osha na roweka mchele wa basmati.
Roweka zaafarani kwa maji ya moto kiasi robo kikombe weka kando.
Chemsha maji, tia chumvi, kisha tia mchele uive nusu kiini.
Mwaga maji uchuje mchele kisha rudisha katika sufuria au sinia ya foil. Nyunyizia zaafarini, na rudisha katika moto upike hadi uive kamili.

Epua, kisha pakua wali katika sahani au chombo upendacho, mwagia juu yake masala ya nyanya. Kisha weka vipande vya kuku ulivyochoma.
Tayari kwa kuliwa.
 
somo la mapishi ni zuri sana kwa wote na linatufaa wote ila naomba chef uwe unaandika na majina ya viambata yalozoeleka kwasababu sometymz inaleta shida unatamani kupika ukifuata maelekezo lakini hujui maneno mengine yanamaanisha nini.asante
 
umeshawahi kupika hiyo biriani ikatokea?
mwenzio sifuri kabisaaaaaaaa
labda nije unifundishe mwenzangu kama ulifanikiwa

yan wewe FP ndo kama mmm nakiri kabisa katika vyakula vyote biriani ndo linalonishinda kabisaaa yaan sifuri, nikiwa naelekezwa nikisikia hizo process nakata tamaa,. nataman atakeliandaa step by step hata kwa picha ikiwezekana atusaidie
 
yan wewe FP ndo kama mmm nakiri kabisa katika vyakula vyote biriani ndo linalonishinda kabisaaa yaan sifuri, nikiwa naelekezwa nikisikia hizo process nakata tamaa,. nataman atakeliandaa step by step hata kwa picha ikiwezekana atusaidie

Kuna simple birian unaweza pika bila usumbufu.ntalileta hapa kwa picha
 
yan wewe FP ndo kama mmm nakiri kabisa katika vyakula vyote biriani ndo linalonishinda kabisaaa yaan sifuri, nikiwa naelekezwa nikisikia hizo process nakata tamaa,. nataman atakeliandaa step by step hata kwa picha ikiwezekana atusaidie
kumbe siyo peke yangu, nimefurahi nimepata mwenza, lol!
ngoja tusubiri, otherwise tutaishia kununua mtaani tu
 
si mtaani tu best, kula kwa majirani esp kipindi cha sikukuu za eid lol
siku hizi wamama tumerahisishiwa sana maisha.....
sikukuu nauliza tu jamani mnataka tule nini, wakisema biriani tu, simu iko wapi.......
Mpika biriani nakuja saa 6 na nusu kuchukua sahani 10, kwisha kazi, lol!
 
Unanikumbusha chennai nje ya appolo hospitali! Kuna watu walikuwa na kitu hiyo tamu sana ilinipunguzia stress za kuuguliwa na mzee wangu
 
mchele wa biliani ni upi?..je,ni huu huu wa kawaida tunaokula kila siku,au kuna mwingne?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom