binti yangu anakula sabuni na mafuta ya kujipaka

grace saria

New Member
Feb 11, 2012
3
0
Jamani nisaidieni mwanangu wa miaka 7 anakula mafuta ya kujipaka na sabuni je ana tatizo GANI NISAIDIENI
 
Jamani nisaidieni mwanangu wa miaka 7 anakula mafuta ya kujipaka na sabuni je ana tatizo GANI NISAIDIENI

Grace, nimeona watanzania wengi wenye addictions za kula mavitu ya ajabu including magodoro, wakiombea pale SCOAN Nigeria na kupona on the spot; mara nyingi ni mapepo (spirits) zinazowapa hamu (urge) ya kula hiyo mivitu. Usipoteze muda, zikusanye tu umpeleke mwanao. Huko hakuna kubahatisha wala ooh imani yako haba ndio maana kujapona. Kwa taarifa zaidi kama una cable angalia Emmanuel TV, haitapita 2 days bila kuonesha rebroadcast za watu kama mwanao. Ucant imagine kuna mtu alikuwa anakula kinyesi chake mwenyewe, lakini alipona.
 
Kuna ugonjwa unaitwa PICA, basically ni hali ya kula vitu ambavyo kwa kawaida si chakula cha binadamu. Una sababu nyingi ikiwemo stress na nutritional deficiencies. Chunguza vizuri mazingira yanayomzunguka mtoto shuleni, nyumbani etc. Pia mpeleke kwa daktari wa watoto akushauri. Pole dada.
 
Jamani nisaidieni mwanangu wa miaka 7 anakula mafuta ya kujipaka na sabuni je ana tatizo GANI NISAIDIENI
Pole ndg. Naandikahii kwa ajili ya kufikiria juu ya jinsi tabia tabia hiyo inavyoweza kuathiriafya yake iwapoa ataendelea kwa muda mrefu kula sabuni,n.k. Tabia au ugonjwa huu wa kula vituvisivyohitajik mwilini au ambavyo ni kinyume na jamii huitwa PICA . PICA yawezakuwa ugonjwa hatari kutegemeana na nini mtu anakula. Kula vitu dutu (visivyo namanufaa) kwa kiasi kikubwa huwezasababisha matatizo katika afya na hata katika matibabu, hata huweza kuwa sumukatika mwili.. Pia kuna hatari ya kuambukizwa kutokana na dutu fulani, kama vileudongo, na matatizo ya tumbo ikiwa ni pamoja na kuvimbiwa, kukosa choona masualamengineyo mengi.
Kwa bahati nzuri, katika kesi yako sabuni si hatarisana, ingawa kwa kiasi kikubwa baada ya muda inaweza kuharibu afya yako. Sabunikwa ujumla siyo sumu na haipaswi kusababisha sumu. Hata hivyo, inawezakusababisha kuharisha, kutapika au ngozi kuwasha. Mafuta ya kujipaka ni hatari kwani ndani kunakemikali nyingi hasa katika nchi yete ambayo watu wanaweka kemikali nyingi ilikujichubua. Kuwa mwangalifu sana.
Sababu za pica hazijulikani lakini baadhi zinaonyesha kwamba yafuatayo yanawezakuchangia kwa hamu ya kula vitu yasiyo ya chakula:
upungufu wa lishe. Kuna ushahidi kuwa Pica ni njiaambayo huuambia mwili wako kuwa hauna virutubisho vya mwili kama vile, Chuma,kalisi, zinki, na vitamini C & D

Stress,
Baada ya kukuambia hayo ningekushauri huenda kwawataalam wakamchunguze mwanao kiundani!
 
Kama umeokoka muombeehata wewe kwa imani hilo ni pepo na litamtoka na kuacha kula hivyo vitu.mtoto wa dada yangu alikuwa anakula magodoro na karatasi hadi umri wa miaka 18 lakini baada ya kuombewa aliacha
 
acheni ulokole! miaka 18tayari alibarehe, wakati wa kutafuta mchumba hivyo alibadili tabia. hii ni psychological problem
 
Grace, nimeona watanzania wengi wenye addictions za kula mavitu ya ajabu including magodoro, wakiombea pale SCOAN Nigeria na kupona on the spot; mara nyingi ni mapepo (spirits) zinazowapa hamu (urge) ya kula hiyo mivitu. Usipoteze muda, zikusanye tu umpeleke mwanao. Huko hakuna kubahatisha wala ooh imani yako haba ndio maana kujapona. Kwa taarifa zaidi kama una cable angalia Emmanuel TV, haitapita 2 days bila kuonesha rebroadcast za watu kama mwanao. Ucant imagine kuna mtu alikuwa anakula kinyesi chake mwenyewe, lakini alipona.
hakuna haja ya Nigeria. kanisa la Emmanuel ni ndimi za moto linajulikana siku zote. kwa nini umshauri mwenzio aende huko? hapa TZ atatibiwa tu! msiwe sana na imani za kukimbilia nje. kwani Tanzania tumelaaniwa hati hatuwezi tibu watu wetu?
 
No problem atibiwe popote, issue ni kupona sio wapi anapotibiwa. Kuhusu kanisa la emmanuel, kwanza si kanisa, Emmanuel ni TV station, kanisa ni SCOAN, mimi ninachoona kwenye hiyo TV station wagonjwa na watu waliofungwa waqnapona, na wanaombewa katika jina la YESU, na Moto inategemea chanzo chake wapi, lakini kwa pale ni HOLY GHOST FIRE hivyo ndivyo ninavyoona (kwenye telly) na ninasikia (kwenye amplifier ya telly yangu)!
 
ok. nalijua sana hilo dhehebu. cha muhimu aachane na hizo sabuni!
 
hiyo itakuwa PICA kama walivyosema wadau, unajua kwanini wanawake wenye mimba wanakula udongo? watalaam wanasema kutokana kuwa na mtoto mwili unapungukiwa na chuma kwa hiyo automatically ili kukompaseti mtu anaanza kula udongo, pengine mwanao amekosa vyakula vya mafuta, hebu liangalie hilo.
 
Back
Top Bottom