Binti yangu anakojoa kitandani

shizukan

JF-Expert Member
Jan 16, 2011
1,158
563
Tafadhali wanaJF kama kuna mtu ana-experience tatizo kama la kwangu na amelitatuaje. Binti yangu ana miaka 13 sasa na anakojoa kitandani almost everyday. Hili tatizo sasa linamuathiri kisaikolojia kwa kuwa amekuwa mkubwa sasa. As you know hapa kwenye hii nchi iliyouzwa kila kitu ni blah blah hospitalini, nisaidieni manake sasa siwezi kusubiri tena manake waliniambia akikua ataacha, sasa ameshaota na matiti sijui akue nini tena
 
Jaribu kuonana na wataalam wa magonjwa hayo (Urologist) hapo muhimbili wanaweza kumsaidia
 
Dawa ya Mtoto kuacha kukojoa kitandani Upate Kwato la N'gombe . Tia ndani yake hilo kwato kaa la moto, Mtoto Apande juu ya Mti kisha umpe hilo kwato la N'gombe alinuse kisha hukohuko juu ya Mti akojoe kisha ashuke afanye hiyo dawa kwa muda wa siku 7 asubuhi na jioni kila siku atapona inshallah

-Akisha maliza kutumia kisha unipe mimi Feedback Source: PhD Mzizimkavu
 
Jaribu kuonana na wataalam wa magonjwa hayo (Urologist) hapo muhimbili wanaweza kumsaidia

Hao waliniambia akikua ataacha sasa sijui kukua gani manake saa hizi watu wanakaribia kuanza kuja kuombaomba maji (ole wenu, nina manati kubwa kama ya kuulia ng'ombe)
 
Dawa ya Mtoto kuacha kukojoa kitandani Upate Kwato la N'gombe . Tia ndani yake hilo kwato kaa la moto, Mtoto Apande juu ya Mti kisha umpe hilo kwato la N'gombe alinuse kisha hukohuko juu ya Mti akojoe kisha ashuke afanye hiyo dawa kwa muda wa siku 7 asubuhi na jioni kila siku atapona inshallah

-Akisha maliza kutumia kisha unipe mimi Feedback Source: PhD Mzizimkavu

Samahani mkuu, hii ni aina gani ya tiba? Nikimaanisha ime-base ktk taaluma ipi?
 
Mchemshie (Mbelewele) ndevu za maindi machanga anywe maji yake kila siku kama juice ni dawa.
 
dawa ya ndevu za mahindi ni nzuri niesikia imesaidia wengi. mara nyingi umri kuanzia miaka mitano huogopa giza, inaweza kusababisha hii hali, wanapata hofu kuamka usiku kwenda kukojoa.mfunze asiogope giza. mazoezi ya viungo ni muhimu hasa mgongo kiuno na tumbo ni vizuri afanye wakati wa jioni lengo ni kuimarisha bladder. lnawekana tatizo lisiwe tabia likahitaji matibabu. nashauri muone mtaalamu atakushauri zaidi.
 
Back
Top Bottom