kande kavu
JF-Expert Member
- Sep 17, 2011
- 234
- 86
Ni mabinti wawili mapacha na jirani zetu. Wazuriiii kwa sura na maumbile hasa yule wa pili.Wa kwanza ni mzungumzaji na mcheshi sana, mwingine ni mkimya na mwenye soni tele.Kisa hiki cha kweli kinamhusu yule binti wa pili.
Wakiwa kidato cha pili na binti wa kwanza akivuma kwa kugawa pipi, sifa nyingi zikapelekwa kwa huyu binti wa pili kwa utulivu. Hakuwahi kusimama atumwapo sokoni wala kisimani, hakuna mtu anashuhudia kuwa aliwahi kumuona huyu binti kasimama au kuongea na yeyote wa jinsia tofauti naye, kwani hata hao mabinti wenzie ilikuwa nadra.Wakati huo balekhe ikichanganya watu tulijaribu bahati zetu tukaambulia patupu kwani binti ni kakakuona.
Mimba jamani mimba! Mimba ni ngumu kuificha kumbe! Huyu binti wa pili akanasa mimba.Sijajua mpaka leo huyo kaka/baba/babu aliyemjaza mimba ile.Habari ikaenea kijiji chote, kwamba yule mpole,mkimya kapewa mimba ukizingatia enzi hizo mimba shuleni ilikuwa bado ni janga na msamiati. Sijui yule binti alizingatia ushauri wa nani, akaamua kwenda kutoa mimba ile. Alisafiri mpaka mkoa fulani hivi ambao sasa ni jiji. Baada ya mawiki kupita, siku moja basi la kutoka mjini likamshusha akiwa amekooonda na kupauka. Waliojua dalili za kutoa mimba wakashudia kuwa ile ni habari ya kweli.
Baada ya siku chache tangu kuwasili kwake kijijini, taarifa kamili ya habari ikaenea kijijini kuwa, zoezi la utoaji mimba awali halikufanikiwa kama ilivyotarajiwa. Baada ya mtumbo kuzidi kumuuma, akapelekwa kwa wataalamu zaidi. Huko akafahamishwa kuwa sehemu ya tumbo la uzazi imeoza na kuwa ikishughulikiwa hatazaa tena. Matibabu yakakamilishwa!
Binti huyu wa pili kuzaliwa ameshaolewa mara mbili na kuachika kwa sababu ya kutoshika mimba, na jamaa za karibu wanasema amekata tamaa sana, na kama angalizo imebidi dada yake mkubwa aishi naye nyumbani kwake japo binti anaweza kujitegemea kwa kipato chake!
SWALI:
Ni kweli watu wakimya huwa ni noooma kwa mikakati ya porini?
Mbona yule binti wa kwanza pamoja na machepele yake hayakumpata haya,je kuzungumza kwake kulisaidia kupatiwa njia za kukwepa mimba?
Ni kweli kuwa wanawake wengi inawawia vigumu kuishi bila mume?