Binti aacha shule akidai naye ameoteshwa

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Binti aacha shule akidai naye ameoteshwa

Imeandikwa na Na Abby Nkungu, Singida; Tarehe: 15th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 54; Jumla ya maoni: 0








WIMBI la watu wanaojitangaza wakidai wameoteshwa na Mungu kuweza kutoa tiba ya magonjwa sugu, limezidi kukua, safari hii ameibuka binti mwenye umri wa miaka 19 ambaye amelazimika kuacha shule aweze kujikita katika utoaji wa tiba ya kikombe.

Binti huyo, Zubeda Nassoro ni mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika shule ya Sekondari ya Mungumaji iliyopo katika Manispaa ya Singida. Zubeda amekiri kuacha shule, akisisitiza ameoteshwa na Mungu ili kutoa tiba mbadala ya magonjwa sugu yakiwemo Kifua kikuu, kifafa, kansa, kisukari na ukimwi.

Tofauti na watu wengine waliooteshwa kutoa kikombe, akiwamo mwasisi wa tiba hiyo, Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapila wa kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro, Zubeda yeye anatoza sh 1,100 kwa tiba ya ukimwi akidai mgonjwa atapona ndani ya siku tatu, huku magonjwa mengine yakichukua saa tano kupona.

Binti huyo, akizungumza nyumbani kwao katika kitongoji cha Irao- Nkuhi kijiji cha Mungumaji nje kidogo ya mji wa Singida alisema kuwa, katika miaka ya nyuma, alikuwa akitibu magonjwa ya kawaida kama malaria, kuhara na mengine mengi.

Alisema kuwa mapema mwezi Machi mwaka huu akiwa usingizini, alioteshwa na Mungu kwamba sasa ataacha kutibu magonjwa ya kawaida na ataanza rasmi kazi ya kutibu magonjwa sugu.

Alisema kuwa katika kuoteshwa huko, alielekezwa kwamba dawa za kutibu magonjwa sugu ni magome ya mti wa mwembe na kwamba malighafi hiyo ataipata kwa wingi mkoani Tabora. Akifafanua zaidi, alisema kila mgonjwa atapaswa kuja na kikombe chake na atalipa gharama
ya dawa sh 1,100/= tu.

Sh 500 ni kwa ajili ya mhudumu wake, Sh 500 atalipwa mtu atakayekuwa analeta magome ya mti wa mwembe kwa maelezo katika ndoto aliambiwa asiwe anafuata magome. Kiasi cha Sh 100 kitakachobaki kitakuwa mali yake.

Baba mzazi wa Zubeda, Nassoro Hamisi (44), alisema katika ukoo wao, wamewahi kuwa na watu wengi tu waliokuwa wakijishughulisha na kutibu kwa kutumia dawa za miti shamba.

Mkuu wa wilaya ya Singida, Pascal Mabiti amekiri kupata taarifa ya binti huyo kuoteshwa kutibu magonjwa sugu matano. Hata hivyo amesema ameshaaagiza wataalamu wa afya kuifanyia uchunguzi dawa hiyo.

Wakati binti huyo akiibuka mkoani Singida, mwandishi Joachim Nyambo anaripoti kutoka Chunya kuwa, mlemavu wa macho asiyeona kabisa, Simon Mahela naye ameibuka na kuanza kutoa tiba ya `kikombe’, akidai naye ameoteshwa kutoa tiba itakayofanya kazi na kuponya kabisa magonjwa katika kipindi cha siku 43.

Alianza kutoa tiba hiyo katikati ya wiki iliyopita katika kijiji cha Mbuyuni, wilayani hapa kwa gharama ya Sh 500.

Wakazi hao walise awali mtaalamu huyo alidai kuoteshwa mara kadhaa na babu yake ambaye sasa ni marehemu, lakini alikuwa akidharau hadi ilipofikia siku hiyo alipomuomba kijana mmoja amsindikize katika milima ya Iseche, Tarafa ya Kwimba, wilayani hapa kwa lengo la kuutafuta mti anaodai kuutumia kutibia magonjwa sugu.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mbuyuni, Romwad Mwashiuya alithibitisha kuibuka kwa mkazi huyo wa Mbuyuni na kusema kuwa Mahela anaishi kwa msaada wa kuongozwa na watu wa karibu.
 
Jamani tunapaswa kusali sana maana huko tunakoelekea hakueleweki. Watanzania wamekata tamaa na maisha na wamekuwa wepesi sana kupokea ndoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiibuka kila siku. Inawezekana kabisa kuna wengine wanadai kuoteshwa ndoto baada ya kupigika na maisha kama waigizaji wa futuhi walivyotuonesha juzi. Wale manabii wa television nao wameongezeka na sasa wamevamia na mikoani. Naunga mkono makala ya johson mbwambo ya kwenye gazeti la raia mwema la tarehe 6/4/2011 kwamba "tumekuwa taifa gonjwa"
 
nimeoteshwa kuwa hadi mwisho wa mwaka huu kutakuwa na watoa vikombe kwenye kila kata nchi hii.
 
Haya sijui wayafuata kutokea wapi?
Maana kawaida ya Ndoto inahitaji tafsiri. Zilizokua hazihitaji tafsiri ni zile za mitume watukufu enzi hizo. Hawa wanaoota sasa ndoto zao zahitaji kutafsiriwa.(Prediction) au (interpretation). Yanayobaki hapo ndio yale yale yasio muelekeo.
 
Ndugu zangu mwenyemacho haambiwi ona, subiri kidogo mtaona maajabu mengi mpaka mtashangaa! ukichelewa kumjuwa yesu utapata tabu sana. lakini nimesikia huko mbeya kijana alikuwa anatoa kikombe bure, majirani na wengine mtaani kwake wakasema atapata shida kuni na kufuata dawa mbozi sasa anatoza 500 lakini yeye hakutaka kutoza pesa.
pia kikombe cha ruvu ni bure kabisa!.
siku si nyingi mtasikia katika familia wameoteshwa zaidi ya mmoja!. hapo ndipo mtakapojuwa kuwa huyo siyo mungu bali ni miungu inayowaotesha!.
 
Hizi ndoto jamani? 2much! Tutashuhudia mengi mwaka huu, sielewi nini mwisho wake! Umakini unahtajika sana kwenye hili, vngnevyo mtakunywa vcvyonywewa.
 
unajua bana hapa africa cjui nisemeje!!! watu wanataka kuishi unajua wao wanafanya usenge''washenzi wakubwa labda kama wanafanya sample hili wajue watu wangapi wana ngoma ama vpi sababu kuna watu wanaugua wanataka uzima sasa haya mambo ya ksenge eti mungu kakuotesha ******** kunywa kikombe na babu yako
 
Back
Top Bottom