Rich Dad
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 748
- 133
- Thread starter
- #41
Mkuu naunga mkono hoja yako....KATIBA mpya ndio suluhisho la haya yote yatokeayo Tanzania, ndio mwongozo wa maisha ya kila mtanzania...kelele, matusi, kashfa, mabishano, ushabiki, malumbano ya sisi kwa sisi hayatatusaidia kuinusuru nchi hii huko tunakoelekea hasa kama hatutaki kumwaga damu...tujenge hoja kwa midahalo na makongamano, tujiulize na kujadili nini kiandikwe katika katiba, nini kiachwe, adhabu gani itolewe kwa mtoa rushwa na mla rushwa (wenzetu China wananyonga hawa), mafisadi, na masuala yote yanayoihusu nchi hii. Rostam anabebwa na mapungufu na udhaifu wa katiba yetu, anatumia mwanya wa tamaa waliyonayo ndugu zetu tuliowapa dhamana ya uongozi kuitafuna nchi hii, anawahonga, anawaingiza katika biashara zake kwa kuwapa pato fulani matokeo yake wanajisahau na kumwacha mtu huyu afanye anavyotaka katika hii nchi....
Wengi wetu (watanzania) hatuna uelewa wa katiba hata tukisema ianze kuandikwa leo tutashindwa hata kutoa maoni...tuisome katiba ya sasa na tujue mapungufu yako wapi ili tuandikapo katiba mpya asitokee mtu wa kuchezea watanzania na rasilimali zetu...TUNISIA Rais kakimbilia uhamishoni lakini je hilo ndio suluhisho la kuleta maendeleo, kumuua Rostam na mtandao wake si kuua vimelea vyote vya ufisadi nchi hii, kuna watu leo tunawaona wenzetu ila kesho tukiwapa nafasi hatutoamini kama ndio hawa tuliokuwa nao jana kundini
Asante mkuu! hapo mwishoni umemalizia vizuri sana!!!