Binadamu wa kwanza kuzaliwa na kuua

Wabongo tumekuwa watu wa ajabu kwa kuamini kila kitu tumeletewa na wazungu na ninaamini hata leo akitokea mzungu halafu aseme wao ndo walileta waafrika kuna waafrika wengi watakaomsapoti yaani tupo pabaya mno kwa kuendelea kujazwa ujinga na hawa wazungu na kuwaamini inashangaza eti mtu kusema kuwa hakuna mungu eti ni imagination tu yaani daah poleni sana waafrika
Kwa hio ww unataka kuniambia sio mwa-africa. Kama ni mwa-afrika basi pole na wewe.

But siamini ktk Uzungu, Naamini yupo Muumbaji halisi, ambaye ni Mungu.
Neno la Mungu ndio uthibitisho wa kile ninachoamini.
Bible ilikuepo toka ma-million ya miaka iliopita.
Na vizazi vyote vitapita lakini Bible itakuepo
 
Kumbuka hawa hawakuuana wakiwa watoto bali watu wazima kwa hiyo kwa kipindi wao wanakua na binadamu walikuwa wanazidi kuongezeka kupitia kwa wazazi wao yaani Adam na Hawa.

Na hata ukisoma maandiko matakatifu yanaeleza kwamba Adam na Hawa waliendelea kuzaa watoto wengine na kadri walivyokuwa wanazaa ndivyo kizazi kilizidi kukua kwa hiyo walikuwa na watoto wengine ukiacha Kaini na Habili ila mm nilichomaanisha ni kuwa binadamu wa kwanza kuzaliwa ni Kaini na baadaye nduguye Habili akazaliwa na ni huyuhuyu Kaini aliyekuwa binadamu wa kwanza kuua baada ya kumuua nduguye Habili.

Alitengwa ili asiuliwe na akina nani ni kuwa kipindi yeye na nduguye kaini wanakua pia watu walikuwa wanaongezeka kupitia adam na hawa na kipindi kaini anamuua ndugu yake tayari watu walikuwa wameshaongezeka.

Kwa Maelezo zaidi soma kitabu cha mwanzo kimeelezea kila kitu kwa undani

Acha kudanganya watu wewe, wengine tushawaza kuhusu hili swala tukawazua mpaka vichwa vikauma

Bible ni kitabu kigumu sana, Biblia inaeleza wazi kwamba, na baada ya Habili kuuawa, Adam akamjua mkewe Hawa kwa mala ya tatu akamzaa mtoto wa kiume wakampa jina Seti, wakamtukuza Mungu kwa kuwaondolea huzuni na kuwapatia mbadala ya mtoto wao aliyeuawa.

Hakuna sehemu kwenye biblia kumeandikwa ulivyoelezea hapa na mtoto wa tatu wa Adam na Eva ni Seti ambaye alizaliwa baada ya Habil kufa..swala la hao watu Cain alokuwa anaogopa watamuua walitoka wapi HALIPO.
 
Wabongo tumekuwa watu wa ajabu kwa kuamini kila kitu tumeletewa na wazungu na ninaamini hata leo akitokea mzungu halafu aseme wao ndo walileta waafrika kuna waafrika wengi watakaomsapoti yaani tupo pabaya mno kwa kuendelea kujazwa ujinga na hawa wazungu na kuwaamini inashangaza eti mtu kusema kuwa hakuna mungu eti ni imagination tu yaani daah poleni sana waafrika

Kwa hio ww unataka kuniambia sio mwa-africa. Kama ni mwa-afrika basi pole na wewe.

But siamini ktk Uzungu, Naamini yupo Muumbaji halisi, ambaye ni Mungu.
Neno la Mungu ndio uthibitisho wa kile ninachoamini.
Bible ilikuepo toka ma-million ya miaka iliopita.
Na vizazi vyote vitapita lakini Bible itakuepo
Lugha gongana
 
Duh ! Kwa majibu yaliyotolewa hapa, inaonyesha dhahiri watu wanaomwamini Mwenyezi Mungu idadi inazidi kuporomoka kwa kasi. Hatari kubwa hii.
Kumbe nawe umeligundua hilo mkuu nilifikiri ni mim tu.inaonesha jinc gani watu hawamjui Mungu kizazi hiki.
 
Wabongo tumekuwa watu wa ajabu kwa kuamini kila kitu tumeletewa na wazungu na ninaamini hata leo akitokea mzungu halafu aseme wao ndo walileta waafrika kuna waafrika wengi watakaomsapoti yaani tupo pabaya mno kwa kuendelea kujazwa ujinga na hawa wazungu na kuwaamini inashangaza eti mtu kusema kuwa hakuna mungu eti ni imagination tu yaani daah poleni sana waafrika
Hahahaha, nimecheka sana niliposoma comment yako, maana navyoona inakugeukia na kukulenga wewe mwenyewe tena. Sijajua umri wako, lakini naamini ni mtu mzima mwenye kuweza kudadavua mambo. Hivi Ukristo uliletwa na nani?
 
Jaman msiwe wavivu wa kusoma ndo maana watu wamekuwa wanajitoa mhanga na kujiua kwa kutojua yaliyoandikwa ..maaana mambo ya dini ni magumu sana unahitaji upate mwalimu wa kweli.

Sasa kuhusu hao watu waliokua wapo kipindi cha adam ni malaika waaasi wengine wanaita majini au mapepo kwa msaada zaid Google neno Nephilim ndo utapata jibu ya hao watu
 
3f0a8d625e7eb4cf29100f87e9066697.jpg

Ukiachana na wanasayansi wanaotudanganya kila kukicha juu ya chimbuko la binadamu neno la Mungu linatueleza kwa kinagaubaga chimbuko la binadamu pamoja na viumbe hai wengine namna walivyoumbwa na mwenyezi Mungu kwa hiyo viumbe hai vyote na visivyo hai vimeumbwa na mwenyezi Mungu.

Hebu leo basi tuangalie juu ya binadamu wa kwanza kabisa kuzaliwa na kuua. kadiri ya kitabu cha mwanzo (Bibilia) katika agano la kale baada ya Adam na mkewe Hawa kula tunda la kati walilokatazwa na Mungu, Mungu aliwatoa katika bustani ya Eden na kuwaamuru wakazae ili waijaze dunia.

Katika kitabu cha mwanzo kinaeleza baada ya Adam na Hawa kufukuzwa kwenye bustani ya Eden, Adam akamjua mkewe na wakapata mtoto wa kwanza KAINI na baadaye wakazaa mtoto mwingine kwa jina HABILI ambao hawa ndo wana wa kwanza wa Adam na Hawa na hawa Kaini na Habili walitunza imani yao kwa Mungu wakamtolea sadaka.

Habili alitoa sadaka yake kwa Mungu katika wanyama bora wa kundi lake akiwa na hali ya unyenyekevu na imani naye Mungu akampokea. Tabia ya Kaini ilikuwa ya kiburi bila ya kumcha Mungu, kwa hiyo Mungu alimkataa (mwanzo 4:1-5, soma ebr 11:4, 1yoh 3:12). Tabia na maisha ya watoaji wa sadaka ina maana kuliko vitu wanavyovitoa, kwa hiyo Mungu alimwambia Kaini kuwa akitaka Mungu ampokee angepaswa kushinda dhambi iliyokuwa ikitaka kumwangamiza. Dhambi hiyo ilikuwa kama mnyama wa mwitu ajikunjaye na kuotea mlangoni ili aweze kumshambulia mtu akitoka nje (mwanzo 4:6-7). Kaini hakushinda dhambi yake na katika hasira na wivu alimuua nduguye Habili.

Tendo lake la kutwaa uzima na ndugu yake ilidai kisasi kwa Mungu aliyetoa uhai ule, kwa hiyo Mungu alimfukuza Kaini aende mbali na mahali walipoishi watu wengine. Ingawa Kaini alidumu katika hali ya kutotubu Mungu katika huruma yake kubwa alimlinda asiuwawe kwa kisasi (mwanzo 4:8-16). Kwa hiyo katika maandiko matakatifu KAINI ndiye binadamu wa kwanza kuzaliwa na kuua baada ya kumuua nduguye HABILI.

God bless you

Nianze kushukuru kwa ufafanuzi wako huo mzuri ila nianze hivi, Adam na Hawa walikuwa na watoto 3 , Cain, Abel pamoja na Seth aliyezaliwa baada ya Abel kuuawa.

Cain alifukuzwa pale alipokuwa anaishi na akaenda mbele zaidi, ila alikuwa na hofu kuwa watu wakimwona watamuua ndio maana akawekewa alama usoni.

Swali wale watu Cain aliiogopa watumwua ni akina nani na walitoka wapi? Naomba kuwakilisha.
 
Simu ikiwa dukani huwa haiwekewi password lkn ikinunuliwa mtumiaji ndio huiekea password.
amini unavyoweza hayo ni maamuzi yako,
lkn usiache kutanguliza akili yako kabla ya kuamini.

naweza kuwaza, naweza kuandika.
wazo huleteleza matendo lkn maneno ni njia ya mawasiliano.

wazazi hurithisha kwa watoto wao,watoto nao huogopa kuhoji kwani wanauoga kwasababu wameogopeshwa! kipimo cha uhakika huchukua kitambo lkn kipimo kisicho uhakika hakichukui kitambo.
 
Simu ikiwa dukani huwa haiwekewi password lkn ikinunuliwa mtumiaji ndio huiekea password.
amini unavyoweza hayo ni maamuzi yako,
lkn usiache kutanguliza akili yako kabla ya kuamini.

naweza kuwaza, naweza kuandika.
wazo huleteleza matendo lkn maneno ni njia ya mawasiliano.
wazazi hurithisha kwa watoto wao,watoto nao huogopa kuhoji kwani wanauoga kwasababu wameogopeshwa!
kipimo cha uhakika huchukua kitambo lkn kipimo kisicho uhakika hakichukui kitambo.

Uko sahihi, kuamini ni kuamini na kushikilia kile unachokiamini bila kutumia akili.
 
Nianze kushukuru kwa ufafanuzi wako huo mzuri ila nianze hivi, Adam na Hawa walikuwa na watoto 3 , Cain, Abel pamoja na Seth aliyezaliwa baada ya Abel kuuawa. Cain alifukuzwa pale alipokuwa anaishi na akaenda mbele zaidi, ila alikuwa na hofu kuwa watu wakimwona watamuua ndio maana akawekewa alama usoni. Swali wale watu Cain aliiogopa watumwua ni akina nani na walitoka wapi? Naomba kuwakilisha.
Mkuu swali lako kuna sehemu nimelijibu hebu itafute hiyo comment uisome
 
Mkuu swali lako kuna sehemu nimelijibu hebu itafute hiyo comment uisome
Usikwepe swali kiujanja ujanja. Hebu toa ufafanuzi. Umesema wakati habil anauawa tayari kulikuwa na watu wengine wengi huku kuna wanaodai mtoto wa tatu wa Adam alipatikana baada ya habil kuuawa. Sasa hao watu wengine wengi unaosema wametoka wapi?
 
Ngoja nikueleze kitu kimoja ambacho ulikuwa hukijui labda na pia itategemea na akili na uwezo wako wa kufkiri. Ni hivi.

MUNGU ; Alipowaumba ADAM NA MKEWE aliwapa watoto wawili asubuhi na wawili jioni, kwa upeo wako ulivyo mdogo unaweza kuuliza mtu atazaaje asubuhi na jioni...?. Kwa MUNGU hilo ni jambo dogo tu kumbuka pia watu wa zamani si kama tulivyo sisi walikuwa tofauti sana na staki niende sana huko acha ni-stick kwenye mada yako.

Watoto waliozaliwa asubuhi ilikuwa hawaruhusiwi kuoana, isipokuwa wale wa jioni ndio ruksa kuoana nikimaanisha kwamba ; Asubuhi walipatikana mtoto we kike na wa kiume ambao hawakutakiwa kuoana na jioni hivyohivyo wawili, sasa huyu wa kiume wa asubuhi alitakiwa kumuoa wa kike wa jioni na vice-versa, hivyo kulikuwa na KABIL NA HABIL.

HABIL alikuwa ni mwenye sura nzuri ila dadake alikuwa ni mwenye sura mbaya na KABIL alikuwa na sura mbaya ila dada'ke alikuwa ni mzuri wa sura.

HABIL akamwambia itabidi nimuoe dada'ko na wee umuoe dada'ngu HABIL anamwambia KABIL mwenye sura mbaya KABIL akakataa katakata siwezi kukupa dada'ngu ana sura nzuri kisha unipe dada'ko mwenye sura mbaya. Huyu ntamuoa mwenyewe na wee muoe dada'ko mwenye sura mbaya.

HABIL akamwambia sheria haituruhusu mutants hivyo ni HARAM tutatenda dhambi, KABIL hakutaka kuelewa hata kidogo na ugomvi ukaanzia hapo ndipo KABIL akafkia hatua ya kumuua nduguye sababu ilikuwa ni mwanamke, sasa wee hukutueleza sababu ya Luis ilikuwa ni nini labda...?.

Ahsanta.
yn hii ni hadithi mpya kabisa kuwahi kuickia tangu nilipoliona jua, kweli hizi ni safari saba za Sindibadi Baharia
 
Binadamu wa kwanza kuzaliwa na kuua aliishi Mabibo Beach.....wafia dini acheni upotoshaji

Kama Mungu alimuumba Adamu na Eva na wao wakazaa watoto wawili wa kiume. Ambao ni Kaini na Habil. Na baadae Kaini akamuua Habili.

Swali;

Binadamu waliweza kuzaanaje mpk kufikia huu wingi tuliofikia hapa?
Au Adamu na Eva walizaa watoto wengine?
Au Habil aliamua kuzaa na mama ake ambye ni Eva?
hii kitu inaniacha hewani sana...

Embu ngoja nisiendelee kuchambua sana maana mtasema nakufuru
 
Ngoja nikueleze kitu kimoja ambacho ulikuwa hukijui labda na pia itategemea na akili na uwezo wako wa kufkiri. Ni hivi.

MUNGU ; Alipowaumba ADAM NA MKEWE aliwapa watoto wawili asubuhi na wawili jioni, kwa upeo wako ulivyo mdogo unaweza kuuliza mtu atazaaje asubuhi na jioni...?. Kwa MUNGU hilo ni jambo dogo tu kumbuka pia watu wa zamani si kama tulivyo sisi walikuwa tofauti sana na staki niende sana huko acha ni-stick kwenye mada yako.

Watoto waliozaliwa asubuhi ilikuwa hawaruhusiwi kuoana, isipokuwa wale wa jioni ndio ruksa kuoana nikimaanisha kwamba ; Asubuhi walipatikana mtoto we kike na wa kiume ambao hawakutakiwa kuoana na jioni hivyohivyo wawili, sasa huyu wa kiume wa asubuhi alitakiwa kumuoa wa kike wa jioni na vice-versa, hivyo kulikuwa na KABIL NA HABIL.

HABIL alikuwa ni mwenye sura nzuri ila dadake alikuwa ni mwenye sura mbaya na KABIL alikuwa na sura mbaya ila dada'ke alikuwa ni mzuri wa sura.

HABIL akamwambia itabidi nimuoe dada'ko na wee umuoe dada'ngu HABIL anamwambia KABIL mwenye sura mbaya KABIL akakataa katakata siwezi kukupa dada'ngu ana sura nzuri kisha unipe dada'ko mwenye sura mbaya. Huyu ntamuoa mwenyewe na wee muoe dada'ko mwenye sura mbaya.

HABIL akamwambia sheria haituruhusu mutants hivyo ni HARAM tutatenda dhambi, KABIL hakutaka kuelewa hata kidogo na ugomvi ukaanzia hapo ndipo KABIL akafkia hatua ya kumuua nduguye sababu ilikuwa ni mwanamke, sasa wee hukutueleza sababu ya Luis ilikuwa ni nini labda...?.

Ahsanta.

Mkuu maandiko yako umetoa wapi? Tupe chanzo
 
Kama Mungu alimuumba Adamu na Eva na wao wakazaa watoto wawili wa kiume. Ambao ni Kaini na Habil. Na baadae Kaini akamuua Habili.

Swali;

Binadamu waliweza kuzaanaje mpk kufikia huu wingi tuliofikia hapa?
Au Adamu na Eva walizaa watoto wengine?
Au Habil aliamua kuzaa na mama ake ambye ni Eva?
hii kitu inaniacha hewani sana...

Embu ngoja nisiendelee kuchambua sana maana mtasema nakufuru
1470245594536.jpg

Hiki. Kitabu kina majibu yote
 
Kama watoto wa Adam na Eva walikuwa wanaume na ni wawili tu, na mmoja kuuawa, na kubaki na wanaume wawili na mwanamke mmoja. Na huyo mwanamme aliyeuwa kupelekwa mbali. Sasa watu wengine wa mfano wao walitokea wapi? Na umesemaja muuaji alienda kwenye watu wengine, je inakuwaje hawa ndio wawe wa kwanza? Yawezekana maana ya neno Dunia kwenye Biblia ni tofauti na tunavyolitumia leo. Yawezekana wao dunia ni ile sehemu yz bustani ya Eden tu ambayo sijui kama ilikuwa kama inavyoelezwa kwenye Biblia.

Halafu hiyo picha uliotuwekea tutaamini vipi uhalisia wake?!

Ukiwa curious hivyo utasikia wewe 'amini' tu....Wataanza kugeuka kukuhukumu "huna imani wewe" ,utaenda motoni"....
 
Back
Top Bottom