Bin zubeiry upo sahihi,kwa hili simba na joyce kiria kuna tofauti gani?

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,640
33,421
Wasalam wanabodi,
Kwanza nikiwa mshabiki wa Simba napenda kuchukua fursa hii kuwatakia heri mchezo wa leo.naamini kwa uzoefu wa Simba na aina ya wachezaji waliopo sasa tunayo nafasi kuwatambia Wanyarwanda leo.
Wanajamvi leo nimesoma makala ktk gazeti la Dimba iliyoandikwa na mwandishi BIN ZUBEIRY nikaona si vibaya na sisi hapa tukaijadili kidogo kuwapa changamoto viongozi wa Simba.Timu ya Simba imezindua kipindi chao kitachokuwa kinarushwa na Clouds Tv kila wiki ambacho ni kitu kizuri lakini kwa timu kama Simba kuwa na Tv show kuna tofauti gani na Joyce Kiria Nkongo mwenye Wanawake Live? Simba ni timu kongwe yenye washabiki mamilioni kwanini wasijaribu kufanya makubwa kama kuomba channel pale startimes wakamiliki TV yao? kama alivyosema mwandishi wa makala kama viongozi na wanachama maarufu wa Simba wana Radio stations na Tv kubwa kwanini Timu yenye jina kubwa kuliko hata majina ya viongozi hao wamiliki kipindi tu? Rage anayo radio station ya kisasa kuliko radio nyingi tu hapa Dar na Hata Abood wa Moro ni hivyo hivyo! Kwanini viongozi wanaogopa kufanya makubwa na kuishia kutaka sifa kwa ku host kipindi tu kama Wanawake Live ya Joyce Kiria? Kwa hili viongozi wa Simba hatuwezi kuwasifu kwa kujaribu kitu kidogo namna hii.Mods naamini kwa maana halisi ya jukwaa hili sijakosea kuirusha huku.
 
Rage na viongozi wengine we need Something Big than this!!
 
Mkuu mbona unawaza mbali sana?, ka jengo lao tu wameshindwa kulikarabati itakuwa kufungua radio au Tv! Hz ni ndoto
Nadhani hata na hy ya kipindi watakuwa wameshawishiwa na watu wa Clouds, ili nao waingize pesa!
 
Mkuu mbona unawaza mbali sana?, ka jengo lao tu wameshindwa kulikarabati itakuwa kufungua radio au Tv! Hz ni ndoto
Nadhani hata na hy ya kipindi watakuwa wameshawishiwa na watu wa Clouds, ili nao waingize pesa!
Ni kweli mkuu inawezekana kuna ushawishi wa Clouds Media maana Ibrahim Masoud ni matayarishaji na mtangazaji nguli pale Clouds na ni Kiongozi wa Ufundi Simba!!
 
Ezekiel Kamwaga naamini wewe ni msomaji mzuri au pengine ni mwanaJF pia ni mtu makini,hebu tuambie ndugu mbwembwe zote zile za nini ku host kipindi tu kwenye Tv ya watu?
 
Back
Top Bottom