Bima ya Afya

luvara

Senior Member
Apr 9, 2011
170
40
Bima ya afya imekuwa inajitanua kila siku ila kwa bahati mbaya huduma zake kwa baadhi yetu ni mbaya sana. Yaani ni sawa na wizi wa mchana. Tunakatwa hela kwenye mishara yetu lakini hatupati huduma. Ukienda hospitali uaambiwa ukanunue dawa au kipimo hiki lipia. Kwa hiyo wengine tumeshindwa na tumeamua kukata tamaa na kujilipia bila kujali kwamba tuna bima, vitambulisho tulivyo navyo ni ushahidi tu wa wizi wa NHIF.

Hata hivyo kwa jinsi nchi yetu ilivyo wakati wa kuwa na kitu kama bima ya afya ulikuwa haujafika, ufisadi na kutokuwajibika ni kwa hali ya juu sana. Hili linanifanya nihisi kwamba hata aliyebuni na kuanzisha mfumo huu hapa nchini ni fisadi papa na lengo lake ni yeye kunufaika binafsi. Na ndio maana sasa bima ya afya badala ya kuboresha huduma zake imegeuka na kuwa chombo cha kudhamini mambo yasiyo na faida kwa wachangiaji.

Ningependa kujitoa kwenye bima ya afya hata hivi leo. Kama kuna anayejua utaratibu wa kujitoa aniaambie kwani atakuwa ameniepusha na ubarazuli wa kunufaisha kundi la wanaokula bila kunawa.
 
NHIF sio hif hamna kujitoa unakomae na hao madaktari wanakuomba kakiwemo kale kamsemo ketu ka Tanzania "unanijua mimi ni nani" hata kama huna cheo chochote mbona kitaeleweka na utapata matibabu bure.
 
wakuu samahani kwanza naomba kujua hawa jamaa wanapatikana wap? Kwa hapa dar utaratibu wao ili upate hyo bima vinahitajika vitu gan? Je malipo yao kwa mwaka ni kiasi gan? Kwa mtu km mi ambaye sijaajiliwa popote yaan nimejiajiri nahitaj vitu vp ?ili kupata hyo kadi nisaidien wadau
 
nimekuja mbio..., nljua nn tena, ok, wenye kujua watakujuza wanapopatkana, wengne ni ma member ila tuliletewa card zetu ofisini.
 
Makao makuu yao yapo mamlaka ya bandari kule,nafikiri jengo linalofuata ni Bima nenda hapo utapata maelezo yote mkuu
 
Mkuu umenishtua sana . Nilidhani wanachama tumefanyiwa kitu mbaya. Mawasiliano yao haya hapa: Mkurugenzi Mkuu, P.O.Box 11360, DSM. Simu +255 22 2130826. Barua pepe: info@nhif.org.tz. Nawasilisha.
 
Nakushauri uende bima nyingine kwani hawa ni wasanii tu. Sisi tulio na kadi hatupati huduma ya maana. Ningeweza kutoka ningetoka ila tulilazimishwa tu na serikali kwa vile yeye ndio mwajiri na anatulipa mishahara hivyo alianza kutukata juu kwa juu. Ulizia AAR na wengineo. Huko utapata huduma nzuri.
wakuu samahani kwanza naomba kujua hawa jamaa wanapatikana wap? Kwa hapa dar utaratibu wao ili upate hyo bima vinahitajika vitu gan? Je malipo yao kwa mwaka ni kiasi gan? Kwa mtu km mi ambaye sijaajiliwa popote yaan nimejiajiri nahitaj vitu vp ?ili kupata hyo kadi nisaidien wadau
 
Nakushauri uende bima nyingine kwani hawa ni wasanii tu. Sisi tulio na kadi hatupati huduma ya maana. Ningeweza kutoka ningetoka ila tulilazimishwa tu na serikali kwa vile yeye ndio mwajiri na anatulipa mishahara hivyo alianza kutukata juu kwa juu. Ulizia AAR na wengineo. Huko utapata huduma nzuri.

KAKA KUTOA USHAURI KWA MTU BILA KUFANYA UTAFITI NI KUMPOTOSHA MTU, MM NI MFAIDIKA WA BIMA YA AFYA YA TAIFA, HIYO AAR UNAYOSEMA KABLA HUJAJIUNGA WANAKUPIMA AFYA YAKO, KAMA HAIRIDHISHI HAWAKUKUBALII PIA AAR GHARAMA NI KUBWA HADI KUFIKIA KIWANGO CHA MCHANGO MIL 18 kwa mwaka kwa MTU mmoja, ambayo NI tofauti Na bima ya afya ya taifa ambayo wanachukua 3% ya mshahara wako ambayo inahudumia familia yako yote,
2. AAR WANA KIKOMO CHA UMRI KUANZIA MIAKA 55 HAWAKUKUBALII KUJIUNGA KTK BIMA YAO TOFAUTI NA BIMA YA AFYA WANAKUHUDUMIA HATA UKISTAAFU MPAKA KIFO CHAKO,
3. kimtandao bima ya AFYA ya taifa ipo nchi nzima Na hospital karibu zote za binafsi kubwa Na ndogo tofauti Na AAR ambao wapo miji michache sana

YAKO MAMBO MENGI SANA YA UBWETE KTK BIMANYA AFYA YA TAIFA KAMA HUJAELEWAMULIZA NITAKUFAFANULIA
 
Zipo ofisi mbalimbali za kanda.. ninayoijua ni Mwenge karibu na Majembe auction mart na makao makuu ni Kurasini karibu na bandari.

Mlolongo wao sasa kaaa.. inabidi ujipange sawasawa hasa ukizingatia wewe ni binafsi, mimi nimepata kwa kuwa ni mtumishi wa Uma ila nilifuatailia karibu mwaka mzima.. Labda kama wamejirekibisha.
 
Asiwadanganye mtu yeyote mm ni mfaidika ukifuata taratibu zinazohitajika unapata kadi yako mapema tena bila usumbufu
Tatizo la watanzania wengi hatupendi kufuata taratibu
 
Nakushauri uende bima nyingine kwani hawa ni wasanii tu. Sisi tulio na kadi hatupati huduma ya maana. Ningeweza kutoka ningetoka ila tulilazimishwa tu na serikali kwa vile yeye ndio mwajiri na anatulipa mishahara hivyo alianza kutukata juu kwa juu. Ulizia AAR na wengineo. Huko utapata huduma nzuri.

wacha kumpotosha mwenzako. wengine wana kadi hiyo ya nhif na wanaishukuru kila kukicha. mwacho aipate ajionee mwenyewe. akishindwa atahamia hizo zingine.
 
Mimi ni mmoja wa familia ninayetumia kadi ya bima ya taifa, lakini chakushangaza huduma ya bure niliyoiona ni kua niliandikiwa dawa lakini dawa nilizopewa bure kupitia bima hii ya taifa ni Paracetamol lakini dawa nyingine nikaambiwa nikanunue!

Mnanishauri nini?
 
wacha kumpotosha
mwenzako. wengine wana kadi hiyo ya nhif na wanaishukuru kila kukicha.
mwacho aipate ajionee mwenyewe. akishindwa atahamia hizo
zingine.

mimi binafsi naishukuru sana bima ya afya ya taifa na hata nikikosa dawa hosptal kuna maduka yana huduma hizo kwa hiyo nikiugua na sina pesa bado ni na amani
 
Mimi ni mmoja wa familia ninayetumia kadi ya bima ya taifa, lakini chakushangaza huduma ya bure niliyoiona ni kua niliandikiwa dawa lakini dawa nilizopewa bure kupitia bima hii ya taifa ni Paracetamol lakini dawa nyingine nikaambiwa nikanunue!

Mnanishauri nini?

Maduka mengi kwa sasa yana huduma za bima nenda utapata
 
Back
Top Bottom