Bima ya afya kwa watu wenye kipato kidogo

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wana JF na wapenda maendeleo. Leo asubuhi (saa 12) nilikuwa nasikiliza kipindi cha BBC na walikuwa na Makala ya Kimasomaso kuhusu Rwanda. Mchangiaji alikuwa mmoja wa mawaziri (nadhani Waziri wa Afya) na alisema wananchi wenye kipato cha chini wana bima ya afya, ambayo wanachangia kwa kulipa sawa na US$2 (dola 2) kwa mwaka.

Kutokana na hiyo, wanapata huduma ya afya kwa kuchangia 10%. Nilipojaribu kuzigeuza kwa hela za kwetu, nikakuta kuwa kama matibabu yatagharimu 1,000,000/- wao wanachangia 100,000/- au kama ni 100,000/- basi wanalipa 10,000/-. Ndivyo nilivyoelewa.

Kama Rwanda, ambayo imekuwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu 1994 hadi miaka ya hivi karibuni, wameweza kutoa bima kwa wananchi wake, ni kweli Tanzania tunashindwa hasa kwa kuzingatia kuwa tuna madini ya kila aina? Kama Chadema walivyokuwa wanasema wakati wa kampeni, kama viongozi wetu wanaona bima ya afya nayo haiwezekani kwa wananchi si wawapishe viongozi wanaoweza kuiifanya iwezekane?
 
Hiyo imetulia bongo hata kwa dawa haiwezekani viongozi wetu wataiba wapi ka pesa zitatumika kwa wananchi?
 
nani alipe madeni ya dowans? hii ndio bongo bana kuliwa kwingiiiiiiiii
 
Tanzania kuna Bima ya afya kwa watu wenye kipato cha chini inaitwa "Community Health Fund" (CHF)

Ni voluntary kwa wananchi wote iko katika halmshauri 29 hadi 2008 sijui kwa sasa?

Premium ni 5000-10000 kwa wilaya tofauti kwa matibabu ya mwaka hospitali/dispensary ya serikali

Rwanda walikuja ku-copy kwetu, as usual wao wanaimplement vizuri sisi tunaweza kudesign (paperwork vizuri)

Implementation sifuri

Mdau wizara ya afya Tanzania.
 
Back
Top Bottom