Billion 9.9 kwa ajili ya matanuzi ya Viongozi na Wastaafu wa Zanzibar!!!

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,407
54,886
..jamani hivi huu si mzigo mzito sana kuwatwisha wananchi wa Zanzibar?

..halafu baadhi ya wanaonufaika na ubadhirifu huu tayari wanatambulika kama viongozi, au wastaafu, katika serikali ya muungano.

..wakati huo huo tunaambiwa hospitali kuu ya Mnazi Mmoja haina kifaa cha Ultrasound kwa sababu ya ukata wa pesa wakati viongozi wametengewa mabilioni.

..habari hii nimeipata gazeti la Nipashe.


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema inatarajia kutumia Sh Bilioni 9.9 kuwahudumia viongozi wake wakiwemo wastaafu kwa kuwalipa pensheni na safari za nje katika Mwaka huu Fedha.


Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Uchumi Omar Yussuf Mzee, Wakati akifunga mjadala wa Bajeti yake katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea katika mji wa Chukwani mjini Zanzibar.


Alisema kwamba kati ya fedha hizo Sh Bilioni 4.4 zitatumika kwa Safari za nje kwa viongozi wa kitaifa wa Serikali pamoja na viongozi wake wastaafu Zanzibar.


Aliwataja viongozi watakao nufaika na kasma hiyo kuwa ni marais wastaafu ambao ni Ali Hassan Mwinyi, Dk Salmin Amour Juma, Amani Abeid Karume, naa Aboud Jumbe Mwinyi.


Aidha aliwataja mawaziri kiongozi wastaafu kuwa ni Ramadhani Haji Faki, Dk Mohammed Gharib Bilali na Waziri wa Mambo ya ndani Shamsi Vuai Nahodha.


Aidha alisema fedha hizo zimetengwa pia kwa ajili ya malipo ya pensheni mbali na kutumika kwa gharama za safari za nje kwa viongozi hao, lakini hakusema viongozi hao wastaafu Zanzibar wamekuwa wakilipwa kiwango gani cha fedha kila mwezi.


Waziri Omar ametoa ufafanuzi huo baada ya Ismail Jussa Ladhu (Mji Mkongwe) kulalamika kwamba Sh Bilioni 4.5 zilizotengwa kwa Safari ni kiwango kikubwa kutokana na Zanzibar kukabiliwa na matatizo mbali mbali ya huduma za jamii kwa wananchi wake.


Hata hivyo, Waziri Omar alisema kiwango hicho cha fedha ni cha kawaida kwa sababu pia kitatumiwa na viongozi wa kitaifa serikalini akiwemo Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed na makamu wake Maalim Seif Sharif Hamad, na Balozi Seif Ali Iddi.
 
Wana mafuta mkuu kwa hiyo Tsh. billioni 9.9 siyo kitu au umesahau? Labda hiyo billioni 9.9 iwe kwa dollar ndiyo itaweza kuwapa taabu...
 
Back
Top Bottom