Bilioni 8, na milioni 500 ya dhamana kwa Iddi simba

Hivi huyu ndiye yule Idd Simba ambaye ni mwenyekiti wa 'wazee wa DSM' amabo mheshiwa Rais anawatumia kuwakilisha ujumbe kwa watanzania wote ikiwa kuna jambo tete nchini kama mgomo wa wafanyakazi/ madaktari n.k ? mwenye kujua naomba anijuze tafadhali.
Ndio huyo haswaa!
 
Shughuli ni pevu kwa Idd Simba. Ila huyu mzee alipiga pesa ndefu sana enzi zile ni waziri wa viwanda na biashara,inasemekana alikuwa anafanikisha deal chafu za wamiliki wa viwanda hususani Ilala kutokulipa kodi.So sishangai maana wahindi walikuwa wanapatia fungu la kumi lililonona ,kitumbua kiliingia mchanga kwenye deal la sukari.
 
Kweli Tanzania imeendelea kuwa shamba la bibi kwani baada ya Idd Simba jana kufikishwa mahakamani na kesi hiyo kuahirishwa alitakiwa kutoa hati yenye thamani ya milioni 500 kama dhamana lakini Idd Simba alivunja rekodi baada ya kutoa hati ya bilioni 8 kama dhamana
swali;Jamani hivi bilioni 8 ni fedha zake halali kweli?
Kama sio kwanini asifunguliwe kesi nyingine ya ufisadi?
Nawasilisha
source ITV

tatizo la mfumo wa sheria zetu ni kuwa ukimfungulia mashitaka utatakiwa kuthibitisha kuwa fedha hiyo siyo halali, itakughalimu zaidi......... Endelea kunywa tusker yako ulale mapema, kwa sheria za tanzania hilo ni gumu kama kumzuia obama asicheze na mbwa wake.
 
Enzi za mwalimu alikuwa mkurugenzi wa State Motor Corporation. Kifupi ukitaka kununua gari unapitia kwake kupata kibali. Kibali kununua gari kilikuwa kama kibali cha kumiliki bastola. Kupata kibali tu pamoja na kwamba hela ni zako ilikuwa mbinde.
 
Back
Top Bottom