Bilioni 5 zatafunwa ttcl na wajanja

kapuchi

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
268
163
Kampui ya simu tanzania imeingia kwenye matatizo ya ufisadi baada ya wafanyakazi wake kudaiwa kuiba Tshs Bil 5 zilizotakiwa kupelekwa TRA.

Inasemekana ufusadi huu ulifanywa na wafanyakazi wa ndani wakishirikiana na benki tofauti na mashirika mbalimbali ambao wahasibu wake walikubali kupitishia fedha hizo kwenye akaunti zao kwa ahdi ya kupata mgao.

wadau mpo?

source ,Gazeti la MWANACHI
 
Kuibiwa mabilioni siyo sasa imekuwa ni kawaida tu kati ya mambo wanayofanyiwa Watanzania? Hakuna kitu chochote kitakachotokea kwani walioiba watalindwa ile mbaya.

Ukiacha wananchi wachache sana, wengi ni kama "sheep in the field" (kunradhi kwa maneno haya kwani ni onyesho langu la huzuni kubwa). Hawatafanya chochote kwani wengi wao hata magazeti yanayoandika haya yote hawasomi, sana sana hununua na/au husoma magazeti ya udaku tu na yale ya michezo ambayo yote hayo yanasheheni asilimia 90 uongo. Saa ngapi wafikirie wafanye nini wanapoibiwa mchana mchana?
 
Last edited:

...You have a BIG point there, Mkuu. Jana alasiri nimezungumza na wafanyakazi watatu wa TTCL ambao ni jamaa zangu hakuna hata aliyekuwa anafahamu kuwa kulikuwa na habari hiyo kwenye gazeti! Na wote wako kwenye ofisi zilizo katikati ya jiji! Yaani mimi ndio nikaanza kuwasomea habari hiyo kupitia kwenye simu! Hebu fikiria, Mfanyakazi wa Shirika la UMMA ambaye mshahara wake una ahueni kidogo kuliko wa mfanyakazi wa serikali anaona ubahili kununua gazeti la shilingi mia 400 kwa siku ili kupata habari!! Umesema kweli, wengi wa sisi Watanzania ni 'Sheep in the Field'! Tupo tupo Tu! Inauma lakini ndio ukweli halisi.
 
Back
Top Bottom