Bilioni 300 zaibiwa kimafia Dar...

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
  • NI MARA TATU YA WIZI WA EPA;
  • DCI MANUMBA ASEMA TAARIFA ZINAFANYIWA KAZI

Ramadhan Semtawa

WATU wasiofahamika wameghushi nyaraka za malipo na kuiba zaidi ya Sh300 bilioni katika benki tatu kubwa nchini na kusababisha mtikisiko mkubwa katika sekta ya fedha, uchunguzi umeonyesha.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, fedha hizo ziliibwa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni kabisa mwa mwaka huu, kwa njia ya mtandao wa kompyuta na kuhusisha wezi wa kimataifa ndani na nje ya nchi.

Tukio hilo ambalo ni kubwa kuwahi kutikisa sekta ya fedha nchini tangu uhuru mwaka 1961, limetokea katika kipindi cha takribani miaka miwili tangu serikali ianzishe kitengo maalumu cha Intelejensia cha kufuatilia Mzunguko wa Fedha chafu (FIU).

Licha ya kuwepo FIU, ambayo iliundwa pamoja na Sheria ya Kupambana na Fedha Chafu ya mwaka 2007, uchunguzi wa Mwananchi, umebaini kutokea wizi huo mkubwa katika benki hizo.

Uchunguzi huo umebaini kwamba, taarifa za awali zinaonyesha fedha hizo ambazo ni mara tatu ya zile za EPA zilizoibwa katika Benki Kuu Tanzania (BoT), zilihamishwa kwa njia ya kompyuta kwa kughushi malipo kwenda kwa wahusika wa mtandao huo katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani ambako Polisi wa Kimataifa wa nchini na wenzao wanahaha kuzichunguza.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, alipoulizwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, alithibitisha kuwepo taarifa za uhalifu huo, lakini akaweka bayana, hakuna ushahidi wa kiwango maalumu kilichoibwa hadi sasa.

"Hizo taarifa zipo zinafanyiwa kazi, ila haijathibitika ni kiasi gani cha fedha kimeibwa na benki zipi hasa, kwa hiyo kusema ni Sh300 bilioni au zaidi ya hapo, si sahihi hakuna uthibitisho wowote," alifafanua DCI Kamishna Manumba.

DCI Manumba aliongeza kwamba, baada ya uchunguzi kukamilika polisi itatoa taarifa za kina, sahihi na kwa wakati kwa wananchi na kusisitiza, "Kwa sasa ngoja tufanye kazi."

Hata hivyo, DCI Manumba alionya na kuzitaka benki na watu wengine kuwa makini katika kuangalia usalama wa mali na fedha katika kipindi chote.

"Unajua, mambo ya uhalifu sisi tunajitahidi kukabiliana nayo lakini bado wengine wanaendelea kwa kutumia mbinu mbalimbali. Kwa mfano tunazuia watu wasibakwe, lakini wanabakwa, hii yote inaonyesha umuhimu wa watu kuwa makini," alifafanua DCI Manumba.

Gavana wa Benki Kuu (BoT) Profesa Benno Ndulu, alipoulizwa kuhusu sakata hilo alisema yuko nje ya nchi kikazi.

"Niko Sweden kikazi, halafu hapa siwezi kukusikia vizuri wala kuzungumza vema kwani kuna shughuli ambayo nimehudhuria," alisema Profesa Ndulu, ambaye taasisi kuu ya fedha ya nchi ina wajibu wa kusimamia benki na taasisi zote za fedha nchini.

Baadhi ya maofisa wa benki hizo ambazo majina yake tunayahifadhi, wamethibitisha kukumbwa na uhalifu huo mkubwa na kwamba wameacha suala hilo mikononi mwa vyombo vya dola.

"Ni kweli kuna vitenfo vya kughushi vimetokea katika benki yetu, lakini hilo hatuwezi kulizungumzia kwa kina kwasababu liko mikononi mwa vyombo vya dola. Polisi wanaweza kulizungumzia hilo," alifafanua ofisa kutoka moja ya benki iliyoibiwa kiasi kikubwa cha fedha karibu Sh100 bilioni.

Wakati DCI Kamishna Manumba, Gavana Ndulu na maofisa wa benki wakizungumzia hayo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba, fedha hizo ziliibwa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni kabisa mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, hadi sasa taarifa za awali zinaonyesha mpango huo mchafu umeanzia ndani ya benki kwa kuhusisha baadhi ya watu ambao ni wanamtandao na wezi wenzao nje ya nchi.

Mwananchi imebaini kwamba, hadi sasa Idara ya Interpol Tanzania kwa kushirikiana na wenzao wa nje wanafanya uchunguzi huo wa kina katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani ambako taarifa za awali zinaonyesha fedha hizo zilikwenda.

Katika uchunguzi huo, Mwananchi imebaini kwamba baada ya mpango huo kufanywa nchini fedha hizo zinaonyesha zilihamishwa kwa njia hiyo ya kughushi kwenda nchi hizo.

Vyanzo hivyo vya habari za kiuchunguzi, zilifafanua kwamba baadhi ya watu katika mabenki hayo ambao wanafahamu mzunguko wa fedha ikiwemo malipo ya ndani na nje, wamepanga njama hizo na kughushi malipo kwa kushirikiana na mtandao mkubwa wa wezi wenzao wa nje ya mabenki ndani na nje.

Habari hizo za kiuchunguzi, zinaonyesha kwamba wizi huo umetikisa mabenki hayo kiuchumi huku duru za kiusalama zikisema vyombo vya usalama vimekuwa makini kuangalia fedha hizo zimeingia mikononi mwa watu gani.

Mwananchi imebaini kwamba, kiasi hicho kikubwa cha fedha kinaweza kuweka usalama wa taifa hatarini endapo kitakuwa kimeingia kwenye mikono ya watu ambao wana nia mbaya na nchi.

"Ni kiasi kikubwa cha fedha, kama kitakuwa kimeingia kwenye mikono ya watu hatari wanaweza kuhatarisha usalama wa nchi, bilioni 300 si kitu kidogo," kilisema chanzo kimoja kutoka moja ya vyombo vya usalama.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kitisho kingine kinachoangaliwa hadi sasa ni iwapo fedha hizo zimeibwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba kwa ajili ya kundi fulani ikiwemo mafisadi kutaka kuzitumia kutimiza malengo yao.

"Tunaangalia pia, maana inawezekana ni mafisadi wakubwa ambao wanajua mzunguko wa fedha ndiyo wamekula njama na kutaka kuhujumu nchi kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu," kilifafanua chanzo hicho.

Ingawa haijathibitika, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kuliibuka ufisadi mkubwa katika BoT ambao zaidi ya Sh 133 bilioni ziliibwa.
 
TISS inafanya kazi gani?
Wako busy na sheria ya uchaguzi na kuhakikisha hakuna mgombea huru kusimama kwenye uchaguzi ujao.Pengine pia na kuendelea na kudadisi wanywa pombe wanasema nini baada ya kulewa.
 
Haya ni madhara ya kutumia technology bila kwanza kuweka wataalamu [waaminifu] wa kutosha kwenye mabenki, sheria, polisi na utawala.

Historia inatuambia tuko wazito mno kujifunza, matukio kama haya yatatokea mara nyingi tu huko mbeleni.

Whatch this space!
 
What this space!
Priority yetu sio technology...ni siasa na ndio maana wajanja wamegundua weakness hiyo wana capitalize.
 
BoT watakuwa wanahusika kwa sababu walianzisha mfumo ambao kila transaction inayozidi Sh bilioni kumi ni lazima ipite kwao
 
I guess there is misrepresentation of facts katika habari hii, kwa ambao tuko informed, ukisoma habari nzima utagundua mapungufu mengi. Siwezi kumlaumu mwandishi, tatizo liko kwenye vyanzo vyake, havijamtanabaisha mwandishi vya kutosha.

Hata kama Benno Ndulu akisafiri, kuna mtu ana act on his position, kwa nini asiwafuate kwa details zaidi? Kapata wapi estimation za TZS. 300 Bil? Je alifanya juhudi zozote za kumtafuta mkurugenzi wa FIU ambao ndio wahusika wakuu wa wizi wa namna hii hapa nchini?

Kuna madhala makubwa sana katika uchumi ambayo yanaweza kutokea kutokana na upotoshwaji kama huu. Wengi wetu tunajua namna masoko ya fedha na hisa yanavyoendesha ambapo kwa asilimia kubwa yanaendeshwa na perception ya players katika soko. Tayari hapa nchini kuna benki kadhaa ziko listed kwenye soko la hisa la DSM, the moment habari zinavuja (either facts or fabricated/exaggarated stories), basi bei za hisa zitaporomoka isivyo kawaida na kuondoa stakeholder's confidence kwenye taasisi za fedha hapa nchini.

Ukiangalia capitalization za benki zetu hapa nchini, upotevu wa namna hiyo unaweza kuwa absorbed na benki kama tatu tu.

Kwa habari ya uchunguzi kama hii, mwandishi angeweza kusubiri na kuuliza players mbali mbali kwa details za uhakika zaidi.
 
...Brooklyn, waandishi wenyewe wa kufanya aina hiyo ua uchunguzi wako wapi?? hawa hawa wetu??
 
...Brooklyn, waandishi wenyewe wa kufanya aina hiyo ua uchunguzi wako wapi?? hawa hawa wetu??

Media houses need to seriously equip their staff. Kwa Tanzania si ajabu ukakuta habari kama hii imeanzia pale Rose Garden, mwandishi kaisikia na haraka haraka akampigia simu Manumba akamwambia hizo habari na yeye anazo kisha akampigia na Ndulu akaambiwa yuko safarini........kesha yake unaiona habari kwenye front page ya gazeti Bilioni 300 zaibwa kimafia Dar.

Huwezi ukawa una ripoti serious news kama udaku wa kwenye gazeti la Kiu ama Ijumaa. Ndio maana credibility ya print media zetu imeporomoka sana, kila habari unayosoma unagundua mwandishi hakufanya homework vya kutosha.

Cha ajabu hata 'reported news' kama za press conference, kunakuwa na mapungufu. Mara kadhaa tumekuwa tukishuhudia taasisi na watu binafsi wanaofanya press conference wakirudi tena kurekebisha habari zilizokosewa kuripotiwa.

Je hawa wanaojiita ma editors wana kazi gani? Hao na wenyewe ni makanjanja???
 
I guess there is misrepresentation of facts katika habari hii, kwa ambao tuko informed, ukisoma habari nzima utagundua mapungufu mengi. Siwezi kumlaumu mwandishi, tatizo liko kwenye vyanzo vyake, havijamtanabaisha mwandishi vya kutosha.

Hata kama Benno Ndulu akisafiri, kuna mtu ana act on his position, kwa nini asiwafuate kwa details zaidi? Kapata wapi estimation za TZS. 300 Bil? Je alifanya juhudi zozote za kumtafuta mkurugenzi wa FIU ambao ndio wahusika wakuu wa wizi wa namna hii hapa nchini?

Kuna madhala makubwa sana katika uchumi ambayo yanaweza kutokea kutokana na upotoshwaji kama huu. Wengi wetu tunajua namna masoko ya fedha na hisa yanavyoendesha ambapo kwa asilimia kubwa yanaendeshwa na perception ya players katika soko. Tayari hapa nchini kuna benki kadhaa ziko listed kwenye soko la hisa la DSM, the moment habari zinavuja (either facts or fabricated/exaggarated stories), basi bei za hisa zitaporomoka isivyo kawaida na kuondoa stakeholder's confidence kwenye taasisi za fedha hapa nchini.

Ukiangalia capitalization za benki zetu hapa nchini, upotevu wa namna hiyo unaweza kuwa absorbed na benki kama tatu tu.

Kwa habari ya uchunguzi kama hii, mwandishi angeweza kusubiri na kuuliza players mbali mbali kwa details za uhakika zaidi.

Have also noted that, hii habari ilitaka uchunguzi wa kina sana, ndio maana hata wahusika wote wa uharifu huu hawakuwa tayari kuripoti....this could be devastating news to the national economy and also stability...sio habari ya kuandika kiushabiki na kulinganisha na ufisadi kuelekea uchaguzi...tungependa kusikia habari kamili,benki gani zimeibiwa? how was it done? nini kifanyike na nini kinafanyika..
 
Nazungumzia ile ya banking kuhusu payments of huge amount of money

Hii taasisi kwani haipaswi kuangalia mabo haya mkuu?....kumbe tunalalamika hali kipesa mbaya since January watu wavevuta..duh...mbona ni miaka ya uchaguzi tu madudud haya yanatokea..I will hate years divisible by 5 now!
 
Media houses need to seriously equip their staff. Kwa Tanzania si ajabu ukakuta habari kama hii imeanzia pale Rose Garden, mwandishi kaisikia na haraka haraka akampigia simu Manumba akamwambia hizo habari na yeye anazo kisha akampigia na Ndulu akaambiwa yuko safarini........kesha yake unaiona habari kwenye front page ya gazeti Bilioni 300 zaibwa kimafia Dar.

Huwezi ukawa una ripoti serious news kama udaku wa kwenye gazeti la Kiu ama Ijumaa. Ndio maana credibility ya print media zetu imeporomoka sana, kila habari unayosoma unagundua mwandishi hakufanya homework vya kutosha.

Cha ajabu hata 'reported news' kama za press conference, kunakuwa na mapungufu. Mara kadhaa tumekuwa tukishuhudia taasisi na watu binafsi wanaofanya press conference wakirudi tena kurekebisha habari zilizokosewa kuripotiwa.

Je hawa wanaojiita ma editors wana kazi gani? Hao na wenyewe ni makanjanja???[/QUOTE]
Mkuu umenifurahisha sana. Unachosema ni sahihi kabisa kwamba ni lazima sote tuanze kuwa makini katika yale tunayoyafanya. Hii habari kama ni kweli basi inatia doa kubwa kwa mara nyingine tena, kwa uchumi wa Taifa letu, na ninaona kama vile bado tumelala sana bila kujua kwamba tukiendelea na usingizi huu, wajanja watatubia mpaka tufilisike.
 
Back
Top Bottom