Bilioni 300 zaibiwa kimafia Dar

Habari za huo wizi zimeandikwa katika gazeti la Mwananchi la leo http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18659. Kama ni kweli basi Tz inatisha.

Kwa faida ya wote.

NI MARA TATU YA WIZI WA EPA;DCI MANUMBA ASEMA TAARIFA ZINAFANYIWA KAZI
Ramadhan Semtawa

WATU wasiofahamika wameghushi nyaraka za malipo na kuiba zaidi ya Sh300 bilioni katika benki tatu kubwa nchini na kusababisha mtikisiko mkubwa katika sekta ya fedha, uchunguzi umeonyesha.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, fedha hizo ziliibwa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni kabisa mwa mwaka huu, kwa njia ya mtandao wa kompyuta na kuhusisha wezi wa kimataifa ndani na nje ya nchi.

Tukio hilo ambalo ni kubwa kuwahi kutikisa sekta ya fedha nchini tangu uhuru mwaka 1961, limetokea katika kipindi cha takribani miaka miwili tangu serikali ianzishe kitengo maalumu cha Intelejensia cha kufuatilia Mzunguko wa Fedha chafu (FIU).

Licha ya kuwepo FIU, ambayo iliundwa pamoja na Sheria ya Kupambana na Fedha Chafu ya mwaka 2007, uchunguzi wa Mwananchi, umebaini kutokea wizi huo mkubwa katika benki hizo.

Uchunguzi huo umebaini kwamba, taarifa za awali zinaonyesha fedha hizo ambazo ni mara tatu ya zile za EPA zilizoibwa katika Benki Kuu Tanzania (BoT), zilihamishwa kwa njia ya kompyuta kwa kughushi malipo kwenda kwa wahusika wa mtandao huo katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani ambako Polisi wa Kimataifa wa nchini na wenzao wanahaha kuzichunguza.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, alipoulizwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, alithibitisha kuwepo taarifa za uhalifu huo, lakini akaweka bayana, hakuna ushahidi wa kiwango maalumu kilichoibwa hadi sasa.

"Hizo taarifa zipo zinafanyiwa kazi, ila haijathibitika ni kiasi gani cha fedha kimeibwa na benki zipi hasa, kwa hiyo kusema ni Sh300 bilioni au zaidi ya hapo, si sahihi hakuna uthibitisho wowote," alifafanua DCI Kamishna Manumba.

DCI Manumba aliongeza kwamba, baada ya uchunguzi kukamilika polisi itatoa taarifa za kina, sahihi na kwa wakati kwa wananchi na kusisitiza, "Kwa sasa ngoja tufanye kazi."

Hata hivyo, DCI Manumba alionya na kuzitaka benki na watu wengine kuwa makini katika kuangalia usalama wa mali na fedha katika kipindi chote.

"Unajua, mambo ya uhalifu sisi tunajitahidi kukabiliana nayo lakini bado wengine wanaendelea kwa kutumia mbinu mbalimbali. Kwa mfano tunazuia watu wasibakwe, lakini wanabakwa, hii yote inaonyesha umuhimu wa watu kuwa makini," alifafanua DCI Manumba.

Gavana wa Benki Kuu (BoT) Profesa Benno Ndulu, alipoulizwa kuhusu sakata hilo alisema yuko nje ya nchi kikazi.

"Niko Sweden kikazi, halafu hapa siwezi kukusikia vizuri wala kuzungumza vema kwani kuna shughuli ambayo nimehudhuria," alisema Profesa Ndulu, ambaye taasisi kuu ya fedha ya nchi ina wajibu wa kusimamia benki na taasisi zote za fedha nchini.

Baadhi ya maofisa wa benki hizo ambazo majina yake tunayahifadhi, wamethibitisha kukumbwa na uhalifu huo mkubwa na kwamba wameacha suala hilo mikononi mwa vyombo vya dola.

"Ni kweli kuna vitenfo vya kughushi vimetokea katika benki yetu, lakini hilo hatuwezi kulizungumzia kwa kina kwasababu liko mikononi mwa vyombo vya dola. Polisi wanaweza kulizungumzia hilo," alifafanua ofisa kutoka moja ya benki iliyoibiwa kiasi kikubwa cha fedha karibu Sh100 bilioni.

Wakati DCI Kamishna Manumba, Gavana Ndulu na maofisa wa benki wakizungumzia hayo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba, fedha hizo ziliibwa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni kabisa mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, hadi sasa taarifa za awali zinaonyesha mpango huo mchafu umeanzia ndani ya benki kwa kuhusisha baadhi ya watu ambao ni wanamtandao na wezi wenzao nje ya nchi.

Mwananchi imebaini kwamba, hadi sasa Idara ya Interpol Tanzania kwa kushirikiana na wenzao wa nje wanafanya uchunguzi huo wa kina katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani ambako taarifa za awali zinaonyesha fedha hizo zilikwenda.

Katika uchunguzi huo, Mwananchi imebaini kwamba baada ya mpango huo kufanywa nchini fedha hizo zinaonyesha zilihamishwa kwa njia hiyo ya kughushi kwenda nchi hizo.

Vyanzo hivyo vya habari za kiuchunguzi, zilifafanua kwamba baadhi ya watu katika mabenki hayo ambao wanafahamu mzunguko wa fedha ikiwemo malipo ya ndani na nje, wamepanga njama hizo na kughushi malipo kwa kushirikiana na mtandao mkubwa wa wezi wenzao wa nje ya mabenki ndani na nje.

Habari hizo za kiuchunguzi, zinaonyesha kwamba wizi huo umetikisa mabenki hayo kiuchumi huku duru za kiusalama zikisema vyombo vya usalama vimekuwa makini kuangalia fedha hizo zimeingia mikononi mwa watu gani.

Mwananchi imebaini kwamba, kiasi hicho kikubwa cha fedha kinaweza kuweka usalama wa taifa hatarini endapo kitakuwa kimeingia kwenye mikono ya watu ambao wana nia mbaya na nchi.

"Ni kiasi kikubwa cha fedha, kama kitakuwa kimeingia kwenye mikono ya watu hatari wanaweza kuhatarisha usalama wa nchi, bilioni 300 si kitu kidogo," kilisema chanzo kimoja kutoka moja ya vyombo vya usalama.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kitisho kingine kinachoangaliwa hadi sasa ni iwapo fedha hizo zimeibwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba kwa ajili ya kundi fulani ikiwemo mafisadi kutaka kuzitumia kutimiza malengo yao.

"Tunaangalia pia, maana inawezekana ni mafisadi wakubwa ambao wanajua mzunguko wa fedha ndiyo wamekula njama na kutaka kuhujumu nchi kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu," kilifafanua chanzo hicho.

Ingawa haijathibitika, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kuliibuka ufisadi mkubwa katika BoT ambao zaidi ya Sh 133 bilioni ziliibwa.
 
Kwa faida ya wote.
Abdulhalim!
Kila siku nalia na sera mbovu za kifedha walizoparamia Ruksa na Mkapa. Wale wote kwao uchumi ulikuwa ni sawa ndoto ya mchana. Mwinyi was and still is a frustrated teacher na hata last year alichapwa kofi na kijana anayepaswa kuwa mjukuu wake simply kwa kushindwa kuusoma mhadhara. Wakati Mkapa akiwa ni mwandishi wa habari mlevi wa hovyo na mpenda wanawake japo bunduki haina risasi.(ni baruti) tu .Dunia nzima hakuna nchi amabyo haina control on forex transactions its only tanzania.Narudia this is only the tip of the iceberg na tutarajie mengi mpaka tutie akili.We should borrow from the past on import licence;export licence and harmonize bank transactions under the control of new BOT. Vinginevyo inakula kwetu mkimwambia Manumba what can he do with his very poorly motivated cops!!! Mkulo na swahiba wako Kikwete acheni kuhudhria mdundiko na hitma hapa na ughaibuni pasueni bongo wacheni mchezo kwani kazi mbaya iatawasuta hata makaburini!!
 
Hata mi nashangaa hapa. The whole thing sounds fishy, miela yote hiyo kuibwa in a nick of very time kwenye uchaguzi 2010?? Je ni kweli tuna system hopeless kiasi fedha nyingi kiasi hicho inachotwa ktk kipindi kifupi??

We are cursed and doomed to death.
 
Tanzania tunadekeza maovu. Hizi pesa zimeibiwa na watu wanaofanya kazi ndani ya benki zetu wakishirikiana na marafiki zao ndani na nje ya nchi. Hii imetokana na nchi kuwa na sera ya kulea na kukumbatia maovu. Katika sakata la EPA, Richmond na Kiwira serikali haijachukuwa hatua zozote za maana kuonesha kwamba matendo hayo ni machafu na wala wahusika hawakuchukuliwa hatua za aina yoyote, sasa kwanini nao mabenka wetu wasifuate nyayo hizo za wizi?. Ukiiba pesa za kutisha ndani ya Tanzania utalindwa na kupewa heshima zote ndani ya nchi yetu.
 
Hata mi nashangaa hapa. The whole thing sounds fishy, miela yote hiyo kuibwa in a nick of very time kwenye uchaguzi 2010?? Je ni kweli tuna system hopeless kiasi fedha nyingi kiasi hicho inachotwa ktk kipindi kifupi??

We are cursed and doomed to death.
Nilidhani wameanzisga TISS kwa ajili ya kudhibiti mambo kama haya. What is happening jamani?
 
Abdulhalim!
Kila siku nalia na sera mbovu za kifedha walizoparamia Ruksa na Mkapa. Wale wote kwao uchumi ulikuwa ni sawa ndoto ya mchana. Mwinyi was and still is a frustrated teacher na hata last year alichapwa kofi na kijana anayepaswa kuwa mjukuu wake simply kwa kushindwa kuusoma mhadhara. Wakati Mkapa akiwa ni mwandishi wa habari mlevi wa hovyo na mpenda wanawake japo bunduki haina risasi.(ni baruti) tu .Dunia nzima hakuna nchi amabyo haina control on forex transactions its only tanzania.Narudia this is only the tip of the iceberg na tutarajie mengi mpaka tutie akili.We should borrow from the past on import licence;export licence and harmonize bank transactions under the control of new BOT. Vinginevyo inakula kwetu mkimwambia Manumba what can he do with his very poorly motivated cops!!! Mkulo na swahiba wako Kikwete acheni kuhudhria mdundiko na hitma hapa na ughaibuni pasueni bongo wacheni mchezo kwani kazi mbaya iatawasuta hata makaburini!!

You are right, quite right! Halafu Meghji alipokuwa Waziri wa Fedha alipiga marufuku makampuni kutoza dola za Kimarekani kwenye ankara zao, ila bado hakuna utelezaji. Yaani hii nchi ina sheria zisizokuw ana meno kabisa!
 
Nilidhani wameanzisga TISS kwa ajili ya kudhibiti mambo kama haya. What is happening jamani?

EPA wameona aibu unafikiri pesa za uchaguzi wanatoa wapi jamani;....
hivi mnafikiri yule raisi alikuwa mjinga kusaini Ule muswaada...hiyo mwanzo
KIDUMU CHAMA CHA MAJAMBAZI
 
abdulhalim!
kila siku nalia na sera mbovu za kifedha walizoparamia ruksa na mkapa. Wale wote kwao uchumi ulikuwa ni sawa ndoto ya mchana. Mwinyi was and still is a frustrated teacher na hata last year alichapwa kofi na kijana anayepaswa kuwa mjukuu wake simply kwa kushindwa kuusoma mhadhara. Wakati mkapa akiwa ni mwandishi wa habari mlevi wa hovyo na mpenda wanawake japo bunduki haina risasi.(ni baruti) tu .dunia nzima hakuna nchi amabyo haina control on forex transactions its only tanzania.narudia this is only the tip of the iceberg na tutarajie mengi mpaka tutie akili.we should borrow from the past on import licence;export licence and harmonize bank transactions under the control of new bot. Vinginevyo inakula kwetu mkimwambia manumba what can he do with his very poorly motivated cops!!! Mkulo na swahiba wako kikwete acheni kuhudhria mdundiko na hitma hapa na ughaibuni pasueni bongo wacheni mchezo kwani kazi mbaya iatawasuta hata makaburini!!

ndugu yangu ukilaumu maraisi mwinyi na mkapa utakuwa hujawatendea haki, sio kila uzembe walaumiwe maraisi, huyo raisi atafanya mambo mangapi nchi hii?
Kwani hana wasaidizi wakumsaidia ktk vitengo husika?
Kwanini hao wasaidizi wasilaumiwe?
Hizi benki ndio za kupaswa kulaumiwa na bot.
Mifumo yao ya kiutendaji ni mibovu kabisa!!
Kwani hizo benki si zina wahusika wa hivyo vitengo vya forex transactions ?
Kwanini wasibanwe hao wahusika moja kwa moja kuhusika na huo wizi ?
Kama wao hawahusiki wataje nani kahusika .
Kwanini unamuona mwizi yule halafu unazunguka mbali kumtafuta nani kaiba?
Mambo ni very clear kitengo chochote uzembe ukitokea walio ktk hicho kitengo wanakamatwa.
Mfano liyumba alikamatwa sababu yeye ndio alikuwa mkuu wa kitengo cha bot kilichohusika na ufujaji wa pesa za ujenzi ktk majengo ya bot.
Mfano mfumo wa kiutendaji wa barlays benki unaniibia hata mimi mlalahoi vijipesa vyangu kwenye akaunti sembuse hayo majipesa makubwa yanayozagaa zagaa kwenye masefu yao?
Pia wote tuliona ktk magazeti wafanya kazi kibao wa barclays walikuwa na kesi ya kujibu kuhusika na kuibia benki na wateja sijui kesi yao ilikuja kuishia wapi.
Conclussion wakamatwe wakuu wa vitengo wabanwe mpaka wajikojolee wataje muhusika nani.
China ukikutwa na kesi ya kuibia umma unanyongwa hadharani!
 
Back
Top Bottom