Bilioni 30.9 ku upgrade ukumbi wa Bunge

Uamuzi MZITO na wa MAANA aloowahi kuufanya Spika Sitta ni ule wa jana wa kuiruhusu TBC1 iendelee kuonyesha kombe la dunia badala ya mijadala ya hovyo, isiyo na manufaa wala tija kule bungeni.
 
Nimejitahidi kuisoma hiyo habari ila sijaona sehemu ilipoandikwa gharama ya ku_upgrade.Hiyo 30.9bn imewekwa kama gharama ya ukumbi huo kwa sasa.Au mimi ndo sijaelewa.Sum1 to help!
 
Nimejitahidi kuisoma hiyo habari ila sijaona sehemu ilipoandikwa gharama ya ku_upgrade.Hiyo 30.9bn imewekwa kama gharama ya ukumbi huo kwa sasa.Au mimi ndo sijaelewa.Sum1 to help!

You are right...baada ya kuisoma vizuri news hiyo, haisemi ukarabati mpya utagharimu Bil 30.9.... japo haisemi pia ni kiasi gani kitatumika kugharamia.

Hata hivyo, bado umuhimu wa kutathmini in the face of many challenges zilizopo, kwenda HIGH-TECH ni priority kwa sasa....whatever the cost..
 
Title haiendani na habari yenyewe! Ukumbi ulijengwa kwa TSh 30.9 bn/-, lakini up-grade haijasemwa itagharimu TSh ngapi! Inawezekana ni kwa vijisenti vya TSh 1bn/- (ambavyo Andrew Chenge anaweza kutupatia toka Offshore account yake)! Pressure yote ya nini wajameni?
 
tayari kuna wenye akili hapo wameishajihakikishia percent fulani kwenye huo mradi.....mh. fuya kimbita naye kishapata vijisenti vya kumgaragazia mbowe kwa kanga na kofia ........ afadhari wazenji wajitenge labda siku moja watafanikiwa kuondoka mkiani mwa umasikini..... huku bara naona tuna contract ya muda usiojulikana na umaiskini...... visa vya kasi mpya za kitoto za kujivunia pipi vinatutosha sasa...... naona hapa TZ ukiwa mzalendo kupata ugonjwa wa moyo ni saa yoyote......
 
Ukumbi ule ulijengwa na wachina kwa mabilioni ye fedha na kufunguliwa mwaka 2006, yaani juzi juzi tu; sasa kumeharibika nini tena katika kipindi hiki kifupi namna hii kuhitaji hela nyingi kiasi hicho?
 
hivi tumewakosea nini hawa viongozi wetu? mbona wanatuadhibu kiasi hiki?


unatenga billioni 30 ya ku-ugrade ukumbi wa bunge wakati mahospitali hayana madawa,hakuna vitanda vya wagonjwa,mashule hayana madawati au majengo yanayofaa.


inamana maisha ya watoto wa shule na wagonjwa hayana maana sana lakini wanasiasa wao wanapewa kila haina ya vitu vya starehe lakini kazi ndio zero,hakuna cha maana wanachoongea kwenye lile jengo zaidi ya kupiga makofi na kucheka cheka hovyo.
 
kinachoshsangaza awa watu ni hali ya viongozi wetu kijilinganisha na wa nchi za ulaya wakati wao ni wa nchi za dunia ya tatu! si lazima bunge letu lijiendeshe kwa teknolojia kama la uk au uko scotland! kwani kila teknolojia lazima uipate, si linategemea na uwezo pia? mbona inapokuja kwenye suala la maslai ya wananchi wa kawaida serikali ndio iko mbele kujitambulisha kua ni nchi ya kimasikini, mishahara tu ya tucta tunakumbuka jinsi check bob wetu alivyoshupaa kuelezea jinsi tulivyo masikini kua hatuwezi lipa mishahara iyo hata miaka 8 ijayo!!!!!!!!!! lakini kwenye kujenga ukumbi wa bunge wenye state of the art technology pesa is always there, ama kweli ukistaajab ya musa ..................
 
Title haiendani na habari yenyewe! Ukumbi ulijengwa kwa TSh 30.9 bn/-, lakini up-grade haijasemwa itagharimu TSh ngapi! Inawezekana ni kwa vijisenti vya TSh 1bn/- (ambavyo Andrew Chenge anaweza kutupatia toka Offshore account yake)! Pressure yote ya nini wajameni?

In ur dreams! In this country of selfishness and corruption, where tenders are made for pure financial gains...i wldn't be surprised to hear it costs more than the amount used to build it!!
 
Sasa mbona title ya thread imekaa kiuptoshaji jamani???????????....Kama vp ibadilishwe basi maana gharama za kujenga ukumbi ndo hizo Tshs.330.9 bil na si gharama za ku upgrade.......Title/heading ibadilishwe
 
Mwaka 2015 majimbo ya ubunge yatagawanywa tena na hilo jengo la bunge itabidi lipanuliwe upya. Na ofcourse technolojia inakua nayo itazidi kuhalalisha hilo la uvunjaji/ukarabati.

Mungu atupishe na matumizi haya yanayochefua ya pesa zetu.
 
nilishtuka kusoma heading .......................nikajua tumeliwa wazi wazi kwa mara nyengine tena ....kumbe gharama za ukarabati bado kutajwa.

najua hii inanipa faraja ya muda tu, manake hiyo gharama ya ukarabati yaweza kutajwa kubwa kuliko bilioni hizo!
 
Sasa nimetambua kwa hakika kuwa tatizo lipo kichwani mwa wabunge wa Bunge letu. Na hatimaye tatizo lipo kichwani mwa watanzania.
Viongozi wabovu wanachaguliwa kutoka katika jamii mbovu. Viongozi wabovu wanachaguliwa na wapiga kura wabovu, wasio na uelewa mpana, wenye upeo finyu, na wasio na nia ya dhati kuudhibiti umaskini wao!
Mifano ipo mingi tu, wananchi wanaona matatizo haya yote lakini utashangaa wakiohongwa kidogo tu, wakati wa uchaguzi wanakuwa wamesahau matatizo haya yote na kujidai eti watu fulani ni machaguo ya Mungu! Shame on you all! Hakuna chaguo la Mungu anayeweza kukubali watu wafe kwa kukosa huduma bora za afya, elimu na miundo mbinu ili eti wabunge wakae na kuendesha shughuli zao pahala bora kuliko wabunge wengine wooote africa! Labda kama huyo mtu ni chaguo la mungu wake na mkewe, na wanae na maswahiba wake, kijiweni kwake, lakini sio Mungu tunayemjua asiyependa uchafu na dhuluma.
Biblia inaandika, "....asiyewajali watu wa nyumbani mwake ni mbaya kuliko aliye ikana imani!...." Je, kwa kutojali huku kunakofanywa na Viongozi wetu, tunathubutuje kuwaita eti ni machaguo ya Mungu? Jibu ni rahisi tu, aidha viongozi hawa ni maswaiba wao ama akili zetu hazina akili!
Mtu mwenye akili hawezi kuwalaza watoto njaa kisa eti akanunue suti mpya ili awashinde jirani zake ama ili aendelee kushikilia rekodi mtaani kwao kwa kuwa na suti ya kisasa zaidi! Huyo lazima awe ZUZU, kama alivyosema hayati Babab wa Taifa!
Hiyo cha mtoto, tuje kwenye hao wabunge wenyewe sasa!
Sasa hivi wapo 340 wanatakiwa kuongezeka hadi kufikia 360! Tujiulize, tumefanya tathmini kujua hao 340 wamezidiwa na kazi ipi inayohitaji kuongezeka kwa hao wengine 20? Mbona wakati wa mwalimu Nyerere wabunge walikuwa wachache kuliko hawa, miundo mbinu mibovu kuliko hii, mashangingi hayakuwepo lakini wabunge hao waliweza kwenda kushughulika na kero za wananchi na wananchi wakaridhika. Sasa kuna miundombinu bora zaidi, mashangingi yapo, ukumbi wa bunge bora kuliko zamani, kero za wananchi bado sipo vile vile halafu eti mnataka kuongeza idadi ya wabunge, kuufanya ukumbi wa bunge kuwa wa kisasa zaidi. Najiuliza: Ili nini?
Ili walale zaidi na kusinzia? Ama kwa vile ni wengi wa wabunge ni wazee, it is therefore necessary to make them as comfortable as possible?
Na isitoshe, mashangingi yenyewe waliyopewa tunayaona mjini yamejazana yanatuletea foleni tu barabarani na hayatumiki tena kwenda huko majimboni kukutana na wananchi kama inavyopasa instead yanatumika kujenga heshima na sifa za kijinga mjini! What a shame?????????
Watanzania wenzangu, we are deep in some serious shit here, something needs to be done and done quickly, kila mmoja ajiulize tu kwa nafasi yake anatakiwa kufanya nini!
 
Sisi ni Mabingwa wa kuweka rekodi katika hali ya umaskini komavu,

1. Nchi ya kwanza Afrika kuialika timu ya brazil kucheza kwenye ardhi ya afrika.

2. Nchi ya kwanza afrika mashariki na kati kuwa na bunge zuri, kubwa la kisasa linalotunga sheria za kizamani.

3. Nchi ya kwanza afrika ambayo ilitoa kiongozi aliyekutana na Raisi Obama.

4. Nchi ya kwanza africa ambayo raisi wa marekani aliishi karibia wiki.

5. Nchi ya kwanza afrika ambayo ina rekodi nyingi lakini wanachi wake ni dhoofu bin hali

Mwenye rekodi nyingine anakaribishwa.

6.0 Nchi ya kwanza duniani kuwa na WASWAHILI WENGI
 
Sisi ni Mabingwa wa kuweka rekodi katika hali ya umaskini komavu,

1. Nchi ya kwanza Afrika kuialika timu ya brazil kucheza kwenye ardhi ya afrika.

Zimbabwe ipo bara gani mkuu?
Anyway ingawa gharama za kukarabati ule mjengo bado hazijawekwa hazarani but i bet zitakuwa ni mamilioni mengi kama kawaida.
Sita anaona anafanya jambo la kishujaa kwa kuukarabati ule ukumbi.
 
Mimi siamini kuwa lengo hasa ni kukarabati ukumbi, bali ni njia ya kupata pesa kwa ajili ya uchaguzi wa octoba. Naona ccmimekosa sehemu ya kupata pesa, ndo maana wakaona ni vyema watumie hiyo njia.

Mbona matatizo Kama matibabu, Waaalimu na wafanyakazi wengine hayapewi kipaumbele kama hili?

NAONA KUNA AMRI KOTOKA JUU.
 
kilichopungua bungeni siyo vitendea kazi bari vichwa vyenye umakini wakati wa wa kufikiri...kwa hiyo kinachotakiwa ni ku replace wabunge waliopitwa na wakati siyo vifaa vya kisasa.... ufanisi wa bunge utatokana na akili za wabunge siyo jengo lenye vifaa vya kisasa wala mashangingi ya kileo
 
Back
Top Bottom