Bila kazi yako,biashara yako,utaweza kudumu kwa muda gani?

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Feb 3, 2010
230
57
waTanzania tunajitahid kufanya kazi. Wengi wetu tumeajiriwa,wengine wamejiajiri wenyewe na wengine kama wachaga na wakinga wanajishughurisha na biashara.
Hoja yangu ni juu ya nin kinaweza tokea duniani. Fikiria umeenda kazini ukakuta barua ya kuachishwa kazi,au umeenda kwenye biashara yako ukakuta moto ndo unamalizia paa za duka lako...Je katika kipindi hcho utaweza kustahimil maumivu ya maisha? Shime waTanzania tujijengee tabia ya kuweka akiba ili hata ukipata matatzo tajwa hapo juu,tuweze ishi walau mwaka mmoja na zaid.. Offer za bia 2zitoazo bar na starehe zngne hazitusaidii kitu..
Wasalaam rafiki yenu mpendwa
 
Una akali sana. Watanzania hatuna utaratibu wa kujiwekea akiba. Inafikia wakati ukiimwa ndugu wanachanga uende hospitali, achilia mbali magonjwa makubwa hata vigonjwa vidogo vidogo unasaidiwa.

Asante kwa kutukumbusha!
 
Back
Top Bottom