Bil64za sikuku ya uhuru na harakati za kuongeza posho wakati wal.300 wanasotea mshahara wa november

Rumishaeli

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
227
72
Walimu 300 ‘wasotea’ mishahara ya Nov Send to a friend


Daniel Mjema,Moshi
ZAIDI ya walimu 300 katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, hawajalipwa mishahara yao ya mwezi uliopita.Habari zilizolifikia Mwananchi jana zilisema kwa kawaida walimu hao walipaswa kupata mishahara yao kati ya Novemba 28 na 30.

Hata hivyo walimu waliopiga simu katika gazeti hili, walilalamikia usumbufu kila wanapokwenda benki na hawaelezwi kiini hasa ni nini cha tatizo hilo ni nini.

Habari hizo zilisema walimu walioathiriwa na tatizo hilo ni wale wanaopokea mishahara yao kupitia Benki ya NBC.

“Tumekwenda benki zaidi ya mara 20 tunaambulia patupu tukiuliza tunaambiwa tumuulize mwajiri wetu tunashindwa kuelewa nini kimetokea,”alisema mmoja wa walimu hao.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Bernedetta Kinabo, alikiri kuwapo kwa tatizo hilo na kwamba linafanyiwa kazi kwa uzito mkubwa.

“Ni kweli kwamba walimu 300 hawajapata mishahara yao, kuna makosa yamefanyika na tumeshawasiliana na benki ili tuyarekebishe,”alisema.

Kinabo aliwataka walimu hao kuvuta subira kwa sababu tayari tatizo limejulikana na linarekebishwa haraka ili waweze kupata mishahara yao katika kipindi kifupi kijacho.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) katika Manispaa ya Moshi, Abdalah Kaumba, alisema tatizo lipo kati ya Benki za NBC na NMB.

Kaumba alisema halmashauri ilitekeleza wajibu wake wa kupeleka hundi ya mishahara kupitia NMB lakini kuna tatizo katika kuhamishia fedha benki nyingine.
SOURCE MWANANCHI Wednesday, 14 December 2011 20:17
 
Hii ndo Tanzania ndugu yangu..........Wanagawiana maposho na maishahara minono eti kisa kupanda kwa gharama za maisha...HIVI HUO UGUMU WA MAISHA HIVI SASA NI KWA WABUNGE TUU?HAO WALIMU NA WATUMISHI WENGINE WANAOLIPWA KIMA CHA CHINI,SIO RAIA WA NCHI HII?WAKATI A KUKAA KIMYA UNAPASW KUKOMA SASA,TUAMKE TUUKATAE HUU UNYONYAJI KWA VITENDO.
 
Jamani Walimu tuvumilieni kidogo katika hili, kwani tarehe 68 tayari imefika? Mbona mnakosa uzalendo hivi nyinyi vijana wa miaka hii?
 
Hamna kuwalipa kwa wakati maana walimu ikifika wakati wa kampeni huwa wanapewa hela za rushwa kisha wanaanza kujichelesha na kusema hakuna chama chenye sera bora kama ccm, vingine vyote ni vya kiukoo na kadini. Serekali ya ccm shikilia hapohapo mpaka tuheshimiane. Walipe mara moja kwa miezi miwili ili wakati wa kura watie akili. CCM hoyeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom